residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 9,534
- 13,464
Mkuu MKANDAHARI , mawakili wasomi hawajitaji,wananchi ndio wanawataja.Humu ndani kumezuka tabia ya baadhi ya watu kujiita "wakili msomi" na wengi wao wameenda mbali zaidi na kuunga mkono hukumu za kesi kadhaa enzi za 5G ila cha ajabu rufani za kesi hizo zinaposikilizwa huangukia pua kwa aibu kubwa. Je, yawezekana kuwa hawa walifaulu kwa kutumia vibuti a.k.a "Juche"???
Nilikuwa napitia huu uzi wa Petro E. Mselewa anae jiita wakili msomi nikapigwa na butwaa kidogo baada ya kuona kina Mbowe wameonekana hawana hatia na warudishiwe fedha zao ila huyu wakili alimuunga bwana simba mkono kabisa
Anaejua CV yake sio mbaya akashea na sisi
![]()
Honestly, Hakimu Mkuu Simba amekuwa 'fair' sana kwa Mhe. Mbowe na wenzake
Mwanzo mwanzoni, natoa pole kwa viongozi wote wa CHADEMA na mwanachama mmoja wa CCM ambao jana wamehukumiwa kwenda jela au kulipa faini baada ya kukutwa na hata kwenye mashtaka ya jinsi yaliyokuwa yakiwakabili Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu. Mashtaka yao yalikuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu...www.jamiiforums.com
Mawakili wasomi ni M. Lamwai, P. Kibatala, M. Marando, T. A. M. Lissu, F. Karume, Prof Safari.
Unawezaje kuwa wakili msomi halafu ukawa upande wa "wanyongaji" !!??
Wakili msomi atasimama upande wa "wanyonge" wakati wote.
