UNI CASH FLOW: Ondokana na Mentality ya Ugumu wa Maisha(~Kwa Wafanyabiashara, Wajasiriamali na Watanzania Wenzangu)

Fact19

New Member
Jan 2, 2019
4
2
Habari wakuu!

Hivi karibuni, nikiongelea miaka kadhaa nyuma, kuna hali mpya ambayo imetutembelea, hali ambayo inajaribu kuishi na sisi, ikitufunga akili, kutunyima furaha na kadri siku zinavyozidi kusonga, hali hii inazidi kuwa na mashiko kaika jamii zetu. Kwa maneno macache ambayo, kama wimbo, yanatumika kuielezea hali hii uko mitaani kwetu….”Vyuma Vimekaza!”; ali hii inaweza kutafsiriwa kuwa kuna ugumu wa maisha ambao kadri siku zinavyozidi kusonga..unapata mashiko.

Labda hiyo haya nzima nliyo andika hapo juu haina maana, ila lengo la mimi kuanzisha nyuzi hii ni kusambaza ujumbe chanya ambao ukiamua kuuchambua na kuchukua yale ya msingi, naamini kuwa hautoimba wimbo ule ule kwa mwaka huu pia.

Kila kitu kinachotokea katika maisha yetu kina sabau, na maisha kuwa magumu(Kama wengi huko wasemavyo) kuna sababu zake pia. Baadhi wamejaribu kuihusisha serikali ya awamu ya tano na ni mada ambayo ina mashiko japo, kwa mtazamo wangu sio sahihi!
Miaka kadhaa nyuma, hali ilikuwa ile ile na iliyopo sasa, kuna kitu kidogo kimeenguliwa na hicho ndicho kinachofanya huu wimbo uwe na nguvu mtaani. Sehemu iliyotenguliwa ni kwenye MZUNGUKO WA FEDHA na ukifahamu kurudi kwenye mzunguko wa awali ambao kwa mabadilko kadhaa ya kimaendelo yanayofanywa na serkaliumeweza toka, basi mwaka huu utakuwa wa amani na furaha.
Binafsi naamini hali ni ile ile, ila kupitia Economic Illusion, uliwezwa kuaminishwa kuwa kuna unafuu kwa kuwa uliweza kupata pesa kiurahisi(walau kidogo kuliko ilivo saa hivi) na kama wengi wanavyolalamika ni kuwa ilikuwa inashikika. Kwa sasa mambo ni tofauti maana kuipata kwa mtu wa kawaida ambae hana ajira ni gnumu. Na hata kwa wale wenye ajira, ni yale yale maana haishikiki.
Sababu iliyosababisha unafuu wa hapo mwanzo, kama nilivyosema ni MZUNGUKO WA FEDHA. Hata sasa bado inazunguka, ila sio kama ilivyokuwa kipindi kile. Toka tupate uhuru, mzunguko wa pesa ulikuwa wa kasi…nikimaanisha kuwa pesa uliyokuwa ukitumia kununua baiskeli ukiwa mwanza….ilikuwa inawezwa kumfikia mtu aliye Dar ndani ya siku hiyo hiyo au kesho yake(Na kwa mkono..yaani Cash)

Ila siku zinasogea na kadri siku zinavyozidi kusogea…huu mzunguko unapungua kasi, na kwa sababu ya mazoea unaathiri wengi. Hali iliyopo kwa sasa, kutokana na maelezo ya hapo juu ni Mzunguko wa fedha kudorora. Kwa asilimia hamsini na tano(55%) pesa inayozunguka Tanzania imewekezwa kwenye mabenki, MobileMoney na Hisa. Na hata ile 45% liyobaki wengi wetu tunaimpact nayo kwa 1-6% tu! Kwa kuwa inaenda pole pole.
Labda kwa mfano huu hapa hoja yangu itaeleweka zaidi;
Miaka kumki na nae nyuma…biashara zilikuwa zinakuwa kwa kasi, na pia hazikuwa na upinzani kama ilivyo sasa. Kwa kusema hivyo namaanisha kuwa, sehemu nyingi zilikwa zina huduma chache ambazo hazikuweza kukidhi mahitaji ya wengi.

Mfano mimi, nimekulia sehemu ambako ulikuwa na maduka mawili tu! Ambayo alikuwa yanahudumia karibia watu 400 hivi kwa wiki.(I am Serious) Kutokana na hali hiyo, wamiliki wa maduka hayo walikuwa wana agiza vitu karibia kila baada ya wiki nne.

Teknolojia ilikuwa ya chini, hivyo kulikuwa kuna kmalipo ya cash ambayo ndiyo alikuwa maarufu. Hivyo hela ambayo nilitumia kununua kilo a unga pale dukani kwake, Kwa asilimia arobaini(40%) kulikuwepo uhakika wa hiyo hela kurudishiwa kwa mteja mwingine kama chenji na uhakika wa asilimia therathini(30%) kuwa hiyo pesa ingesafirishwa kupita mikoa kama mine hivi kufika Dar(ambako mwenye duka alikuwa akinunua bidhaa kwa bei ya jumla) ikiwa katika Cash. Asilimia 30% nyingine ni uhakika kuwa ile pesa angu ingeenda kuhifadhiwa benki, kuhifadhiwa nyumbani na kutumika kulipa watu wengine waliokuwa wakimfanyia kazi huyo baba.
Hao ilikuwa mtaani ninako ishi, na hali hii najua ilikuwa ikiendelea sehemu nyigni hapa Tanzania. Hiyo inatosha kuonesha kuwa pesa ilikuwa ina samba kwa kasi. Hivyo ilikuwa inashikika, yaani ungebaki na elfu kumi ndani kwa siku kadhaa isinge haribu zmunguko wa mtaani kwako kama ilivyo leo!

Tukizifaamu sababu zilizopelekea mzunguko wa nyuma kuenda kwa kasi na wa sasa kuenda kama tunavyo uona, basi itakuwa ahisi katika kufanya maamuzi sahihi ambayo yatasaidia kuondoa hiyo hali, kilio husika!

Sababu Zinazoelekea Mzunguko wa sasa kudorora.

• Teknolojia
Hapa nadhani inajielezea kiurahisi, kadri siku zinavyoenda…kazi nyingi ambazo zilikuwa zinafanya na watu zinafanywa na kompyuta. Pia takwmu zang zinaonesha kuwa esa inayozunguka ni ndogo kuliko iliyo hifadhiwa hii ina maanisha kuwa kuna faida ambayo watu wanadhani wanapata kwa kuhifadhi hela zao kuliko kuziweka kwenye sytem…haswa wale wenye nazo!

Sio hivyo tu, tumeshuhudia matapeli wakiongezeka kila siku na wana akaili nyingi…na kwa bahati mbaya, huwa wanafahamu kile ambacho hatujui hivyo kutushawishi tujifunze kupitia kwao.

• Ushidani
Ushindani wa kibiashara, unazidi kupamba moto kila kukicha. Ninaongea hivi maana kama mjasiriamali, ninaona mambo mengi nay a ajabu ya kitendeka. Watu siku hizi awafikri bali wanarudia kile kinachofanywa na wengine hivyo kuleta hasara ya jumla.

Ukienda Youtube na kutazama n channel ngapi za kitanzania zinatoa habari ile ile…taarifa zile zile, ikiweekana kama kuna footage au picha zinakuwa zile zile…maana wanajali wapae AD Views na Impressions…henc pesa. Hawajali maslahi ya kile wanachokifanya. Hii inapelekea traffic kuwa haina quality, kusambaza taarifa za ongo, clickbait na mabo mengine ya ajabu kama hayo.

Lwenye mfano wangu nimesema kulikuwa na maduka mawili ila kwa sasa, sehemu ile ile, kuna maduka kumi na tisa! Kuuza hapo itakuwa tabu. Na hata ikitokea mtu ameuza, zile fedha atahifadhi ili zijitoseleze kuleta mzigo mwigine. Kwa hali hiyo, anakwamisha mzunguko wa pesa mtaani, na kwenye taifa kiujumla.

• Ubinafsi
Hii inabeba uhalisia na kweli ndani ake..maana ni kitu tunachokishuhudia, na kimefanya tukifanya moa a misingi yetu ya kiamii. Nimekuwa mfuatiliaji wa mada nyingi za kiujasiiamali humu JF na nimeshuhudia kila mtu anaejaribu kuelezea fursa akiitwa tapeli.

Pia nimebahatika kuwafuata baadhi ya watu hawa wanao toa fursa humu humu na kitu nilichogundua ni kuwa wengi wao ni wabinasi…wanakufunulia kitu kwa macache ili waweze kukutumia kama fursa utakapoitaji kujifunza zaidi.

Hata mawazo yetu sasa ni akibinafsi! Kila wazo la kibiashara mtu atakalo kuwa nalo..linamuhusisha yeye peke ake. Au na watu kama wane tu na wazo huska aliko Scalable(Yaani biashara huska haiwezi kukuzwa). Nachojaribu kusema unakuta mtu ana 3.5M anataka kununua pikipiki/bajaji amuajiri tu mmoja tu wakati kwa mtaji le ule angeweza kuja na wazo linalomuwezesha kuajiri watu ishirini…(Nnayo mawazo mengi kama haya…hivyo siandiki kitu nisichokijua)

UNATOKAJE KWENYE MZUNGUKO HUU UNAO DORORA NA KURUDI KWENYE ULE UNAO ENDA FASTER?

Nimetoa sababu nne ambazo zinaweza kuwa zinapelekea huu mzunguko wa sasa kuwa hivi, na nina amini kuwa wewe unaesoma unahusika kama siokwenye mbili ya hizo..basi zote! Na ukiacha unakuwa unaboesha mzunguko wenyewe.
Hautoaca kuanya hivyo na kuona Tanzania yote ikisema kuwa “Vyuma vimewekewa Grease!” hamna…ila mabadiliko utaanza kuaona kwenye familia ako, mtaani na kadri unavyozidi kuwa na impact kubwa ndivyo kasi ya mzunguko nazidi kuongezeka.

Hivyo kama una wazo la biashara mbalo una amini lina faida kubwa na unakosa mtaji. Wafuate wenzio mjikuanye na muanzise biashara kwa pamoja…usisubiri zije!

Kama unao mtaji na huna wazo la biashara, usianze kufungua biashaa usizofahamu, tafuta marafiki msaidiane na kuleta kitu imara zaidi.
Haa kama na 5000…kama unajua utkavyoweza kutengeneza Milioni ukiwa na laki tano, usisubiri siku utakayopata hiyo laki tano, tafua wenye nazo(Na kama unajua kuzalisha pesa hivyo…nitafute tuyajenge!)

Kama wewe ni mtu usiye na ajira, basi usiwe na mawazo ya kujiajiri na huna mtaji huku miasha kwako ni magumu! Tafuta ajira…ukiwa ready ku move on,. Utakuwa umesaidia familia yako na kazi ako pia!
Kwa wale wenye maduka kama mimi(Zipo njia kadhaa za kuuza faster na kuukwepa usihindani. Tumia hizo kuliko kupakia duka lako na viu ambavyo vitakaa maani kwa miezi.

Kama unachoma mahindi stendi..na wapo watu ishirini kama wewe wanafanya hivyo hivyo….mansidana kuuzia watu wanaokuja na mabasi na mmoja wenu ndo tu anauza, jiongeze! Shawishi wenzio muunane muwe na biasharamoja, bidhaa zenu ziwe packaged na muuonoe huo ushidani,

Umoja una nguvu kuliko tunavyodhani…na kuliko jamii inavyotaka tuamini! Njia nyingine ya kuwahisha system, ni kwa kushae huu uzi na zle zenye tija katika maendeleo li usinufaike eke yako…bali nyote kwa pamoja!

Nawasilisha!

Fact19 | 001
 
Back
Top Bottom