Nini maana ya msemo 'Mwenda tezi na omo marejeo ngamani'

ninavyo elewa mimi ni kwamba zunguka unavyozunguka, tafuta unavyotafuta lakini mwisho wa siku utarejea nyumbani (ngamani) tezi na omo ni pande za ngalawa (mbele na nyuma) ngamani ni pale katikati kwenye lile tanga.
 
Hii methali inamaanisha kuwa yule mtu ambaye anakwenda mbele na nyuma, mwishowe huwa hana msimamo.
Anaye hangaika huku na huko, mwisho wa siku hutulia mahali salama kwake.

Hii ni iwapo tezi na omo ina maana mbele na nyuma ya jahazi na nga'amani ni katikati ya jahazi.

Hivyo ukienda mbele, itayumba na ukienda nyuma itayumba. Mwisho wa siku itakubidi ukae katikati ili mambo yawe sawa
 
ninavyo elewa mimi ni kwamba zunguka unavyozunguka, tafuta unavyotafuta lakini mwisho wa siku utarejea nyumbani(ngamani) tezi na omo ni pande za ngalawa (mbele na nyuma) ngamani ni pale katikati kwenye lile tanga
good answer
 
Umepiga ndipo
 
MKUU WEWE KUNA UWEZEKANO NI MZARAMO KABISAAAA.NAKUPONGEZA MKUU WANGU WA KAZI
 
ZINAITWA NI MINYORORO
nimeitoa mahali hii

Je, wajua ngamia inayosemwa kupenya tundu la sindano sio yule mnyama ? Ni ngamia kamba nene na ngumu aghalabu hutumiwa kutilia nanga vyombo vya majini hususani meli. via: #probeatz.ga

Umoja Wa Walimu Wa Somo La Kiswahili Tanzania - UWASOKITA
 
duu aisee mimi nilifikia karibu kama Kichaa.Sikwenda mbali hivo.Ila mzee baba basi uko vizuri sheikh
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom