Baada ya Mheshimiwa Rais kuzindua mradi mkubwa wa maji jijini Mwanza, wananchi tuliamini kuwa adha ya maji ilikuwa imefikia mwisho. Lakini hali ya sasa ni aibu kwa taifa na mateso kwa wananchi.
UKWELI TUNAUJUA NA TUNAUISHI:
UKWELI TUNAUJUA NA TUNAUISHI:
- Maji hakuna kabisa katika maeneo kama Nyegezi, Buhongwa, Butimba, Mkolani na mengineyo.
- Mgao wa maji haupo tena – hakuna ratiba, hakuna taarifa, hakuna majibu!
- Wananchi wamehamia mitoni na mabondeni kutafuta maji, huku vigogo wakifurahia maji kila siku.
- MWAUWASA wanatoa kisingizio cha "umeme kutotulia" – lakini TANESCO hawajathibitisha lolote. Ni kweli au ni siasa ya maji? Umeme upo mwauwasa wanadia Tanesco wana unstable power🤔
- Mradi mkubwa unaonekana kuwa mateso mapya kwa wanyonge, badala ya kuwa suluhisho.
TUNATAKA UKWELI – MSIMFICHE RAIS!
Mheshimiwa Rais ametimiza wajibu wake.
Lakini ukweli ni kwamba – hadi sasa, maji bado ni adha kubwa sana kwa wananchi wa Mwanza.
MWAUWASA, viongozi wa mkoa, wizara husika – msimfunike Rais kwa taarifa zisizoeleza hali halisi.
TUNADAI:
- Ratiba ya wazi ya mgao wa maji – kwa maeneo yote. Maana hata mgao wa zamani sasa umepotea hali imekua mbaya kupindukia.
- Kauli rasmi ya TANESCO kuhusu tuhuma za kusababisha tatizo hili.
- uwajibikaji wa viongozi wa MWAUWASA waliotelekeza dhamana yao.
- Uchunguzi huru wa utekelezaji wa mradi wa maji Mwanza – je, kuna hujuma?
- Usawa wa huduma – siyo maji kwa wakubwa tu, wananchi nao ni binadamu.
MAJI NI HAKI YA MSINGI – SI HISANI.
MSITUTESA KWA MRADI TULIOUKARIBISHA KWA MATUMAINI.
WANANCHI WA MWANZA TUNASEMA: IMETOSHA!