MWANASIASA HURU
Senior Member
- Oct 4, 2012
- 180
- 240
Wadau habari zenu, natumai nyote hamjambo kabisa.
Mimi ni mkazi wa huku kigamboni, ni kijana na nina familia. nina wazo ambalo naona linaweza kufanya kazi.
Kama kuna mtu mwenye shamba maeneo ya kigamboni lakini ameliacha bila kulifanyia chochote kwa muda huku akisubiri mambo yake yakae sawa naomba tuonane tuandikishane mimi niwe mtunzaji wa shamba huku nikilitumia kupata chochote.
Najua wapo watu wenye maeneo yao wamewekeza na wanasubiri mambo yao yakae sawa ndo waendeleze. nitalitunza kwa maana ya uangalizi wa karibu huku nikilima kujipatia riziki kulingana na asili ya shamba lenyewe.
Naamini mimi ni mtu mwaminifu lakini licha ya hilo tunaweza kuandikishana ili kuepuka 'ningejua' na 'sintofahamu'.
ushirikiano ni muhimu sana.
Ahsanteni na naomba kuwasilisha.