Mwenge wabaini ufisadi wa TZS 65B kwenye miradi 49 ya halmashauri 38 Je, nini kitaendelea?

😂😂😂
Ule mwenge Kuna jambo si bure, ukute kuna matambiko ya kufa mtu, kama unaamini kwenye uchawi huna budi kuamini kwenye Mwenge...
Sina uhakika lakini, haiwezekani watu watumie gharama kiasi hiko...
Ndio kuna jambo ambalo ni,

Kuleta nuru kwenye giza
Kuleta amani kwenye mafarakano
Kuleta Upendo kwenye chuki
Kuleta furaha penye huzuni
Kuleta faraja kwenye kukata tamaa
Kuleta umoja kwenye utengamano
Kuleta heshima kwenye dharau,
Kumulika wezi na walanguzi
 
Ndio kuna jambo ambalo ni,

Kuleta nuru kwenye giza
Kuleta amani kwenye mafarakano
Kuleta Upendo kwenye chuki
Kuleta furaha penye huzuni
Kuleta faraja kwenye kukata tamaa
Kuleta umoja kwenye utengamano
Kuleta heshima kwenye dharau,
Kumulika wezi na walanguzi
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri,

Uzalendo unahitajika sana kwaajili ya Taifa hili
 
Uoga tu. Ndio maana na wao wanajua mwisho wao unakaribia wanakuja na visababu vya kipuuzi kama hivyo eti kumulika mafisadi sijui nini na nini?!

Wewe koroboi inamulika vipi mafisadi. Wanachofanya ni kuupotezea heshima yake kwa kizazi kipya sababu wanashangaa kitu cha kihistoria hadi leo bado kipo tu kwenye shughuli za kiserikali kina umuhimu gani?!
Mkuu naona hujajua vizuri kuhusu falsafa,
 
Mwenge wanusa harufu ya rushwa na ufisadi kwenye miradi 49 kati ya miradi 1,097 yenye thamani ya 1.2trilioni iliyozinduliwa | TZS 65b zahofiwa kutafunwa na mchwa,Je ni kweli Mwenge haufai? mnaosema Mwenge hauna faida hamfai kuchaguliwa hata kwenye jitongoji tu,​

" Chato tunasema Asante "​

Mtakumbuka Mwenge wetu wa Uhuru uliwashwa rasmi tarehe 17|05|2021 Makunduchi Zanzibar na leo tarehe 14|10|2021 Mwenge wa Uhuru Umefikia kilele chake Mkoani Geita ikiwa ni baada ya kumalizika kwa siku 150 za matembezi yake bara na Visiwani katika Wilaya za kiutawala 150,mikoa 31 sawa na jumla ya kilometa 21,480 hakika ni jambo la kupongezwa na hii ndio tofauti ya CCM na vyama vingine vinavyoupinga,

Mgeni rasmi alikuwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ( Chief Hagaya ) aliyeambana na DP Dk Philip Mpango,Rais wa Zanzibar na Mkt wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwingi,Waziri Mkuu wa JMT Mhe Khasim Majaliwa Majaliwa,Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma,Mawaziri,wabunge,wakuu wa wilaya na mikoa pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa vyama na Serikali,Kilele hicho asubuhi kilitanguliwa na Misa Takatifu ya kuwaombea Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere baba wa Taifa hili ambae leo ndio siku yake kitaifa,Hayati Julius Kambarage Nyerere alifariki 14|10|1999 lakini pia alikumbukwa na kuombewa Rais wa awamu ya Tano Hayati Dk John John Joseph Pombe Magufuli na baadae shughuli iliendelea katika Uwanja wa Magufuli Chato.

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru kabla ya kuhitimisha kilele chake umezindua Jumla ya miradi mikubwa 52 mkoani Geita,Kiongozi wa mbio hizi za Mwenge wa Uhuru Kitaifa alikuwa mwanamama Lt Josephine Mwambashi akisaidiwa CPL.Hafidhi Shaban, CPL. Mohamed Mbegu, CPL. Rehema Haji,Pte. Dismas Mvula na Lt Jofrey Juma Vijana hawa wanastahili pongezi kubwa na kwahakika tumeuona Uzalendo wao kwa Taifa lao walikuwa wakali kama nyuki Pindi wanapokuta miradi ya maendeleo ya Serikali haiko sawa hakika wanastahili,

Katika hali isiyoyakawaida Kiongozi wa mbio za Mwenge Lt Josephine Mwambashi alitoa ripoti ya mwenye iliyoonesha kuna harufu ya Rushwa na Ufisadi kwenye Jumla ya miradi 49 yenye thamani ya Tshs 65.34BL kati ya miradi 1,097 yenye thamani ya Tshs 1.2trilioni iliyozinduliwa nchi nzima katika Wilaya 38 ambazo Lt Mwambashi ameomba iundwe tume huru kwaajili ya Uchunguzi zaidi huku akimkabidhi Rais ripoti ya awali ya Takukuru huku Mhe Rais Samia Suluhu Hassan akiahidi kulifanyia kazi huku akishangaa wakati haya yote haya yanatokea RCs,RASs,DCs,DASs,DEDs,RASOs, DSOs wanakuwa wapi hadi Mwenge ufike na kuona madudu hayo?

Hitimisho hili limetanguliwa na siku nane ( 8 ) za kongamano la Vijana na hapa kipekee kabisa naomba niwapongeze sana Mhe Jenistha Muhagama Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Pamoja na Mhe Patrobas Katambi|Ummy Nderiananga manaibu wake Pamoja na Waziri wa michezo wa Zanzibar kwa kulifanya kongamano la vijana na shughuli nzima ya maandalizi ya mwenge kuwa yenye tija kwa Geita na Taifa kwa Ujumla wake,Miongoni mwaviongozi Mawaziri wakujivunia kama Taifa ni hawa watu watatu may The almighty God bless them wanajituma sana watu wa Geita watakubaliana na Mimi 100%

Kama Taifa tuendelee kuwaombea pumziko la milele na kufuata nyayo zao viongozi hawa Hayati Dk John Pombe Magufuli,Hayati Dk Benjamin Mkapa na Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere-Amina

IMG-20211013-WA0009.jpg

Waooh,

Kazi nzuri sana hii ya mwenge wa Uhuru,
Wenye dhamana kuweni makini acheni kucheza na pesa za watoto hawa wa masiki mwisho wenu utakuwa mbaya,
 
Kila siku huwa nawaambia serikali ya Jiwe ilijaa wezi na yeye akiwafumbia macho kwa sababu alijaza watoto wa Kanda pendwa.

Ulikuwa huwezi sikia mambo ya fushwa ,ukitamka tuu wanakufanya kitu mbaya yaani ni mwendo wa pambio za Jiwe na kujiita wazalendo huku wakiiba nchi.

Ukiitisha uchunguzi kwenye miradi ya Jiwe utastaajabu ya wazalendo majizi.
 
Mungu amsimamie Rais wetu anakwenda vizuri
 
Kila siku huwa nawaambia serikali ya Jiwe ilijaa wezi na yeye akiwafumbia macho kwa sababu alijaza watoto wa Kanda pendwa.

Ulikuwa huwezi sikia mambo ya fushwa ,ukitamka tuu wanakufanya kitu mbaya yaani ni mwendo wa pambio za Jiwe na kujiita wazalendo huku wakiiba nchi.

Ukiitisha uchunguzi kwenye miradi ya Jiwe utastaajabu ya wazalendo majizi.
Mkuu inbox
 
Machadomo yalisema mwenge hauna faida yataufuta,
Bila mwenge tungejuaje wizi wa haya mabilioni,
Yasichaguliwe sera zao ni tatanishi sana
Kwa hiyo CAG, TAKUKURU na TISS wafutwe, kubaki na mwenge tu. Huyo Kiongozi wa mbio za mwenge anapata wapi taarifa za matumizi mabaya ya fedha ?
 
No, Mkuu hata hiyo makala mbona imesema inaripoti ya TAKUKURU?

MWENGE NI WAMUHIMU KULIKO UMUHIMU WENYEWE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom