Mwenye Macho Haambiwi Tazama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenye Macho Haambiwi Tazama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by X-PASTER, Oct 11, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mwenye Macho Haambiwi Tazama

  Makala hii inakusudia kutazama japo kwa ufupi tu jinsi miaka arobaini na Tisa (49) ya kujitawala kwetu ilivyokwamisha au kurudisha nyumba maendeeo ya taifa letu.

  Kama navyo julikana Watanganyika walisimama kumtimua mkoloni ili waweze kupata huduma bora zaidi. Vile vile tunaona kuwa wenye macho wameanza kuwa na wasiwasi endapo kweli tuko huru, tumeendelea, tumeondoa ujinga, maradhi na umaskini na endapo kweli tumejikomboa.

  Je wasiwasi huu wa wenye macho unatoka wapi? Katika miaka ya mwanzo ya uhuru ilionekana kama vile tunasonga mbele katika harakati za kubadili hali zetu za maisha kutoka hali duni kuingia hali bora zaidi. Baadhi ya mambo waliyotuachia Wakoloni yaliweza kuendelea kutumika kuwapatia huduma wananchi.

  Mabenki yaliyoachwa licha ya kubadilishwa majina na kutaifishwa yalipanuliwa pia. Hatua hii iliongeza ajira kwa wananchi. Benki mpya kama Benki ya Nyumba (THB), Benki ya Rasilimali, Benki ya Maendeleo Vijijini (CRDB) n.k. zilianzishwa. Ulipofika wakati wa Azimio la Arusha majumba ya watu binafsi yalitaifsihwa. Hatua hii ilienda sambamba na ujenzi wa nyumba zilizofahamika kama nyumba za taifa chini ya Shirika la "National Housing Cooperation (NHC). Hatua hii ilisaidia kuwapatia wananchi makazi bora pamoja na ofisi.

  Shule za watu binafsi nazo zilitaifishwa katika kile kilichodaiwa kuwa ni kuwapa fursa watoto wote nafasi za elimu nchini. Sambamba na hili ada za elimu zilifutwa ili watoto wa watu maskini waweze kufuta ujinga bila bughadha.

  Mpango wa elimu kwa wote (UPE) ulianzishwa kwa shabaha ya kuhakikisha kuwa watoto wote wenye uwezo wa kwenda shule wanafanya hivyo. Hatua zilichukuliwa kujenga shule nyingi za msingi na ilipogunduliwa kuwa waalimu ni haba vyuo vya kata zilianzishwa na waalimu waliokuja kufahamika kama waalimu wa UPE waliandaliwa na kuingia kazini.

  Ndani ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hatua zilichukuliwa kuwadhibiti viongozi ili wasijilimbikizie mali.

  Katika kuhakikisha kuwa nchi inaongozwa na wananchi wenyewe, wataalam wengi wa Kizungu waliondoshwa na badala yake kuajiriwa wazalendo. Jambo hili liliongeza ajira pia. Mameneja wa mashamba makubwa yaliyotaifishwa wakawa Waswahili wenzetu. Yalikuwepo mashamba makubwa ya miwa, katani, kahawa, pamba, chai n.k. Mamlaka nyingi zikaundwa; mfano Mamlaka ya Chai, Mamlaka ya Kahawa n.k.

  Ifahamike kuwa licha ya ajira, mashamba haya yalikuwa yanatoa mazao yaliyouzwa nje na kulipatia taifa fedha za kigeni.

  Kulikuwa pia na viwanda mbalimbali kuanzia vya nguo, sukari, mafuta n.k. Viwanda vya nguo kama Sunguratex, Mwatex, Kilitex vilikuwa mashuhuri kwa ukubwa wake.
  Ni katika siku hizo hizo za mwanzo ambapo reli ya uhuru ilijengwa ili kuimarisha mawasiliano. Kampuni kubwa ya mabasi iliyojulikana kama Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA) iliweza kutoa huduma takribani nchi nzima. Hapa Dar kaapuni ya mabasi ya Usafiri Dares Salaam yaani UDA nayo ilitamba.

  Ni kweli kuwa yapo mengi zaidi ya niliyoyataja ambayo yalifanyika kwa jina la kuwaletea wananchi maendeleo. Wengi wakadhani kwamba kwa kuwa nyota njema huonekana asubuhi basi muda si mrefu wangelishuhudia faida na matunda ya kutimuliwa kwa mkoloni.

  Hali ilivyo leo wakati ninapoiandika makala hii wananchi wanaiona ile kauli ya mwanzo eti nyota njema huonekana asubuhi kama ndoto tu ambayo haina ukweli wowote.
  Kila kilichosemwa hapo juu ama kimekufa au kipo taabani.

  Mshamba yaliyotoa mazao na ajira leo yamegeuka mapori, viongozi waliotakiwa kuwa mfano wa mwananchi wa kawaida leo utajiri wao hauelezeki, makampuni makubwa kama KAMATA,UDA n.k, yamefilisika. Viwanda kama Sungura tex, Mwatex na Kilitex na vimesalia tu katika historia.

  Shule za sekondari za serikali zilizodaiwa ni kwa ajili ya wote leo zina watoto wa wenye fedha tu!

  Wenye macho wameshuhudia kupanda na kuanguka kwa KAMATA, UDA, THB, T.I.B, Tanganyika Packers, Sunguratex, Kilimanjaro Machine tools, Urafiki, Mang'ula n.k.

  Wameshuhudia pia jinsi uongozi wa makampuni, viwanda na mamlaka husika walivyoweza kufanikiwa kutoa maelezo ya 'hali halisi' na hivyo kutokuwajibishwa.

  Baadhi yao wanaishi katika majumba ya kifahari huko Mbezi, Masaki, Oysterbay na kwingineko jijini. Watoto wao wanasoma ng'ambo au katika shule zilizojengwa hivi karibuni jijini zenye hadhi ya 'kimataifa ambazo wanafunzi hupelekwa na kurudishwa nyumbani kwa magari.'

  Wenye macho pia yanashuhudia jinsi watoto wao wanavyoshindwa hata kuingia shule za msingi. Wanashuhudia jinsi nyumba zao zilivyo mbovu. Wanavyokosa ajira, mafao yao yanavyochelewa huku waheshimiwa wakilipwa haraka haraka ili wawahi kampeni n.k.

  Hali hii ya maendeleo basi ndiyo inayopelekea wananchi kwa maelfu hujaribu kuleta mabadiliko kwa kuwaunga mkono mitume wa siasa ambao wanaonekana kuongea lugha inayoeleweka kwao.

  Ni wazi kuwa hoja zilizomo katika makala hii ni baadhi ya vigezo ambavyo vitawafanya wapenda Tanzania kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili hatimaye ifikapo 31 Oktoba wapige kura itakayozaa Tanzania mpya.
   
 2. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Trc, atc & tpdc
   
 3. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Makala yako nzuri hongera, YES We need changes time is now, VOTE FOR Dr SLAA 31st Oct 2010

   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Unatafuta ugomvi. Mimi simo......
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kisa...!?
   
Loading...