Mwenye CV ya mgombea wa CHADEMA Chalinze Mathayo Torongey

Mwenye CV ya mgombea wa CHADEMA Chalinze Mathayo Torongey

Iliwahi kuombwa cv ya Mbowe humu lakini mpaka leo sijaiona. Isije kuwa na huyu mgombea nae haitopatikana.

Nawashangaa akina Mohamedi Mtoi kwanini hawataki kuweka cv ya huyu mgombea wao. Kuwa na cv si lazima awe na shahada za vyuo, inaweza kuwa hajasoma sana lakini kaelimika.

Weka ya kwako kwanza
 
Tumaini Makene ebu kata mzizi wa fitina weka CV ya mgombea wenu Chalinze.
 
Last edited by a moderator:
Iliwahi kuombwa cv ya Mbowe humu lakini mpaka leo sijaiona. Isije kuwa na huyu mgombea nae haitopatikana.

Nawashangaa akina Mohamedi Mtoi kwanini hawataki kuweka cv ya huyu mgombea wao. Kuwa na cv si lazima awe na shahada za vyuo, inaweza kuwa hajasoma sana lakini kaelimika.
Soma majibu ya pingamizi lake utajua Cv yake.......
 
MAJIBU YA HOJA YA PILI; Kwanza, nieleze wazi
kuwa nimesikitishwa sana na tuhuma hizi
ambazo zina lengo la kunichafua mbele ya jamii
na Taifa kwa ujumla, zina lengo la kuichafua
jamii ya watanzania kutoka familia za wakulima
na wafugaji, watu ambao wana kipato kidogo
na ambao wanaishi vijijini kuwa ni watu wa
hovyo na hawajui kusoma wala kuandika, ni
tuhuma za kuwadhalilisha watanzania ambao ni
kutoka jamii za wananchi wa vijijini
wanaotafuta fursa ya kuchaguliwa kwamba ni
watu wa wanaoomba nafasi wakiwa hawajui
kusoma wala kuandika, kwa kweli nasikitika
sana kwa hili na lilikuwa tusi ambalo
msimamizi wa uchaguzi hukupaswa kulipokea.
Aidha, nashindwa kutoa ushahidi hapa kwani
hata wewe umeziamini tuhuma hizi kuwa mimi
sijui kusoma wala kuandika na ndio maana
ukanitaka nizijibu, japo ni ukweli ulio wazi kuwa
sahihi yangu kwenye fomu haikuwa ya "kuweka
dole gumba" niliweka sahihi kwa kuandika na
mbele yako na sikuandikiwa. Pili; Yafaa
mgombea huyu pamoja na wale wote
waliomtuma wakatoa ushahidi wake kwako
kuwa mimi Mathayo Mang'unda Torongey sijui
kusoma wala kuandika, na hii itamsaidia
kuaminika mbele ya jamii ya wananchi wa
Chalinze ambao anataka kuwaongoza. Hata
hivyo naomba nitoe majibu mbele yako kwa
maandishi na kwa kusoma kitu ambacho wewe
utataka nisome na kuandika ili uwe uthibitisho
kwako kuwa najua kusoma na kuandika .

Sidhani kama 2tapata CV apa
 
Weka ya kwako kwanza

Fungulia nyuzi utawekewa tu au unaweza kutumia "search" ya JF au ya google, utanikuta tu. Hapa tunataka cv ya mgombea wa magwanda wa Chalinze.

Upo hapo ulipo?
 
Iliwahi kuombwa cv ya Mbowe humu lakini mpaka leo sijaiona. Isije kuwa na huyu mgombea nae haitopatikana.

Nawashangaa akina Mohamedi Mtoi kwanini hawataki kuweka cv ya huyu mgombea wao. Kuwa na cv si lazima awe na shahada za vyuo, inaweza kuwa hajasoma sana lakini kaelimika.

FaizaFoxy namchukia zaidi ya wanalumumba wote. Ritz ndio mwenye akili walau kidogo kati ya wanalumumba.
 
Last edited by a moderator:
Huu uwanja nawaachia mpigane wenyewe kwa wenyewe kamanda yupo kapumzisha mwili tayari kwa pambano na wezi wa nchi hii
 
Kamanda, mimi sipo huko kwenye sheria za uchaguzi ni kawaida yetu humu ukumbini kuangalia CV za wagombea majuzi tuliona CV ya dada yetu kule Kalenga tukaijadili ni CV nzuri kwa kweli, siyo vibaya tukiona CV ya huyu mgombea wa Chadema, Chalinze.

Mkuu nadhani uongozi ni talanta na siyo maambukizi ya ujuaji (tunaita elimu au CV) hizo CV tunazopigania kila siku hapa hazikushushwa toka mbinguni ni binadamu wenzetu kwa upeo wao waliona inafaa kitu hiki kuwa hivi na kikawa na kikakubalika kuwa ndio kibali au kipimo cha ujuaji! Vitabu vya MUNGU vimesema juu ya Elimu "Chunga sana elimu asije akaenda zake" lakini haimaanishi hizo CV's tu tunazopigania hapa maana yake kubwa ni mwanadamu usiwe mvivu wa kutafakari na kuamua kwa hekima. Tukijua nini maana halisi ya Elimu hakika hakuna atakaye mdharau mwenzie kwani kila mtu ana elimu kichwani, au kwa ufupi binadamu anapokuwa na utashi wa kutafuta majibu ya vikwazo juu ya maisha yake hiyo tayari ni elimu! huu upofu tuliobatizwa na watu wa magharibi umeupiga ganzi bongo zetu tuone kuwa hatuna taaluma au elimu! hayo ma CV ni kukopi na kupest maana ni mamiaka mamilioni watu hukariri maandishi hayo hayo tu kinachobadilika ni rangi ya vitabu na maandishi katika lugha tofauti! tuwe wepesi wa kujiamini na sio wepesi wakutokuamini kile bongo zetu ziwashapo taa ya majibu! cha muhimu hapa tuangalie hekima/Busara na kipawa cha uongozi na sio utawala unaokumbatiwa mara nyingi na kava la CV's
 
Mkuu Ritz ukiona polojo nyingi na CV haitoki ujue shule huyi hana au hajakamilika, angekuwa na elimu huyo wala isingechukua muda kuletwa hapa.
 
Last edited by a moderator:
MAJIBU YA HOJA YA PILI; Kwanza, nieleze wazi
kuwa nimesikitishwa sana na tuhuma hizi
ambazo zina lengo la kunichafua mbele ya jamii
na Taifa kwa ujumla, zina lengo la kuichafua
jamii ya watanzania kutoka familia za wakulima
na wafugaji, watu ambao wana kipato kidogo
na ambao wanaishi vijijini kuwa ni watu wa
hovyo na hawajui kusoma wala kuandika, ni
tuhuma za kuwadhalilisha watanzania ambao ni
kutoka jamii za wananchi wa vijijini
wanaotafuta fursa ya kuchaguliwa kwamba ni
watu wa wanaoomba nafasi wakiwa hawajui
kusoma wala kuandika, kwa kweli nasikitika
sana kwa hili na lilikuwa tusi ambalo
msimamizi wa uchaguzi hukupaswa kulipokea.
Aidha, nashindwa kutoa ushahidi hapa kwani
hata wewe umeziamini tuhuma hizi kuwa mimi
sijui kusoma wala kuandika na ndio maana
ukanitaka nizijibu, japo ni ukweli ulio wazi kuwa
sahihi yangu kwenye fomu haikuwa ya "kuweka
dole gumba" niliweka sahihi kwa kuandika na
mbele yako na sikuandikiwa. Pili; Yafaa
mgombea huyu pamoja na wale wote
waliomtuma wakatoa ushahidi wake kwako
kuwa mimi Mathayo Mang'unda Torongey sijui
kusoma wala kuandika, na hii itamsaidia
kuaminika mbele ya jamii ya wananchi wa
Chalinze ambao anataka kuwaongoza. Hata
hivyo naomba nitoe majibu mbele yako kwa
maandishi na kwa kusoma kitu ambacho wewe
utataka nisome na kuandika ili uwe uthibitisho
kwako kuwa najua kusoma na kuandika .

Sidhani kama 2tapata CV apa

Yaan kashindwa ata kusema ningepataje div 4 ya form 4 kama sijui kusoma na kuandika?bila shaka huyu kweli hakuhudhuria kabisa darasani.
 
Mkuu Ritz ukiona polojo nyingi na CV haitoki ujue shule huyi hana au hajakamilika, angekuwa na elimu huyo wala isingechukua muda kuletwa hapa.
Mkuu wangu Rich Pol

Hata mimi nashangaa makamanda badala ya kuleta CV wanakuja na maelezo marefu ambayo hawakuombwa.

Wiki iliopita wenyewe waliweka CV ya yule dada mgombea wa Kalenga, na walimsifia sana leo wamebadika wanasema CV siyo muhimu.

CC; chama Mingoi MSALANI lusungo
 
Last edited by a moderator:
Wanaukumbi.

Kuna utata wa elimu ya mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chadema Mathayo Torongey, kuna wengine wanasema kasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wengine wanasema kasoma Uingereza.

Mwenye CV yake tunaomba atuwekee kama walivyofanya kwa Grace Tendege, mgombea wa Chadema Jimbo la Kalenga.

Ni vizuri tukajua viwango vya elimu vya mgombea kama utaratibu wetu humu JF.

acha kielehele, kwn wewe ni mpga kura wa chalinze? na ukishajua elimu yake utafanya nini, ama upo TCU?
weka yako kwanza na utwambie unafanya kazi gani?
 
CV ya TENDAGA iko mafichoni kama ile ya LEMA, usitegemee chochote kipya!
 
Yaan kashindwa ata kusema ningepataje div 4 ya form 4 kama sijui kusoma na kuandika?bila shaka huyu kweli hakuhudhuria kabisa darasani.

Kweli mkuu kunastyle za kujitetea kama kweli umetafuna books walau hata kidato cha nne.
 
Back
Top Bottom