Mwenye Nyumba ameleta mganga wa kienyeji anatulazimisha tulambe unga anahisi kuna mchawi kwenye nyumba yake

beatboi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
457
1,125
Habarini ndugu wanaJF,

Baba mwenye nyumba amemleta mganga kutoka kusini huko anadai kwenye nyumba yake kuna mtu anamchezea (mambo ya kichawi), sasa anatulazimisha tulambe ungaunga mweupe nimesikia wanauita 'usembe' ili kumbaini mchawi kwenye nyumba yake.

Binafsi nilikataa kulamba vitu visivyoeleweka na sina hizo imani, ila alinichimba mkwala hadi jtano nimpe jibu nikishindwa nihame kwake.

Dhumuni la kuleta hili jambo kwenu mnipe ushauri wa kufanya sababu alinipa siku tatu ambayo ya mwisho ndio leo na hapa nipo job nafikiria nikirudi home nimpe jibu gani.

Kwa kuongezea tumebaki wapangaji wawili ambao tumekataa kulamba hayo madude yake.

Je, yana madhara yoyote kiafya wataalam wa mambo?
 
habarini ndugu wanajfm,
Baba mwenye nyumba amemleta mganga kutoka kusini huko anadai kwenye nyumba yake kuna mtu anamchezea (mambo ya kichawi), sasa anatulazimisha tulambe ungaunga mweupe nimesikia wanauita 'usembe' ili kumbaini mchawi kwenye nyumba yake. binafsi nilikataa kulamba vitu visivyoeleweka na sina hizo imani, ila alinichimba mkwala hadi jtano nimpe jibu nikishindwa nihame kwake. dhumuni la kuleta hili jambo kwenu mnipe ushauli wa kufanya sababu alinipa siku tatu ambayo ya mwisho ndio leo na hapa nipo job nafikilia nikirudi home nimpe jibu gani.
kwa kuongezea tumebaki wapangaji wawili ambao tumekataa kulamba hayo madude yake,

je? yana madhara yoyote kiafya wataalam wa mambo

Pole sana Mkuu

Fanya utaratibu uhame hapo.
 
Back
Top Bottom