Hahaha,mkuu nimependa umevyojieleza.Maana ukitaja pesa watu haoo.
Nakushauri ukinunua jaribu kuwa na fundi,maana hivi vigari sio siri vinapindwa kuliko uwezo wake.
Sasa kama ukiingia kichwakichwa kwa kuangalia bodi basi imekula kwako.Na Ukimpa Dereva akijua ni kibovu kila siku ni kesi.
Hesabu yake kwa wiki sio mbaya,nikweli utapata mkate wa kila siku.
Lakini ungeweka Budget yako ingesaidia kufanya uchaguzi sahihi,maana hizi gari wengi hawazitii sokoni na wakizitia sokoni basi kipo Taabani.
Usala Jingine,nunua zile za taa za square ukinunua zile za duara ni mashaka matupu,na iwe Four wheel drive ndio bora zaidi.