Laki 7 mbona kubwa sana mzee baba,Fanya biashara ya kuuza juice za matunda ile ya kutengeneza mwenyewe kwenye blender,tena mtaji wake ni mdogo nunua blender yako elfu 70,vikopo vya kuwekea juice au waweza nunua glass,mirija,kama ukihitaji friji yako mwenyewe nunua ya bei chee laki 3 au waweza muomba mtu awe anakuhifadhia kwenye friji lake kwa kuchangia gharama za umeme.Namna ya kuuza ni kutembeza kwenye mikusanyiko ya watu wengi isikae sehemu moja.Hii biashara haina cha kodi wala tra ukiwa na jitihada ya kuuza una uhakika wa kulaza faida ya 15000-20000.KAZI KWAKO