Mwenye Angels' Park aua gangstar kwa risasi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenye Angels' Park aua gangstar kwa risasi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Jul 14, 2010.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sadam ameauwa kwa kupigwa risasi mchana wa leo katika baa maarufu ya Angels' Park iliyoko Ilala Sharief Shamba jijini Dar es salaam!! Kijana huyo inadaiwa kuuawa na mmiliki wa bar hiyo baada ya kundi la vijana wengi, akiwemo marehemu, kuvamia kwa lengo la kumpiga mwenye baa ili kulipiza kisasi! Mtandao huu umeeleza na mashuhuda kuwa, sakata lilianzia jana baada ya vijana wasiojulikana kudaiwa kumkaba mteja mmoja wa baa hiyo akiwa toilet na vijana hao kukamatwa na kuplekwa polisi ambako walishikiliwa hadi leo. Imedaiwa kuwa baada ya kuona wenzao wanasota rumande, pengine kwa sababu ya mmiliki wa huyo, waliamua kumfuata ili kulipiza kisasi kwa kumfanyia.
  Wakiwa kundi huku wameshika silaha mbalimbali vikiwemo visu, vijana hao walivamia baa hiyo na kuanza kumpiga mwenye baa na kumchoma kisu ambacho bahati nzuri hakikumdhuru sana. Kuona hali hiyo, mwenye baa alitoa bastola yake, akapiga hewani ili kuwatisha, lakini waliendelea kumfuata na kumshambulia huku wakiharibu mali za baa hiyo, likiwemo gari lake lililovunjwa kioo cha nyuma. Awali vijana wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa na marehemu aliendelea kumfuata mwenye baa na ndipo alipopigwa risasi na kufa papo hapo!​


  My take: Ikifikia hali kama hii ni dhahiri kuwa sasa watu wamekata tamaa na maisha yao​
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jul 15, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Unfortunately, mimi sikubaliani na hadithi hii kabisa. Huyu jamaa mwenye baa alichofanya ni murder, ila kwa Tanzania yetu ya leo ambapo mwenye pesa ndiyo shujaa, kijana huyu atakufa kibudu bila kupata justice yoyote. Hata kama alikuwa na tabia mbaya, hakuna mtu mwenye haki ya kuondoa uhai wa mtu mwingine hapa duniani.


  1. Haiwezekani mchana ule eti lije kundi la vijana kadhaa wajaribu kumchoma kisu na kumkosa, halafu eti apate nafasi ya kurusha risasi hewani.
  2. Haiwezekani kuwa baada ya kurusha risasi hewani bado vijana wale waendelee kumfuata.
  3. Hata kama huyu Saddam aliendelea kumfuata kwa vile "hakuona hiyo bastola ya mwenye baa na wala hakusikia mlipuko wa risasi iliyorushwa hewani," kama kweli ilifanyika hivyo, kwa vile Saddam hakuwa na silaha ya kutisha, matumizi hayo ya deadly force hayakuwa justified: kilichotakiwa ni kum-subdue hasa kwa vile ilikuwa ni mchana kabisa.
  Tangu serikali iliporuhusu umilikaji holela wa silaha za moto Tanzania, je kuna sheria zozote zilizowahi kutungwa kusimamia matumizi ya silaha hizo. Nimeshasikia mara nyingi watu kuuwawa au kutishiwa kwa bastola kutokana na ubishi mdogo tu. Zaidi ya marehemu Ditopile aliyewa dereva wa daladala kwa jambo dogo tu, kuna mtoto wa waziri aliyeuwa mtu hapo kwetu Tabora kwa sababu ya kubishania msichana. Hapo Dar nimewasikia mastaa kibao kama vile Kanumba, Mbilinyi, na wengineo wakitishia wenzao kwa bastola. Tunahitaji sheria kali sana za kudhibiti matumizi ya silaha kali kwa vile zimezagaa sana nchini.
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa hukubaliani na hadithi na wewe unatunga hadithi nyingine.
  ukiondo case nyingine za silaha. Kama maelezo ya habari hayako biased jamaa likuwa na haki ya kujilinda pia.
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliana na wewe kwa asilimia 100%. Mwenye haki ya kutoa uhai wa mtu yeyote yule kwa mujibu wa sheria ni "Nyonganyonga" tu anapokuwa anatimiza hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama na kuidhinishwa na Rais wa jamhuri kwa mujibu wa katiba. kuna mambo mengi ya kufanya kama unavamiwa, moja likiwa ni kuita polisi lakini jingine ni kujihami kwa kukimbia kama haiwezekani ni kutumia minimum reasonable force. kinacholeta utata hapa ni kuwa kama ilikuwa kweupe mtu anakufuata na kisu kwa nini ulenge moyo?, ina maana alikusudia kuua. angeweza hata kumpiga mguu ili kumu-incapacitate ila inavyoelezwa kana kwamba vurugu zile zina-justify kuua. Nafikiri watu wanatakiwa kujua kuwa kuu kwa njia yoyote isikuwa ya kisheria ni kosa la jinai.

  Angetumia busara sana kwa kuwa anawafahamu waliokuwa wanafanya fujo hapo bara na kufuata sheria. Kama hawa jamaa walikuwa wanalipa kisasi kwa wenzao kuwekwa mahabusu bali tutarajie sasa kisasi kitazaa kisasi na ili kupunguza tension ni lazima mwenye bar ashitakiwe kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

  Binafsi kuna jamaa yangu mmoja aliisha wahi kupigwa na wamiliki wa bar moja kwa kuwa alikuwa ni baunsa wa bar nyingine na siku hiyo akaenda pale kujivinjari wakamfukuza akasema anatumia pesa yake, basi walimpiga kama mwizi na kumpakia kwenye landrover wakiwa na dhana ya kwenda kumtupa baada ya kuzimika, kuna jamaa mmoja alikuwa anakunywa bar ile akawasha gari na kuanza kuwafuata kwa nyuma na kuwaamuru wampeleke kituoni chang'ombe. wao walidhani amekufa na kusema ni mwizi alivamia bar yao na kupigwa na watu wenye hasira. Ila alipopelekwa hospital akaamka na kuanza kutibiwa. Kilichofuata ni kundi la rafiki zake mabaunsa kuvamia bar na kuichoma yote. Kisa hiki kinanikumbusha stori ile.
   
 5. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kweli sasa vijana wamepinda yaani mchana kweupe!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jul 15, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mojawapo ya matatizo yetu watanzania ni ni hii tabia ya kukubali kila tunaloambiwa kiasi kuwa hatuwezi kuliangalia kwa mapana namerfu. Mimi najitahidi kuliangalia kwa mapana na marefu; sijatunga hadithi nyingine kama unavyodai kwani sijasema kilitokea hiki au kile, ninachofanya ni kuuuliza maswali kulingana na maelezo yaliyotolewa.

  Inawezekana ndugu yangu nawe ni mmoja wa wanaoamini kuwa ukishakuwa na silaha kali basi unaweza kuitumia "kumwua- kwa kupiga risasi moyoni (kama picha ya marehemu ilivyoonyesha)" mtu yeyote atakayekufanyia jambo lolte la maudhi hata kama ni la kukuvunjia kioo cha gari au kukurushia jiwe kwa kombeo au manati; hapana, haki hiyo haiko hivyo. Unaruhusiwa kumwua mtu kama namna ya kujilinda iwapo tu kushindwa kumwua kutakuletea madhara ambayo hayatarekebishakika tena katika maisha yako yote, ikiwa pamoja na kupoteza uhai wako wenyewe au wa mtu mwingine.

  Hadithi iliyoko mbele yetu hapa hainyoneshi kuwa Saddam alikuwa anelta madhara ya aina hiyo. Kumbuka kuwa kuua kama nama ya kuadhibu ni ultimate penalty ambayo ikifanyika kwa makosa haiwezi kurekebishika.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kuna haja tena kubwa kwa serikali yetu tukufu kurejesha mfumo wa NGUVUKAZI. Haiwezekani vijana wanazagaa mtaani mchana kweupe bila shughuli za kujiongezea kipato halafu tunalalama eti sisi ni nchi maskini. Matokeo yake ndio haya kushinda baa na kufanya madudu yasiyo na kichwa wala miguu.

  BTW, RIP kijana aliyeondolewa uhai.
   
 8. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kubali kwanza hii hadithi uliyoipokea halafu fanyia uchunguzi au ngojea habari nyingine iliyo tofauti na hiyo ndio uanze kutoa maoni yako. haya mauaji hayakufanyika chumbani watu walikuwepo na ni kwenye public place kama hii sio sahihi basi utaipata sahihi. sasa hawa wtu na mapanga kwenda kushambulia mtu ndio sahihi au ndio mnataka kuendeleza uhalifu? vijana wa aina hii wako sehemu nyingi hapa Dar wanaachwa bila kuchukuliwa hatua kwa sababu Eti wananchi hawana uwezo wa kuchukua sheria mkononi baadae yanakuwa kama ya jana ya Prof kule salasala. inategemea uko kwenye mazingira gani ukingoja kuchukua hatua hata ya ya pili waweza usiifike na umauti utakuwa umauti utakuwa ushakufika.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  murder kivipi bana?
   
 10. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Huu kweli ni mwaka wa shetani, mauaji kila kona.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hadithi ya global publishers haijakaa kimantiki.......

  'walikuwa na silaha ikiwemo visu' ............silaha gani? na visu vya ukubwa gani?

  'alichomwa kisu lakini hakudhurika'..................alichomwa kisu wapi, katika mazingira yepi, ilikuwaje kisimdhuru?


  'baada ya vijana wengine wawili kujeruhiwa kwa risasi Saddam bado aliendelea kumfata mwenye bar na kupigwa risasi na kuuawa hapo hapo' ....hao vijana wawili nao pia walipigwa risasi baada ya mwenye Bar kufyatua risasi hewani au la?

  na hao mashahidi ni kuwa baada ya risasi kufyatuliwa hewani bado walikuwepo eneo la tukio wanatizama au?
   
 12. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,753
  Trophy Points: 280
  hivi watz hawaogopi BUNDUKI eeh.....kila mara utasikia mtu kauawa akijaribu kupambana na majambazi wenye silaha etc....sasa hawa vijana tena wanaleta u-gangstar mbele ya cha moto.....sheria haikulindi usiuawe,utakufa then sheria ndio itafuata mkondo
   
 13. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,753
  Trophy Points: 280
  na hao mashahidi ni kuwa baada ya risasi kufyatuliwa hewani bado walikuwepo eneo la tukio wanatizama au?

  watz pekee dunia nzima,bunduki ikilia wanakimbilia eneo la tukio kuangalia,kwahio usishangae mashahidi kuwepo hapo wakati risasi zikilia....
   
 14. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Duh! Mi chichemi kitu!!
   
Loading...