Mwekezaji amchoma moto raia Dar

jamani - kweli hii inauma sana. Wakati adhabu ya mtu kula mlo hotelini ukawa huna malipo adhabu ni kuosha vyombo - sasa huyu kuingia tu bila malipo - ndio kuchomwa moto - hivi ingekuwa kijana wa kihindi angemfanyia hivyo????

naamini hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki (mhindi) wa hotel hiyo.

Mungu ampe kupona kijana wa watu.:angry::angry:
 
Lazima hapo Sheria ichukue mkondo wake kwa huyo muwekezaji bila kujali fedha, utaifa wake.

hakika amefanya kitendo cha kinyama sana huyo.
 
Wakuu labda huyo mwekezaji hajui vituo vya polisi vilipo anajua tu anapohifadhi viberiti. Itapendeza kama ataweza kupelekwa kuexperience maisha ya Segerea, huko atatuliza akili kuliko sasa anavyopata upepo wa South Beach unaovuruga mbongo na utashi wake.
 
amekosa nini. Hawa get crusher ndo adhabu yake

bora wa tz tuambizane ukweli, kila siku tunachoma moto watu walioiba kuku au cellphone lakini huyu kamudhibu mwizi wake tunakuja juu. Jiangalie.
 
Sina hamu kuchangia.Kumbe mambo ya walevi !.
Walevi ni walevi tu wakiwa waasia au wauropa.
Habari imepotoshwa hilo ni baa,siio hoteli.Hakuna uwekezaji katika baa,ni uhuni tu.
Hata wakiuwana sina habari nao.
 
Mbona hueleweki mkuu.
Sina hamu kuchangia.Kumbe mambo ya walevi !.
Walevi ni walevi tu wakiwa waasia au wauropa.
Habari imepotoshwa hilo ni baa,siio hoteli.Hakuna uwekezaji katika baa,ni uhuni tu.
Hata wakiuwana sina habari nao.
 
Dawa ni kuikabidhi hotel hiyo kwa familia ya marehemu maana Lila hatunaye tena duniani.

Mungu ailaze roho ya marewhemu mahali pema.

Hivi hiyo guest house bado tu haijawa majivu mpaka muda huu???:disapointed:
 
Jamani tuache munkari na tuwe REALISTIC katika haya mambo. Ni mara ngapi tunashuhudia na kushabikia wadogo zetu wakichomwa moto mitaani, kisa tu mtu kaiba au kasingiziwa kuiba nazi sokoni? Sasa leo inatuuma kwa sababu LABDA aliyotoa amri ya kufanya hicho kitendo ni MUHINDI?

Hili ni fundisho kubwa sana kwetu, kwani pengine kesho akawa mwao, au wewe mwenyewe pale watu watakapo kuzingishia au kukutuhumu kwa wizi na watu wakaamua kuchukua sheria mikononi mwao. Tukumbuke kwamba siku zote MTENDWA AKITENDWA ndio huwa na majonzi makubwa na kuhusi ameonewa.
 
Back
Top Bottom