Mwenye kujua CV ya Petro E. Mselewa

Mwenye kujua CV ya Petro E. Mselewa

Mkuu usishangae, hata shangazi (wakili mahili) alenda kuargue mahakamani kwa kutumia sheria iliyokuwa imeshafutwa tayari!
Wanasheria nao ni binadamu kama watu wengine.
"Mtu mzima unapovuliwa nguo chutama", sasa huyu jamaa tutamjuaje ni mtu mzima kama akivuliwa nguo anakimbia huku na kule akijiita nguli wakati tunamuona yupo uchi?
 
Ama tunamuhukumu sana maanahata wakili mahiri pia hupoteza kesi na kwa kupoteza kwake kesi hakumuondolei umahiri wake bali humpa fursa ya kujipanga vyema ili kama kuna namna basi anakata rufaa kupinga hukumu ama kukubali matokeo hivyo sioni kama ni sahihi kwa muktadha wa kisiasa tu kuona kuwa si lolote kwenye nyanja ya sheria
Una CV yake bro?
 
Humu ndani kumezuka tabia ya baadhi ya watu kujiita "wakili msomi" na wengi wao wameenda mbali zaidi na kuunga mkono hukumu za kesi kadhaa enzi za 5G ila cha ajabu rufani za kesi hizo zinaposikilizwa huangukia pua kwa aibu kubwa. Je, yawezekana kuwa hawa walifaulu kwa kutumia vibuti a.k.a "Juche"???

Nilikuwa napitia huu uzi wa Petro E. Mselewa anae jiita wakili msomi nikapigwa na butwaa kidogo baada ya kuona kina Mbowe wameonekana hawana hatia na warudishiwe fedha zao ila huyu wakili alimuunga bwana simba mkono kabisa

Anaejua CV yake sio mbaya akashea na sisi

Pia, soma:

- Honestly, Hakimu Mkuu Simba amekuwa 'fair' sana kwa Mhe. Mbowe na wenzake

- Asante sana Mkuu MKANDAHARI, hii ni CV yangu kwa kifupi
Mimi huwa ninaandika au kufanya uchambuzi wa maswala ya kisheria hapa Jamii forums pamoja kuwa ni wakili lakini sipendi kujiita au kujitambulisha kama wakili au wakili msomi kwa kawaida huwa ninajitambulisha kwa jina langu na kujitambulisha kama Senior JF Member na mara chache sana ujitambulisha kama law fitnaologist (legal fitnaologist) ambalo ni jina la utani ambalo wananiita mawakili wenzangu.

Mimi ni muumini wa uzito wa hoja za kitaaluma na kitaalamu na sio muumini wa hadhi au cheo cha kitaaluma cha mtoa hoja.
 
Nimekusoma vilivyo, ila nilichojifunza hapa ni kuwa kwenye 5G watu wengi walijichomoa akili, na sio kwamba ni kwa matakwa yao, bali ni kwa sababu ya hali zao kwa the time being! Imagine ilifika time mpaka akafananishwa na Yesu, wapumbavu wakasadiki..
Nini maana ya "5 G"?
 
Tatizo la watu wengi wakiwa udsm hata vihande wanajiona wapo sawa kichwani...
 
Mjadala mpana wa Law reports of Tanzania na uchambuzi wa hukumu zilizomo ktk Law reports za Tanzania

"KITABU CHA SUPREMACY OF LAW CHA JUDGE SAMATTA, NI HAZINA KUBWA." Prof. CHRIS. M.PETER


Prof. Chris Maina Peter, Mhariri wa kitabu cha Supremacy of Law akikichambua kitabu cha Supremacy of Law, cha Judge Mkuu Mstaafu, Barnabas Albert Samatta, akikielezea nini kilichopo ndani ya kitabu hicho. Judge Samatta aliwahi kuwa DPP pia amefanya kazi Zimbabwe kama jaji na baadhi ya hukumu zake kufanywa rejea katika Mahakama za Afrika ya Kusini. Hukumu ya Jaji Samatta ya kesi ya Yesu si Mungu iliyoendeshwa kule Morogoro na kuzua hisia na mjadala mpana

Source : NGOWI TV

Jaji Warioba: Wanasema Umeshinda Kesi Ngapi na Siyo Umetenda Haki Ngapi Mahakamani


Amesema hayo Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta uliofanyika Wakili House jijini Dar Es Salaam
Source : Wakili tv

Rule of law vs. rulers of law. justice Barnabas Albert Samattas road to justice​

This book reproduces some of the leading judgements written by Justice Samatta. It highlights, in a critical fashion, some of his beliefs and observations as embedded in his decisions and speeches. This is to celebrate him as an example of an ethical lawyer whose integrity cannot be questioned, making him a worthy model for the younger generation to emulate and draw inspiration from. Justice Samatta's decisions touched on key areas of: Rule of Law and the Consitution, where he emphasised that the constitution crystallises a consensus among citizens as to the nature and character of their polity and governance; Access to Justice, about which he believed that the doors to justice should be opened to all regardless of their station in life or economic position; Ethics, Integrity and Professionalism where he frequently quoted Nyerere 'There are some jobs in our society that can be done by unethical people...Being a judge or a magistrate is not one of these jobs...'; and Environmental Law where he argued 'The vulnerability of our planet has reached such a depressing degree that there is no greater service judges can render to mankind than playing their role in the protection of the environment...' He summarised his life-long conviction by saying: 'Let everyone in our society give justice a chance to prevail'.
Source : https://www.researchgate.net/public...tice_Barnabas_Albert_Samattas_road_to_justice
 
Hawa ndo kina Kabudi in the making...maprofesa uchwara kama Tundu Lissu anavyowaitaga. Wazee wa kuilamba CCM makalio kusubiri teuzi
 
Nimekusoma vilivyo, ila nilichojifunza hapa ni kuwa kwenye 5G watu wengi walijichomoa akili, na sio kwamba ni kwa matakwa yao, bali ni kwa sababu ya hali zao kwa the time being! Imagine ilifika time mpaka akafananishwa na Yesu, wapumbavu wakasadiki..
We unasema yesu, Prof Kabudi alimwita Magu Mheshimiwa Mungu!!! Sikuamini masikio yangu,niliirudia hiyo video mara kumi kumi!!
 
Back
Top Bottom