Mwema kuwapa donge nono polisi wanaokataa rushwa

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema.[FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la Polisi nchini, limetangaza mkakati wake wa kukomesha vitendo vya baadhi ya askari wake kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwazaidia kiasi cha fedha walichokataa kupokea.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mpango huo ulitangazwa na mkuu wake, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema juzi wakati akizungumza na vikosi kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, mjini hapa.[/FONT]

“[FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la polisi sasa rushwa basi, tunataka kuaminiana na wananchi wetu…Tanzania nzima kati ya Januari na Machi kama kuna askari aliyekataa rushwa ya kiasi chochote kwa ushahidi, atalipwa kiasi hicho, hata kama ni milioni 10” alisisitiza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema, hatua hiyo ndiyo njia pekee itakayosaidia kumaliza tatizo la rushwa ndani ya jeshi hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa na kutuhumiwa kuwa linajihusisha na vitendo hivyo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwataka askari watakaoendelea kujihushisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa wajiondoe mapema katika jeshi hilo, vinginevyo watakabiliwa na hatua kali za kisheria.[/FONT]
“ [FONT=ArialMT, sans-serif]Kula rushwa ili uuze haki ya mtu ni dhambi, una mdhalilisha mtu… gharama ya mtu anayekupatia rushwa inataka umdhulumu mwingine haki jambo ambalo ni la hatari sana kwa maendeleo ya nchi, ” alisistiza Mwema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwaagiza makamanda wa mikoa nchini wapokee, kuyapitie na kumpatia majina ya askari waliokataa kupokea rushwa kati ya Januari hadi Machi 2, mwaka huu hata kama ni Sh milioni 10,000 jeshi hilo limpatie mara moja.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Vilevile aliwatahadharisha wagombea na wapiga kura watakaoshiriki kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu wasijihusishe na rushwa.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema yeyote atakayepuuzia agizo hilo atakumbana na mkono mrefu wa Serikali kwa madai kuwa safari hii polisi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kukomesha tabia hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mwema yupo katika ziara ya siku tano mkoani hapa ikiwa ni ya kwanza kuifanya tangu ateuliwe na Rais Jakaya Kikwete kuliongoza Jeshi la Polisi.[/FONT]CHANZO: NIPASHE
 
SHUPAZA

SHUPAZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2009
Messages
556
Likes
7
Points
35
SHUPAZA

SHUPAZA

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2009
556 7 35
Sasa mbona ofisini kwetu hatujaambiwa wenzetu wanakula rushwa kama kawaida tunaomba utoke waraka
 
K

Kabengwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2009
Messages
242
Likes
6
Points
35
K

Kabengwe

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2009
242 6 35
Kwenye hili, nnapata tabu kuelewa ni jinsi gani hili zoezi litafanikishwa!

Kumrudishia askari kiasi kile kile alichotaka kupewa kama rushwa?!

Bado hainiingii akilini hilo zoezi litafanyikaje!
Na kwann wasifanye kuwaongezea askari mishahara kama hizo hela za kuwagawia zipo, coz tatizo la wao kupokea rushwa ni mishahara kuwa midogo sana. Au anataka wawe wanasingizia wametaka kupewa rushwa ya kiasi kadhaa kila siku?!

Sijui ni kitu gani Mwema anachofikiria mpaka kutoa hii kauli, na ukizingatia askari wetu wapo kila kona ya nchi!

Sijui ni kiasi gani kitakachokuwa kinalipwa kila siku ili kuwa compansate askari wanao rubuniwa kwa rushwa?!

Bado nipo gizani ya jinsi gani hili zoezi litafanikiwa!
 
Masikini_Jeuri

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
6,803
Likes
380
Points
180
Masikini_Jeuri

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
6,803 380 180
Aaah! Wonders will never ceaseto happen!

Na hili ni mojawapo

Kabengwe ndugu yangu, watu wote wenye akili wanapata sana shida kila wafikiliapo hil na mengine mengi yanayofanana na hili; hivi ndio namna tunavyotatua suala la rushwa kwa baadhi ya askari wetu?
1. Unaanzia wapi kumatch hicho kiwango ; ama utaamini tu maneno ya askari husika?
2. wapi unazitoa hizo pesa za ku match kiwango anachotaka kuhongwa?

jamani eeh hebu tupumzisheni na hizi kauli zenu zisizo na mashiko VICHWA VINAUMA karibu tupatwe na mishtuko ya mioyo kwa kutoamini tunayoyasikia kama yanatoka kwa mliokabidhiwa madaraka kwa niaba yetu; hivi ni kwanini mmetugeuza wabongo wote mambumbu?
 
M

malope

New Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
1
Likes
0
Points
0
M

malope

New Member
Joined Feb 9, 2010
1 0 0
Nasikitikia kazi nzuri anafanya but washika dau wake wamekuwa cronic kwa rushwa, sijui atatumia sindano gani maana **** isa kuwa jiwe.mimi leo nimesimamishwa barabarani afande akinituhum makosa nisiyoyajua baada yakukagua gari na kukosa hitilafu,anatoa vitisho chungu nzima,anadai rushwa kwa nguvu na anapokelea kituoni,ajabu jana tu mh.aliwaasa kutowabambikia raia kesi,tutapona babaa!

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema.[FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la Polisi nchini, limetangaza mkakati wake wa kukomesha vitendo vya baadhi ya askari wake kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwazaidia kiasi cha fedha walichokataa kupokea.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mpango huo ulitangazwa na mkuu wake, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema juzi wakati akizungumza na vikosi kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, mjini hapa.[/FONT]

“[FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la polisi sasa rushwa basi, tunataka kuaminiana na wananchi wetu…Tanzania nzima kati ya Januari na Machi kama kuna askari aliyekataa rushwa ya kiasi chochote kwa ushahidi, atalipwa kiasi hicho, hata kama ni milioni 10” alisisitiza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema, hatua hiyo ndiyo njia pekee itakayosaidia kumaliza tatizo la rushwa ndani ya jeshi hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa na kutuhumiwa kuwa linajihusisha na vitendo hivyo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwataka askari watakaoendelea kujihushisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa wajiondoe mapema katika jeshi hilo, vinginevyo watakabiliwa na hatua kali za kisheria.[/FONT]
“ [FONT=ArialMT, sans-serif]Kula rushwa ili uuze haki ya mtu ni dhambi, una mdhalilisha mtu… gharama ya mtu anayekupatia rushwa inataka umdhulumu mwingine haki jambo ambalo ni la hatari sana kwa maendeleo ya nchi, ” alisistiza Mwema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwaagiza makamanda wa mikoa nchini wapokee, kuyapitie na kumpatia majina ya askari waliokataa kupokea rushwa kati ya Januari hadi Machi 2, mwaka huu hata kama ni Sh milioni 10,000 jeshi hilo limpatie mara moja.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Vilevile aliwatahadharisha wagombea na wapiga kura watakaoshiriki kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu wasijihusishe na rushwa.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema yeyote atakayepuuzia agizo hilo atakumbana na mkono mrefu wa Serikali kwa madai kuwa safari hii polisi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kukomesha tabia hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mwema yupo katika ziara ya siku tano mkoani hapa ikiwa ni ya kwanza kuifanya tangu ateuliwe na Rais Jakaya Kikwete kuliongoza Jeshi la Polisi.[/FONT]CHANZO: NIPASHE
 
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,563
Likes
1,591
Points
280
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,563 1,591 280
hivi wewe IGP unafikiria haya mambo kabla ya kutaamka au unaongeaongea tu?polisi akamate rushwa??yethu na maria sijui kama itawezekana.Na ikiwa hivyo basi Yesu atarudi
 
nyaunyau

nyaunyau

Senior Member
Joined
Oct 28, 2009
Messages
122
Likes
8
Points
35
nyaunyau

nyaunyau

Senior Member
Joined Oct 28, 2009
122 8 35
kaaaaaaaaaaaaazi kwelikweli vijana wake wanamuumiza kichwa.
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280
Kweli wanaokataa rushwa wazawadiwe, lakini….

Maoni ya katuniJuzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, alitangaza mpango kabambe wa kuwazawadia askari polisi wanaokataa kupewa rushwa na kwamba chombo hicho kina uwezo wa kuwazawadia hata Sh milioni 10 watakaokataa kupokea.
Mwema alisema mkakati huo ni sehemu ya kampeni za Jeshi la Polisi kusema ‘sasa rushwa basi’ ili kujenga imani ya chombo hicho kwa wananchi. Hakuishia hapo tu, alieleza wazi kwamba rushwa inapora haki, kudhalilisha na ni dhambi, kwa maana hiyo haikubaliki kwa misingi yote, kijamii hata kiimani.
Aliwakumbusha askari polisi kwamba ni lazima wabadilike hasa kwa kuacha kupokea rushwa, aliweka wazi kwamba wanaoendeleza vitendo hivyo ama wajiondoe wenyewe kwenye chombo hicho au watawajibishwa na hatua kali za kisheria kuchuliwa dhidi yao.
Katika kutambua askari watakaokataa rushwa, IGP Mwema alisema makamanda wa polisi wa mikoa wahakikishe ushahidi wa hali hiyo na ikibainika pasi na shaka yoyote, basi askari husika azawadiwe mara moja.
Sisi tunapongeza hatua hizi anazobuni IGP Mwema katika kulisafisha na kulipanga upya jeshi hilo; tunatambua fika kwamba tangu akalie kiti hicho amejitahidi kadiri ya uwezo wake kurejesha heshima ya chombo hicho kwa umma hasa hali ya sasa inapolinganishwa na ilivyokuwa wakati wa mtangulizi wake.
Kila tukitafakari tunaona uzito wa kazi inayomkabili IGP Mwema, hakuna ubishi kwamba Jeshi la Polisi lina changamoto nyingi na nzito; wapo askari wanaotuhumiwa kwa ukiukaji wa maadili uliotopea; wapo ambao maisha kwao bila kuwabambikizia raia kesi, hakuna.
Wapo ambao wanatuhumiwa kushirikiana au kusaidia wahalifu. Hawa wanawapa kinga kama ya kutokamatwa baada ya kupokea kitu kidogo kwao, lakini pia jinsi walivyogeuza raia kuwa ni migodi yao ya kuchuma, hata wahalifu hufanywa vivyo hivyo.
Kwa miaka mingi uhusiano baina ya raia na polisi umekuwa wa kutokuaminiana, wapo raia waliotendewa mambo mabaya kiasi cha kukata tamaa kufikisha suala lao polisi; wapo ambao wakisimulia mikasa iliyowakuta huwezi kujizuia kupandwa na mori wa kulipa kisasi, pengine kutamani kusukwa upya kwa Jeshi hilo.
Polisi pia wana changamoto za kuishi mazingira magumu, ujira usiofanana na uzito wa majukumu yao, lakini kibaya zaidi wakitakiwa kuvumilia shida wakati wanaona wazi kwamba ndani ya nchi yao wapo wanaonufaika zaidi na keki ya umma wakati wengine wanataabika; hii yote ni mizigo anayostahili kuibeba IGP Mwema kama kweli anataka kubadili hali ya mambo ndani ya chombo hiki.
Pamoja na changamoto hizo, kuna suala la mchakato mzima wa ajira ya askari polisi; je, kuna utaratibu gani wa kina wa kuwachuja kabla ya kujiunga na jeshi hilo? Je, kuna utaratibu gani wa kina wa kuendelea kuwachunguza mwenendo wao wakiwa kazini? Nani hasa anawajibika na kazi hii? Kuna chombo huru cha kufuatilia mwenendo wao au wanajichunguza wenyewe na kusafishana wenyewe?
Kimfumo kuna mambo muhimu ya kufanya katika uchukuaji wa askari wanaojiunga na Jeshi hili; kwa mfano ni kwa kiwango gani umma unahusika kumtathmini askari aliyeajiriwa? Ni kwa kiwango gani polisi wanatambuliwa na jamii anayohudumia?
Serikali imekuwa ikizingumza habari ya kupeleka madaraka zaidi kwa wananchi, ndiyo maana siku hizi hata shule za sekondari zinasimamiwa na halmashauri; kama utaratibu ni huo, inakuwaje basi kila askari polisi awajibike makao makuu ya polisi, kwa nini jamii isihusike katika kumtathmini juu ya mwenendo wake na kuwa na njia zilizokubalika ambazo wahusika wanakofanyia kazi wataeleza yote yanayomhusu.
Mwisho kuna suala la mafao bora kwa askari, si jambo zuri kuwaacha askari wakiishi maisha ya ombaomba, ni utaratibu usiofaa kwa wafanyabiashara kuwa ndio wanaotoa misaada mingi ya kusaidia uendeshaji wa shughuli za polisi katika maeneo yao; kuna taarifa za kutoa mafuta, spea za magari na nyenzo nyinginezo kwa jeshi.
Ufadhili huu kama unatolewa labda uwe kwenye ngazi ya kitaifa kisha vitu hivyo visambazwe nchi nzima bila kujali vilikotokea, vinginevyo kila RPC akikubali kufadhiliwa hiki na kile ndio mwanzo wa kulea uhusiano usiochangia ufanisi na tija kwa jeshi hili. Tunarudia kuunga mkono juhudi za IGP Mwema katika kusafisha chombo hiki adhimu kwa ulinzi na maisha ya raia, lakini changamoto bado ni nyingi na zinahitaji kukaza buti zaidi ili kupiga hatua za maana.CHANZO: NIPASHE
 
Forum statistics

Threads 1,250,967
Members 481,547
Posts 29,752,891