Ndiyo maana akapelekwa mafunzo nchini Canada, kisha kujiunga na jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ / TPDF
Inaonesha miaka hiyo haikujalisha nasaba yako , bali kama ni mzalendo unaweza kuajiriwa vitengo nyeti na katika vyombo.
Babu yangu aliniambia kuwa kuvuja taarifa za kuwepo njama za mapinduzi, zilianzia kutoka kwa mtanzania tajiri mzalendo mgiriki (mzungu) ambaye alikuwa mmiliki wa hoteli ya Motel Agip jijini Dar es Salaam.
Huyu mgiriki alikuwepo katika listi ya watanzania wa asili mbalimbali waliokuwa wakitegemewa kupenyeza taarifa nyeti kwa vyombo vya usalama.
Tukumbuke hata mzee Dewji mnyiramba wa Singida alishiriki vita vya Kagera na kuendesha Lori hadi mpakani mwa Uganda na Sudan huko Arua akiwa mgambo aliyejitolea kushiriki katika vita hiyo ya Kagera
Jeshi kulikuwepo watu wa nasaba mbalimbali za wazalendo wa kiTanzania na hata kushiriki kutaka mbadiliko (uhaini ) au pia walishiriki kuzuia uhaini kama raia wengi waTanzania.
SOMA ZAIDI : mchango wa raia wa kigeni kabisa wasio raia :