kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,931
- 7,828
ukiangalia hii dhana ya mradi wa DART utaona ni dhana sahihi kutatua tatizo kubwa la usafiri wa umma katika jiji la Dsr es Salaam. Dhana ya bus transit sio ya zamani imeanza mwishoni mwa miaka ya 1990. Miji ya kwanza kujengwa rapit transit ilikua kule amerika ya kusini Curitiba Brazil na Bogota Colombia. Pia China kuna miji mingi tu wamejenga mifumo ya Bus Transit.
Mfumo wa bus transit unahusisha ujenzi wa njia maaluum kwa mabasi ya usafiri wa umma tu na uwepo wa kampuni za kuendesha usafiri wa mabasi katika njia hizo. Kampuni zinaweza kua za umma au binafsi inategemea umiliki upi utakua na tija. Tatizo wazi linaloonekana kwetu kwa jiji la Dar es Salaam ni kushindwa kuanzisha kampuni bora yenye weledi ya kuendesha usafiri baada ya ujenzi wa barabara za DART.
Kwanza kabisa mradi wa ujenzi wa Bus Transit lazima ujenge depot ambapo kunakua na karakana ya huduma ya kiufundi, bohari la vipuri, kituo cha kujaza mafuta, uwanja wa kuegesha mabasi na jengo au majengo ya utawala. Ukiona mahali DART wamejenga depot hapa jijini utashangaa maana ni kwenye mkondo wa maji mto msimbazi ambapo maji hutuama na kuwepo mafuriko kwa mvua kidogo tu. Sijui mtaalaam gani alishauri kujengwa hapo depot. Kampuni inayoendesha mradi bila shaka imepata hasara kubwa kwa uzembe uliyofanyika.
Jambo la kushangaza maeneo mawili mali ya serikali ambapo yangefaa kabisa kua depot za mabasi kwa mradi wa DART ni iliyokua depot ya UDA kurasini na ile iliyokua depot ya UDA Ubungo. Badala yake maeneo hayo yaliyokua kwa miaka mingi ni kwa ajili huduma ya usafiri wa umma jijini yamepewa kampuni binafsi kwa shughuli zingine. Kurasini kuna kampuni ya GSM wanaendesha depot ya makontena na Ubungo kuna mtu amepewa kujenga majengo ya kukodisha kwa biashara. Kama navyojua mimi mradi wa DART hauna depot yoyote ya uhakika.
Inaelekea wapanga mipango wao wanaona kutoa kandarasi kwa ujenzi wa barabara za DART ndio kazi imeisha. Hivi sasa ujenzi upo njia zote zilizopangwa mpango wa DART. Kutokana na ujenzi huo huduma ya usafiri wa umma imevurugika sana. Kuna msongamano wa magari kila njia. Kampuni ya UDART iliyopewa kutoa huduma inaonekana kukosa weledi kwa kiwango kikubwa. Kati ya mabasi kama 300 waliyoanza nayo miaka michache ni mabasi 60 tu tumeambiwa yanafanya kazi. Mengine yamesimama kwa ubovu. Inavyoelekea tutagharamika kujenga barabara maalum za mabasi huku huduma nzuri iliyotarajiwa ikikosekana