Mwenye uelewa kuhusu bidhaa za simu Used za Nje Almaarufu "Used from Abroad"

Sheikh23

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,128
1,842
Habari ,nimeshawishika kutaka kununua simu used from abroad ambazo zinauzwa na kunadiwa mitandaoni, hii ni kutokana na kigezo kimoja tu cha bei, kwani nyingi ni za viwango na ni za matoleo ya hivi karibuni, pia bei zake ni affordable ukilinganisha na bei ya simu hizo kama utazinunua kwenye masoko yetu ya kariakoo au makumbusho na kwingineko.

Naomba shuhuda za ubora haswa wa betri (battery life) na mambo mengine uliyo observe baada ya kutumia simu hizo.

Natanguliza shukrani kwenu.
 
Simu used ni bahati nasibu, kuna wanaocheka na wanao lia ila kama unapenda za hivyo chukua iphone zina unafuu ukilinganisha na wenzake, usichukue simu za miaka mingi iliopita mfano simu za 2019 kushuka achana nazo ila ya 2020 waweza chukua
 
cha muhimu ni warranty mkuu, Pia na warranty inasemaje na itakusaidiaje pale unapopata shida.. Warranty ikiwa ya uhakika... lazima huduma na bidhaa itakuwa nzuri, maana kuna wengine wanauza "refurbished" kwa kuzi lable kama used kutoka nje.
 
Habari ,nimeshawishika kutaka kununua simu used from abroad ambazo zinauzwa na kunadiwa mitandaoni, hii ni kutokana na kigezo kimoja tu cha bei, kwani nyingi ni za viwango na ni za matoleo ya hivi karibuni, pia bei zake ni affordable ukilinganisha na bei ya simu hizo kama utazinunua kwenye masoko yetu ya kariakoo au makumbusho na kwingineko.

Naomba shuhuda za ubora haswa wa betri (battery life) na mambo mengine uliyo observe baada ya kutumia simu hizo.

Natanguliza shukrani kwenu.
Kua makini nyingi ni REFURBISHED au za WIZI wana zi label kama USED from Abroad... Na bora upate inayosumbua software unaweza solve kirahisi sio upate mbovu hardware au vyote kwa pamoja utalia... Kama una hela na unapenda simu used fanya tu kuagiza mwenyewe eBay utasubiri walau 3 weeks au mwezi inategemeana na usafirishaji...
 
Back
Top Bottom