Ushauri wangu kwa kujifunza lugha ya kigeni ni mazoezi ya kusoma na kusema (ningelikwambia kuzungumza lakini kwa kwetu ni shida kupata watu wa kuzungumza nao.
Kwa uzoefu kusoma vitabu itakusaidia sana kujua sarufi na kupasi mitihani, lakini ili uweze kuzungumza fanya yafuatayo:
1. Soma vitabu, magazeti au maandishi yoyote katika lugha ya kifaransa. Si lazima uelewe kila unachokisoma. Lengo ni kuuzowesha ulimi wako kutamka kwa haraka na kwa ufasaha.
2. Wakati wa kusoma, soma kwa sauti badala ya kusoma kimya kimya. Kusoma kwa sauti kutakurahisishia hilo hapo juu.
3. Sikiliza radio za kifaransa na iga wanavyozungumza ili kupata "tune yao".
4. Nunu kinasa sauti (kwa sasa unaweza kutumia hata simu yako) ili wakati unapokuwa unasoma kwa sauti "ujirekodi" unachosoma, baadaye jisikilize. Mwanzo mwanzo naamini hutojipenda, lakini kadiri unavyofanya mazoezi ndivyo utavyoona unapiga hatua.
Kila la heri.