Kwa walimu waache tu wakatwe, tena hata zingekuwa zaidi ya hizo, ni haki yao tu. Maana hakuna watu mambumbu kama walimu Tanzania. Yaani hii ni kada ya wafanyakazi wa serikali wasiojua haki zao wala stahili zao halali. Ni watu wanaoonewa kunyanyaswa na kudharauliwa na serikali kupindukia lakini ndiyo wa kwanza pia kujipendekeza serikalini. Ukiwaambia tugome hawataki, tulikubaliana mwaka 2010, tugome kuandikisha na kusimamia uchaguzi, kuja kushitukia ndiyo kwanza baadhi ya walimu wamekwenda kuomba kabisa. Yaani walimu ni headache katika nchi hii. Acha tuumie tu, pengine siku moja tutaamka usingizini na kuelewa ni nini tunachokistahili.