Mwenye Mawasiliano ya Rais Kikwete amjulishe hili

MpigfilimbiwaHamelin

JF-Expert Member
Aug 5, 2014
652
167
Wadau,

Nimesikia leo katika vyombo vya habari kuwa Rais Jakaya Kikwete atawapa vyeti vya uraia wakimbizi wa zamani wa burundi. Mimi ni mdau kwa vile nimekulia mkoani katavi. Kuwapa uraia ni sawa hasa kujali muda waliokaa ktk makambi hayo, lakini nasikia atatangaza pia kuwa watu hao waendelee kukaa katika kambi hizo wakiwa raia kamili. Hapa ndio pagumu, hawa watu wameishi zaidi ya miongo 4 lakini hawakujichanganya na watanzania. waliendelea kuoana wao kwa wao tu na hata kuenda kuoa burundi. Hivo suala la kuwaacha kuishi peke yao bila kuwahamisha waishi na watanzania ni kutengeneza burundi ndogo humu nchi.

Kumekuwa na uingizaji sil;aha sana katika kambi hizi. Is a serious matter, nadhani jk hajashauriwa vizuri. Najua jf ina wadau wengi, naomba anayeweza kuwasiliana na jk au washauri wake amweleze haraka - kabla ya mchana huu wa leo - kuwa angalau aahirishe kutamka makazi ya raia hao wapya yatakuwaje.

Uraia sawa ila angalau kupatikane njia nzuri kuwachanganyisha na watanzania wengine. La sivyo vizazi vijavyo vitapata shida kwa kuwa na vinchi ndani ya Tanzania hasa ukizingatia kambi hizi zipo maporini na zina eneo kubwa, wataitwa watu toka burundi na kuweka makambi ya uasi either wa burundi au Watanzania katika mapori hayo. Wapo viongozi walioshuhudia dalili hizi za uasi kasim majaliwa akiwa dc wa urambo alipambana sana na hili. Makosa yasirudiwe.

Hima jamani JK ajulishwe now.

 
hawa watu wameishi zaidi ya miongo 4 lakini hawakujichanganya na watanzania. waliendelea kuoana wao kwa wao tu na hata kuenda kuoa Burundi. Hivo suala la kuwaacha kuishi peke yao bila kuwahamisha waishi na watanzania ni kutengeneza Burundi ndogo humu nchi.

Ukiwa mkimbizi unatakiwa ukae kambini na usijichanganye na wazawa ndio maana hata wakitoka makambini huwa kwa ruksa maalum wakitoka kienyeji hukamatwa na uhamiaji.Kama hawa warundi walikaa kwenye makambi na hawakuchanganyika na wazawa kwa miongo yote minne basi wanaonyesha kuwa ni watii sana wa sheria za ukimbizi na kuwa wasingependa serikali ya tanzania ipate shida kuwatambua kama warundi kama ambavyo wahamiaji toka nchi nyingine hufanya ili kupoteza urahisi wa kuwajua.

Hao warundi naona hamna tatizo la kuwapa uraia wapewe tu.Na wakishapewa watakuwa sasa huru kwenda kokote,kuoa na kuolewa kokote na kuishi popote na hapo ndipo utawaona wakijichanganya ki-rasmi na watanzania.
 
Ni kweli kabisa . Endapo JK katangaza jambo kama hilo ,basi shauri wako una mashiko. Kuwaacha watu wa nchi nyingine sehemu moja ,kuwaacha waaishi kwa itikadi zao na tamaduni zao,hakika ni kutengeneza nchi nyingine ndani ya nchi nyingine.
 
Ni kweli kabisa . Endapo JK katangaza jambo kama hilo ,basi shauri wako una mashiko. Kuwaacha watu wa nchi nyingine sehemu moja ,kuwaacha waaishi kwa itikadi zao na tamaduni zao,hakika ni kutengeneza nchi nyingine ndani ya nchi nyingine.

Kuna wahindi na waarabu tanzania wameachwa kuishi na tamaduni zao na itikadi zao.Pia kuna makabila kibao yameachwa na itikadi zao na tamaduni zao lakini hazileti shida kwenye nchi.Cha muhimu si kutaka wao waue itikadi na tamaduni zao bali waishi nazo waishi kwa kutii sheria za Tanzania.Hizo itikadi na tamaduni hata kila mtanzania anazo! Si kigezo cha kuwazuia eti waziache ndio wapewe uraia!
 
Atakujibu nimemuona amesoma kabla hajakujibu cm yake imeisha chaji ndo mama salma kamletea chaji ameweka kwenye umeme kwahiyo subiri
 
Kuna aina za uraia 1. By birth, 2. Registration 3. Naturalization. Hivyo atakuwa amezingatia aina hizo. Hapa ni suala la nchi ili wapate raia wengi. Mbele kuna swali je watakuwa makini na laws za nch.
 
Ushauri wako murua sana. Nadhani Mkuu MwanaDiwani utasaidia kuufikisha kwa walengwa.
 
Tatizo la jk mkuu sio msikivu ndio maana hata katiba imependekezwa kubabe we mwache tu siku zinasonga atakuja kuwajibika tu hata kama atakuwa amekufa atawajibishwa na mungu
 
Watu wake wanapita sana humu jf Nina uhakika atapata taarifa. Ila 'kumbuka kauli yake Akili ya kuambiwa changanya Na ya kwako'
 
Kuna wahindi na waarabu tanzania wameachwa kuishi na tamaduni zao na itikadi zao.Pia kuna makabila kibao yameachwa na itikadi zao na tamaduni zao lakini hazileti shida kwenye nchi.Cha muhimu si kutaka wao waue itikadi na tamaduni zao bali waishi nazo waishi kwa kutii sheria za Tanzania.Hizo itikadi na tamaduni hata kila mtanzania anazo! Si kigezo cha kuwazuia eti waziache ndio wapewe uraia!
Naona mkuu East African Eagle hujaelewa vizuri post, mtoa post alichomaanisha ni kwamba hawa wakimbizi wakishapewa uraia wasiachwe wakaishi katika eneo moja wapewe uhuru wa kwenda mahali popote watakapo ili kujichanganya na watu wa jamii nyingine, kwa sababu hawa watu wakiendelea kukaa watu wa jamii moja manake unatengeneza ukabila katika eneo hilo....MH. JK hao wakimbizi wakipewa uraia waruhusiwa kwenda mahal popote watakapo ndan ya nchi hii, kuwaacha wakikaa sehemu moja ni kuitengeneza BURUNDI nyingine kwenye nchi yetu.
 
Back
Top Bottom