Mwenye nyumba kauza bado tupo ndani, mkataba haujaisha; tumchukulie hatua gani?

ESPIRIT

JF-Expert Member
Jul 3, 2014
665
522
Msaada wenu wanasheria, huyu baba mwenye nyumba tuliyopanga kaiuza, tumeenda kwa mjumbe, bado hata haitikii wito wa mwenyekiti. Huyu aliyenunua hataki kutuona wapangaji ifikapo tarehe mosi. Na mimi kwa mfano nilikuw nmelipa kodi hadi September. Je, ndugu zangu wanasheria, mimi sijui sharia. Je nichukue hatua gani nyingine
 
Mikataba gani mlisaini?, najua mikataba ya anyumba inakuwa na notice ya miezi si chini ya mitatu, lakini kwa wewe alipashwa kukurudishia pesa yako na akaupe notisi ya miezi mitatu ya kutafuta nyumba ya kwenda
 
Hiyo hela uliyomlipa ya pango hadi Septemba, una vielelezo au ushahidi wowote au mlipeana tu bila maandishi halali?
 
Msaada wenu wanasheria, huyu baba mwenye nyumba tuliyopanga kaiuza, tumeenda kwa mjumbe, bado hata haitikii wito wa mwenyekiti. Huyu aliyenunua hataki kutuona wapangaji ifikapo tarehe mosi. Na mimi kwa mfano nilikuw nmelipa kodi hadi September. Je, ndugu zangu wanasheria, mimi sijui sharia. Je nichukue hatua gani nyingine
We endelea kukaa na kufanya mambo yko ya kiutafutaji km kawaida. Siku akija mtu YEYOTE anakwambia TOKA huyo ndoo kitoweo chako mahakamani!. Utamshitaki huyo anaekutoa hapo (Enterference with quit enjoyment of Land) kama mlalamikiwa sahihi (proper party) na unamuunganisha na mwenye nyumba (necessary party) kwenye baraza la KATA (km upo wilayani etc) kama upo manispaa, jiji utaenda baraza la Ardhi na nyumba wilaya (DLHT) maana kisheria, mjini mabaraza ya kata hayana uwezo wa masuala ya Ardhi.
 
Back
Top Bottom