chuma cha mjerumani
JF-Expert Member
- Dec 4, 2013
- 11,118
- 22,505
Aliekuwa anampiga zaidi siajabu katoka kuzini na mke wa mtu.
Mbona wanaokuibia mabilioni huwakatishii maisha yaohuyo ni mwizi chokoraa
Tena tuna watukuza na kuwasifia wanafanya 1 wrong choice mamilioni wanateseka wengine wanakufa.... lakini hata hatuwezi kuwarushia ata jiwe.Wale wezi wa T1.5 mnawapigia makofi barabarani
Hapo ndipo nguvu za wanaume wa dar zilipo tu. Kupiga mwizi wakiwa kikundi. Kwetu mwizi anakimbizwa na mtu mmoja na anachezea kichpo cha mtu mmoja hadi anakua uji uji
Wangemvunja mkono wamwache ,,,,,,,,Japo Wanaudhi sana na kukera Ila wamefanya Maamuzi magumu mno ya kumuua
hawa wana kitu hivyo wanastahili kupongezwa na kuimbiwa wimbo wa sifa kwa kuwa ni wajanja eti walitumia fursa vizuri.Mbona wanaokuibia mabilioni huwakatishii maisha yao
Kijana nimependa sana wazo lako ps njoo PM nowifike wakati kabla ya kufanya maamuzi hebu tujaribu kufaa viatu vyao na tuone ingekuwa sisi tungefanyaje? imenichukua muda mrefu kuamua kusoma uzi huu kwa kufikiria uchungu na mateso aliyoyapata mtoto huyu kwa yaliyotokana na malezi mabaya au kutowajibika kwa wazazi.
upo uwezekano mkubwa watoto hawa walikataliwa na baba zao au hawakutendewa haki kwenye jamii kama watoto wengine ikawalazimu wajikatae na kuwa machokoraa achilia mbali waliotolewa kafara kuwa hivyo kwa ajili ya biashara za jamaa zao hapo mjini na leo inawezekana tukaona ni kifo cha kawaida kumbe ndo hatua za ukamilisho kuwa msukule zimekamilika.
binadamu tumekuwa watu wa roho mbay tunajari fedha na mali kuliko uhai wa mtu huwenda wangemkamata wakampeleka polisi njiani wakati wa kumuhoji mtoto angeweza kukutana na huruma zenu ambazo zingemfanya awe sehemu nyingine kimaisha siku zijazo.
jamii inatakiwa ijifunze kutafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi si swala la hasira hizi damu ndizo zinazotugharimu kwa kuwa zinalaani nchi.
Hapa ndipo wanapokosea kulazimisha mambo utakuta mtu kamkataza usiafishe lakini yeye katumia nguvuWafe tu kuna mmoja aliwahi kufuta gari ya mtu aliponyimwa hela akatoa chuma akachuna ile gari kuanzia mwanzo hadi mwisho
Hawa watoto ni wezi huwezi kupatia ajira nyumbani kwako,wameisha haribikiwa kichwani siku nyingiDaaaah hapana kwani hata kumvunja mkono ni adhabu kubwa sana kwani ingewezekana hata kumpa kumchukua yule toto na kumpeleka home na kumpa hata kazi ili aondokane na Maisha ya mtaani
We acha tu nilitamani hata kuingilia kati ila nilikuwa Siti ya nyuma sana kwa daladalanoma sana,kwa nini hukupiga simu police kituo si kipo nyuma ya stand tu apo! not making sense wezi wakubwa wa mabilio mnawaacha wanakula viyoyozi mdokozi wa wiper anauwawa asbh na mapema! aibu kubwa sana.
Hawaniibii mimi wanachukua pesa walizokusanyaMbona wanaokuibia mabilioni huwakatishii maisha yao