Mwenye jibu nampa zawadi

sky walker

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
1,160
824
MWENYE JIBU NAMPA ZAWADI YA VOCHA 1000 TIGO

Nilenda bar siku ya fainali ya kombe la dunia kuangalia mechi ya CROATIA NA UFARANSA,baada ya kukaa kwenye kiti akaja dada muhudumu na akasema kiingilio ni soda na soda wanauza 600 ,kwa bahati mbaya mfukoni nilikuwa na 500 kwahyo nikamuomba nimpe mia tano halafu asinipe soda ,akakubali nikampa na akaondoka.

Baada ya nusu saa akaja mkaka akajitamburisha yeye kuwa ni meneja wa bar na akauliza mbona huna kinywaji nikamuelezea ilivyokuwa ,akasema hawa wajanja sana na akanipa 100 akasema muite mpe hii 100 akuletee soda yako.

JE MENEJA ALIPATAJE FAIDA KWA HILI?

ANGALIZO:mie sina jibu ila nitaangalia tu mwenye jibu lenye ushawishi tu nitamtumia hyo vocha hapo chini kama zawadi.
 
Alipata faida kwa kuwa bei ya ile soda ni sh 500(faida ipo tayari) wameweka 600 kwa sababu ya mpira ili wapate faida zaidi kwa kuwa watu ni wengi. Hivyo alivyokupa ile 100 wewe ukatoa 500 ataenda kuchukua 100 yake na bado kutakuwa na faida kwenye 500 yako(bei ya kawaida).
 
Alipata faida kwa kuwa bei ya ile soda ni sh 500(faida ipo tayari) wameweka 600 kwa sababu ya mpira ili wapate faida zaidi. hivyo alivyokupa ile 100 wewe ukatoa 500 ataenda kuchukua 100 yake na bado kutakufa na faida kwenye 500 yako(bei ya kawaida).
Mkuu hili ndio jibu sahihi,
 
Meneja ana roho mbaya na yupo tayari kuingia hasara ili mtu mwingine asipate hela. Kwakifupi wote walipoteza ila meneja aliingia hasara ya hiyo 100 aliyotoa mfukoni kwake na yule dada alipoteza hiyo 500 na kama alikuwa ameshatumia kwa kujua ameipata bure hapo ndo inakula kwake
 
Hivi mtoa mada huoni kabisa kuwa ulitoa RUSHWA kwa kumpa yule mdada tshs 500/=?
 
unaaendaje kuangalia mpira Bar ukiwa na Jero mfukoni ? Kama mimi ni uyo dada ningekukana kabisa hujanipa hata hiyo jero
 
Kinachoniuma ni kwamba mpaka namaliza kusoma jibu langu lilikua ni 'Wilaya ya Kinondoni' nashangaa hapa nakuta namba tu zinatajwa
 
Meneja ameresort kwenye marketing strategy, faida yake hapo ni ya long term zaidi kuliko ya siku hiyo moja.

Uwezekano wa mteja kurudi tena hapo tena akiwa na wenzake ni mkubwa kuliko angemtaka kuondoka.
 
Faida aliyopata Meneja ni wateja wote kuwa sare sare kwa kila mmoja kuwa na soda mkononi.

Akili yangu inaniambia mliimbishwa wimbo wa

Sare sare maua
Asiyejua kuchagua
Kabila lake mzigua
 
Kinachoniuma ni kwamba mpaka namaliza kusoma jibu langu lilikua ni 'Wilaya ya Kinondoni' nashangaa hapa nakuta namba tu zinatajwa
Hahaa Katibu hii wiki nzima inawezekana ulipata kitu roho inapenda kwenye kamati pendwa!.
Majibu yako yanakua classic sana
 
Acha ungese wewe unataka kupoteza watu humu, mmeshindwa kukamata watu humu JF sasa mnatumia njia za kifala mtupate, mpate namba za simu kisha mtupoteze Pumbavu zenu na Huyo Mbuzi anayewatuma.
KIVIPI MKUU, au bado una wenge kuna mtu kaombwa namba hapo juu au kuna sentensti ina sema weka namba.
 
JE MENEJA ALIPATAJE FAIDA KWA HILI?
kwa siku husika meneja hakupata faida,

Faida atakayoipata ni baada ya wewe kuwa mteja wa kudumu, Kwa jinsi alivyo onyesha kukujali,( kujali mteja wake) , Sidhani kama siku nyingine utaenda kwenye baa nyingine tofauti na hiyo kwa huduma ya kuangalia mpira. La hasha

MyTake
  • Wapo wafanya biashara walio tayari kupata hasara kwa siku au wiki moja, ila akajenga mazingira ya yeye kuendelea kupata faida miaka na miaka.

  • Nitumie vocha yangu ya buku faster
 
Faida ni kujua wote mlioingia siku hiyo kuangalia game mmelipa kiingilio kwake ni kuhesabu vilivyopo .
 
Back
Top Bottom