Wakuu habari yenu
Naomba mwenye uelewa wa teknolojia ya namna ya kufanya biashara ya kukopesha simu . Nataka kufanya hii biashara ila nashindwa pa kuanzia.
Natanguliza shukran
Mkuu ipo hivi kuna njia mbili za kufanya hii biashara,
Njia ya kwanza, ni kuwa wakala wa kampuni hizi wanazokopesha simu, ambapo utafungua duka la simu hapa utaweka vitochi ila upande wa smartphones wanakuletea hawa guruz wa loan phone, unalipwa kadri unavyopush mauzo, unaweza ukajiongeza kwa kuweka vijana wako wa kupush mzigo wako mtaani hata kwa kutumia bodaboda. Hi njia mtaji wake ni mdogo hadi zero, yaani unaweza ukaanza na mtaji zero.
Kampuni maarufu kwa sasa ambazo unaweza ukawa wakala ni
Onfon Microfinance, Watu Credit, Easy Buy, SunKing, Dlight, n.k.
Njia ya pili ni kununua software kutoka china, kisha unanununua na mzigo wa simu kutoka china kama contena moja hivi kisha wataalamu wa IT wanafanya installation za hiyo software kwenye hizo simu zote, hiyo software ndio inacontol mfumo wa simu, kukopesha, taarifa za mteja, n.k , hii inaitaji mtaji mkubwa zaidi, inaitaju uwaajili watu zaidi, n.k.
Kama utaitaji connection kati ya hizo njia unaweza kunicheki, vigezo na masharti kuzingatiwa.
T&C applied.