figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Rais Mstaafu, Dk Jakaya Kikwete akishika Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago Kiwangwa Bagamoyo.
My take:
Kauli mbiu ya mbio za Mwenge kwa mwaka huu inasema, “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU.”
Sasa naanza kuelewa umuhimu wa Mwenge huu kuwekwa Makumbusho. Mambo ya Kilimo kwanza yashapitwa na wakati, sasa hivi ni Tanzania ya Viwanda.
Kama wamekosa viwanda bora upite Mashuleni uhamasishe kutokomeza zero.
Ombi langu
Namuomba rais Magufuli awatumbue wote wanaoturudisha nyuma na kufifisha mkakati wetu wa Tanzania ya Viwanda kwa kuendelea kukumbatia Sera zilizoshindwa. Huu ni usaliti kwa Serikali ya Magufuli kuendeleza Kilimo kwanza wakati ni Wakati wa Viwanda.
Hatuwezi kuendelea bila kuwa na dhamira moja. Tumuunge mkono rais Magufuli, tufikie Viwanda.
Sababu 2020 ikifika bila Viwanda, anaweza sema mimi nilikuwa natekeleza Tanzania ya Viwanda ninyi mkanisaliti kwa Kilimo kwanza ndo maana hatukufanikiwa.
Kama kweli tulimchagua tumuunge mkono.
Hadi Sasa sijaona Sababu ya kuachana na Kilimo kwanza na Big Result Now na kujikita na Tanzania ya Viwanda. Ujumbe umefika
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni