Simu Mpya vs Simu Used

Big Phil

Member
Nov 20, 2019
50
338
Unahitaji kununua simu mpya lakini kwa bei hiyo hiyo unakutana na simu used yenye uwezo mkubwa zaidi ya mpya. Unabaki njia panda

Maamuzi sahihi ni kununua simu mpya na maamuzi sahihi ni kununua simu used. Namaanisha

SIMU-MPYA
inakuhakikishia kuwa wewe ndiye mtu wa kwanza kuitumia kutokea kiwandani hivyo inakuja na Warranty ya miezi 12 hadi 25.

Pale itakaposhikwa na tatizo lolote ambalo hujalisababisha wewe unaweza irudisha na ikapokelewa na kurekebishwa na kurudishiwa Kubadilishiwa. Pia kuna kampuni zinatoa mpaka Warranty ya kioo kupasuka pia kuna issue ya hizi simu za laki 1,2,3,4 kustuck

kawaida kama ya simu mpya ila kuna limitation Mfano unauziwa simu unaambiwa usiifanyie software update mara nyingi hizi huwa ni kwenye zile Chinese version zikizowekwa Google services kwa njia za mkato ukiupdate tuh zote zinapotea kuzirudisha pia kuna uwezekano zisirudi tena.

SIMU-USED
napo siku hizi sio kinyonge unauziwa simu na unapewa na Warranty card nyingi huwa ni miezi 6. Warranty inafanya kazi. Kwa kipindi icho hizi huwa kwenye simu nyingi za Huawei na Xiaomi.

Kwenye hizi Google Pixel muuzaji anakupa uhuru wa kufanya kila kitu, kuna ile imetokea umeupdate Pixel yako kwenda Android 12 lakini unakutana na bugs nyingi (changamoto).

Hii sio serious issue sana kwasababu hizo changamoto za software huwa zinatokea kwenye simu zote ni mteja kuwa mvumilivu kusubiria correction update ya kuja kufix hizo changamoto na huwa hawachelewi kutuma hizo updates.

CAMERA
Kwenye Camera zina uwezo mdogo sana kulinganisha na Used. Tuchukue

Mfano Xiaomi Redmi 10C, Samsung A12, Oppo A16k na Infinix hot 12i hizi ni simu z budget ya laki 3 zimetumia camera sensors zilizotengenezwa na makampuni yasiofahamika na ni unnamed ikiwa na maana Kuwa ni cheap components.

Tukiangalia simu used za bei hiyo ni Google Pixel 3 hii imetumia Camera sensor kutoka kwenye kampuni kubwa ya SONY inayoitwa Sony Exmor IMX363 hizi ni expensive inapiga picha ukali hii simu mpya yake pale Marekani ni Tsh. 950K huku used unauziwa 350K

PERFORMANCE
Hapa simu mpya zote hazioni mbele za laki 2,3,4 zaidi ya 95% zimetumia MediaTek Helio hizi ni processor za hovyo simu kustuck ni kawaida, zinaifanya simu iogope kupokea update mfululizo.

Used kama Pixel 3 ina Flagship Chipset ya Snapdragon 845 simu ilotoka ikiwa na Android 9 now ina Android 12 speeds test yake ni kiwembe kulinganisha na hizi mpya za bei hiyo.

Au Huawei P40 Pro 5G used yake ni 950K alafu tuilinganishe na Xiaomi Mi 11 lite 5G NE au Samsung A53 5G bado simu bora ni P40 Pro na tena ipo level nyingine kabisa.

DISPLAY
Simu mpya tena hapa zinapoteza hili pambano kizembe sana, "Always Simu Pro italinganishwa na Pro" simu mpya za laki 2,3,4,5 zaidi asilimia 95% zimetumia Display za IPS LCD na PLS LCD 720x1612 pixels

Kwa laki 5 kuna Samsung S10 yenye Display AMOLED HDR10+ 1440x3040 pixels.
Humu used zinapiga mwingi mno na tena ikiwa ni Samsung S na Note series ndio basi tena.

BATTERY
Ndipo sehemu simu mpya zinapoupiga mwingi ukiachana na battery zenye ukubwa wa 4000mAh - 7000mAh kwenye hizi simu bado ndizo zinazoongoza kutunza chaji kwa muda mrefu.
Simu used hizi za chini ya 2019 kwenye upande wa battery huwa hazipo njema sana nyingi zina 2000mAh - 4000mAh.

HARDWARES
Simu mpya huwa zinatumia cheap materials kwenye utengenezaji wake ukilinganisha na used kwa kutumia kigezo cha ufanano wa bei. Ukikaa sehemu ambapo kuna network ya shida ni rahisi hizi simu za bei rahisi kupoteza signal kuliko hizi used.

Pia simu mpya ni dhaifu kwenye board zake kulinganisha na hizi used
Simu used bei zake rasmi kwa kipindi zinavyoingiza sokoni huwa zinafikia zaidi ya mara 5 inategemeana na muda ambao simu imechukua kukaa sokoni.

Kwa hii comparisons niliyoifanya inaonyesha ni bora ununue simu used. Lakini kila wiki simu mpya zinaingizwa sokoni kwa budget zote kuanzia 200K - 4m na zinanunuliwa kwa idadi kubwa.
 
Sitasahau siku niliyo nunua galaxy S10+ used dukani kwa 700k na warranty yake ya miezi sita matatizo iliyo kua nayo yalinifanya niirudishe siku hiyohiyo mahali nilipo nunulia simu used ubahatishe nyingi vimeo ndio maana zikauzwa tena
Ilikuwa na shida gani?

Na ulipoirudusha waliipokea na kukurefund?
 
Mzee nmedaka used note10+ ni noma na nusu Kwanzaa ni mpyaaa kila kitu kasoro box tu
 
Back
Top Bottom