Mwekezaji amchoma moto raia Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwekezaji amchoma moto raia Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 11, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,056
  Trophy Points: 280
  Mwekezaji amchoma moto raia Dar


  na Hellen Ngoromera  RAIA wa Kiasia anayehusishwa kumiliki hoteli moja maarufu iliyopo Kigamboni anadaiwa kumjeruhi kwa kumchoma moto mkazi wa Mjimwema, Lila Hussein (25), baada kuingia hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana, ndugu wa majeruhi huyo, Abdullah Saiwaad,alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi majira kati ya saa 5:00 na 6:00 usiku.

  Alisema kabla ya kuchomwa moto, Lila ambaye amelazwa wodi namba 7 katika Hospitali ya Temeke akiwa hajitambui, alivuliwa nguo kisha kumwagiwa mafuta ya petroli na kwamba amejeruhiwa vibaya kuanzia sehemu za magotini hadi shingoni.

  Alisema chanzo cha tukio hilo ni Lila kuingia kwenye muziki hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
  "Hali ni tete, Lila yupo hospitali ya Temeke akipigania maisha yake baada ya kuchomwa moto na mhindi ambaye ni mmiliki wa hoteli ya South Beach, ameungua vibaya tunamwomba Mungu anusuru maisha yake," alisema Saiwaad.

  Alisema baadaye aliokolewa na wafanyakazi wawili baada ya kuamua kupeleka taarifa kijijini Mjimwema.
  Kutokana na tukio hilo wanakijiji wametishia kuchoma moto hoteli hiyo na kwamba hali hiyo imesababisha mkuu wa kituo cha Kigamboni kupeleka askari wa doria kusimamia usalama hotelini hapo.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Davis Misime, alikiri kuwepo kwa taarifa hizo na kuahidi kuzifuatilia kwa kina. Kwa mujibu wa Misime, usiku askari walipata taarifa kuwa kuna mtu amechomwa moto hotelini hapo ndipo walipokwenda na kumchukua majeruhi na kumpeleka katika kituo cha afya Kigamboni kisha baadaye kupelekwa Temeke. Hata hivyo, habari zinapasha zaidi kwamba baadaye jioni ya jana, Lila alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na hali yake kuwa mbaya.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Dawa ni Wananchi kuichoma Guest House cum Hotel ya South Beach haraka sana iwezekanavyo ... Mmiliki amechukua mamlaka basi na wananchi hawana budi kutenda vivyo hivyo!
   
 3. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  dawa kuchomewa g house
   
 4. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tusishangae huyu aliyetenda unyama huu akalindwa
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Huwa naumia sana nikisikia haya mambo yaani muuza vitu vidogovidogo Kariakoo mtanganyika anaitwa machinga na mchina biashara hiyo hiyo anaitwa mwekezaji!
   
 6. F

  Fedrick Lumambo Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli dawa ni kuichoma hiyo Hotel pamoja na huyo mmlika asiye kuwa na hata chembe ya ubinadamu
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hivi hiyo guest house bado tu haijawa majivu mpaka muda huu???:disapointed:
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni kweli kabisa

  Palikua na purukushani kubwa sana jana usiku na nadhani watu wanaokwenda south beach wawe waangalifu sana... vijana wa mjimwema ni wema sana ila wakiapiza kufanya kitu, basi watafanya tu!!!

  Lakini haya yote yanatokana na nini?
   
 9. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  hawa wahindi wanaona bongo ni pepo yao hawa tukiiondoa CCM na wao waunge tela kuhama nchi vinginevyo watakiona:rip:
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Wahindi wanatudharau sana watu weusi!naunga mkono SBR ichomwe moto!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  mimi nawalaumu hawa wananchi, badala ya kwenda kupiga moto hotel wao wanatoa onyo
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,056
  Trophy Points: 280
  Mwekezaji huyu ashughulikiwe
  Tanzania Daima

  MOJA ya habari za gazeti hili leo inahusu hatua ya wananchi wa Mjimwema, Kigamboni, jijini Dar es Salaam kuvamia Hoteli ya South Beach, wakitaka kulipiza kisasi kwa mwekezaji anayedaiwa kumchoma moto mwenzao, anayetambuliwa kwa jina la Lila Hussein (25).
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo na zilizoripotiwa na gazeti hili tangu juzi, mwananchi huyo alivuliwa nguo na kumwagiwa mafuta ya petroli na mwekezaji wa hoteli hiyo kisha kuchomwa moto kwa sababu aliingia kwenye ukumbi wa muziki wa hoteli hiyo bila kutoa kiingilio.
  Itiliwe maanani kuwa kutokana na kufanyiwa kitendo hicho, mwananchi huyo alijeruhiwa vibaya kuanzia sehemu za shingoni hadi magotini na hadi jana alikuwa amelazwa kwenye wodi namba 7 katika Hospitali ya Temeke akiwa hajitambui.
  Kwa mtazamo wetu, kitendo kilichofanywa na mwekezaji kama ilivyoelezwa ni cha ukatili wa hali ya juu na kisichojali utu wa binadamu, kinapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kuhakikisha kinakomeshwa ili vitendo vya namna hiyo visiendelee kutokea ndani ya nchi yetu.
  Haikuwa sahihi hata kidogo kwa mwananchi huyo kuvuliwa nguo na kuchomwa moto, kwa vyovyote vile kilichofanywa ni ukatili kwani hata kama ni kweli mwananchi huyo aliingia kwenye muziki hotelini hapo bila kutoa kiingilio, bado utawala wa hoteli hiyo ungeweza kumkamata na kumchukulia hatua kwa kumfikisha kwenye vyombo vya dola kama polisi na hatimaye mahakamani ambako tuna uhakika asingehukumiwa kuchomwa moto bali angepewa adhabu inayostahili kwa mujibu wa sheria.
  Izingatiwe kuwa kutokea kwa kitendo hicho kulithibitishwa pia na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Davis Misime, ambaye aliahidi kulifuatilia suala hili na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.
  Tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu akiwemo Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Salim Noto(53) kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo, wengine wakiwa ni Meneja wa hoteli, Salum Nassoro na John Mkwanjiombi, ambaye ni dereva. Kama inavyobainishwa na habari yetu ya leo kuhusu sakata hilo, wananchi wenye uchungu dhidi ya ukatili uliofanyika, waliivamia hoteli ya mwekezaji huyo wa Kiasia na Jeshi la Polisi lililazimika kufyatua risasi kuwatawanya wananchi hao waliodaiwa kuwa walikuwa wakifanya fujo.

  Hatuungi mkono wananchi hao kujichukulia hatua mkononi na kutaka kumwadhibu mwekezaji huyo wenyewe, lakini tunaamini kama hatua kali za wazi na za haraka zingechukuliwa dhidi ya mwekezaji huyo na watendaji wake wote katika tukio hilo, wananchi wangeridhika na pengine wasingefikiria kujaribu kujichukulia sheria mkononi. Wakati tukiwasihi wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi, tunachukua fursa hii kuvitaka vyombo vya dola kumchukulia hatua kali mwekezaji huyo ili kukomesha vitendo hivyo vya unyanyasaji wa kibinadamu. Aidha, serikali iliyowajibika kumleta mwekezaji huyo aliyefikia hatua ya kuchoma moto wananchi, ichukue mara moja jukumu la kumhudumia majeruhi huyo na kunusuru maisha na mateso yake. Tanzania Daima tunafuatilia kuhakikisha mwekezaji huyo anashughulikiwa.


  [​IMG]


  [​IMG]
   
 13. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  oho mungu tusaidie waja wako
   
 14. M

  Maimai Senior Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  amekosa nini. Hawa get crusher ndo adhabu yake
   
 15. K

  Kivia JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huyu kijana nilimuona muda mfupi baada ya kuchomwa, kweli hali ni mbaya saana. Ameungua saaaana.
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  siamini hii kauli

  Rostam anapokelewa na walinzi, mwenye shida ya mlo mmoja mnamchoma moto?
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Daaah. Ukatili wa hali ya juu. Alichofanya na alichofanyiwa hata haviendani.
   
 18. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hivi hoa wananchi huko wanasubiri nini kumtia kibiriti huyo Muhindi maana nae anastahili moto ili aona raha yake
   
 19. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  nahisi hauko sawa akilini mwako kama kweli wewe ni mtanzania ila kama wewe ndio muhindi uliemchoma moto huyo kijana wa watu basi jiandae nawe utachomwa moto na hiyo hotel yako ******
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Siku hizi kila mtu anaitwa mwekezaji hata kama amekuja nchini kuuza maji
   
Loading...