Mwenye nyumba atayepandisha kodi 'msimu' huu atakuwa na maruhani kichwani!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,636
2,725
Duh! Kwa jinsi pesa ilivyokuwa ngumu katika 'msimu huu wa tumbua tumbua' tunawaomba wenye nyumba wajizuie kupandisha kodi...
Sisi wapangaji hali zetu ni tete japo hakuna namna lazima mjini tuendelee kuishi, maana hata tukihama hapa huko bara hali ndiyo itakuwa mbaya zaidi vile hapa mjini tumezoea kuishi kidili dili na kupigana tafu.
So yani mtu unajazia jazia kodi itime alafu mwenye nyumba ndio naye anakuja kukuambia kodi imepanda, lazima akapimwe kichwa maana atakuwa hayuko sawa.
Au nyie wadau mnaonaje juu ya hili?
 
Na bado mtatia akili nyumba yangu halafu unipangie nisipandishe kodi wakati mie natekeleza agizo la Rais vijana kama nyie mrudi Shamba mkalime huko sio tunajazana tu mjini hapa
 
Kipindi hiki kigumu wangekubali tuwalipe kwa miezi miwili au mitatu, kuipata kodi ya mwaka mzima ni ngumu kwa mazingira haya.
 
Duh! Kwa jinsi pesa ilivyokuwa ngumu katika 'msimu huu wa tumbua tumbua' tunawaomba wenye nyumba wajizuie kupandisha kodi...
Sisi wapangaji hali zetu ni tete japo hakuna namna lazima mjini tuendelee kuishi, maana hata tukihama hapa huko bara hali ndiyo itakuwa mbaya zaidi vile hapa mjini tumezoea kuishi kidili dili na kupigana tafu.
So yani mtu unajazia jazia kodi itime alafu mwenye nyumba ndio naye anakuja kukuambia kodi imepanda, lazima akapimwe kichwa maana atakuwa hayuko sawa.
Au nyie wadau mnaonaje juu ya hili?
hahahhhahahhahhah kuna ukweli ndani yake
 
Hakuna kitu kizuri kama kuwa na kwako!mambo ya kuishi kiwasiwasi kuhofia mwenye nyumba kupandisha kodi....ni shida
 
Mkuu kama watu wote tukijenga nani atakuwa mpangaji? Kuna kauli kama hiyo. Nadhani uliwahi kuisikia.
Hahaha kweli!kila nauli hiyo huwa inaturudisha nyumba,any way basi serikali ijengee nyumba wananchi wazipange kwa bei nafuu
 
Mkuu kama watu wote tukijenga nani atakuwa mpangaji? Kuna kauli kama hiyo. Nadhani uliwahi kuisikia.
Eti, sie tuache kula vizuri, kuvaa vizuri na kuendesha magari mazuri kisa tunajibana kujenga??? Kujenga ujanani ni uoga wa maisha. Muongeze na hiyo...
 
Back
Top Bottom