Mwarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wapewa kazi ya kuendesha Mabasi ya Mwendokasi

Serikali imedhamiria kusaini mkataba wa ubia na Shirika la Emirates National Group (ENG) lenye makao yake makuu Dubai ili kuendesha usafiri wa mabasi yaendayo haraka Dar (DART) awamu ya 1 mwezi ujao.

ENG chini ya Mkurugenzi Bw. Ahmed Abood Al Boasy (Pichani) inamiliki na kuendesha makampuni ambayo yanashughulika na njia zote za usafiri wa kibinafsi na wa umma, pamoja na huduma zao za ziada.

Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema kuwa ENG ilishinda zabuni hiyo.

Serikali imechukua hatua ya kukaribisha sekta binafsi kuendesha DART ili kuboresha huduma za usafiri mijini kutokana na kasi kubwa ya mabasi kuharibika, kuruka abiria kwenye stendi nyingi za mabasi mbali na vituo vikuu na mabasi mazima kubaki machache.

Mwekezaji huyo atapewa nafasi ya kupewa ruti kwenye awamu ya pili ya mradi iwapo itathibitika kuwa ameweza kuboresha huduma kwa kiasi kikubwa.

Kafulila aliongeza kuwa kuwa mwekezaji mpya anatarajiwa kuleta idadi ya kutosha ya mabasi ili kumaliza msongamano huo.

Kafulila alisema pia kuwa utiaji saini unatarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo, huku ENG ikitarajiwa kununua mabasi na kutoa huduma za usafiri “wakati jukumu la DART litakuwa ni kusimamia mapato.”
Kama wameamua kubinafsisha na iwe total wasimamie uendeshaji,ukusanaji mapato,Admin Yaani walipe gharama za Barbara na Kodi ya serikali basi.Udart wapewe kazi nyingine.
 
Nyerere aliwaamini Wachina kwenye uwekezaji
Mwinyi aliwaamini Wananchi wake kwenye uwekezaji
Mkapa aliwaamini Makaburu kwenye uwekezaji
Kikwete aliwaamini Wazungu kwenye uwekezaji
Magufuli aliwaamini Wahindi na Mawaziri na Ma RC wake waongo uanzishwaji viwanda
Mama Samia anawaamini Waarabu kwenye uwekezaji

Ngoja tuone!
kila zama na kitabu chake
 
Serikali imedhamiria kusaini mkataba wa ubia na Shirika la Emirates National Group (ENG) lenye makao yake makuu Dubai ili kuendesha usafiri wa mabasi yaendayo haraka Dar (DART) awamu ya 1 mwezi ujao.

ENG chini ya Mkurugenzi Bw. Ahmed Abood Al Boasy (Pichani) inamiliki na kuendesha makampuni ambayo yanashughulika na njia zote za usafiri wa kibinafsi na wa umma, pamoja na huduma zao za ziada.

Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema kuwa ENG ilishinda zabuni hiyo.

Serikali imechukua hatua ya kukaribisha sekta binafsi kuendesha DART ili kuboresha huduma za usafiri mijini kutokana na kasi kubwa ya mabasi kuharibika, kuruka abiria kwenye stendi nyingi za mabasi mbali na vituo vikuu na mabasi mazima kubaki machache.

Mwekezaji huyo atapewa nafasi ya kupewa ruti kwenye awamu ya pili ya mradi iwapo itathibitika kuwa ameweza kuboresha huduma kwa kiasi kikubwa.

Kafulila aliongeza kuwa kuwa mwekezaji mpya anatarajiwa kuleta idadi ya kutosha ya mabasi ili kumaliza msongamano huo.

Kafulila alisema pia kuwa utiaji saini unatarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo, huku ENG ikitarajiwa kununua mabasi na kutoa huduma za usafiri “wakati jukumu la DART litakuwa ni kusimamia mapato.”
Jambo jema
 
Kusema kweli ccm haiwatendei haki Watanzania.

Badala ya huyu mwekezaji kupewa haki ya kuendesha huu mradi kwa 100% angelazimishwa atafute patner mzawa ili afanye naye hii kazi. Kwa namna hii tungepata faida 3;
1. Tungewajengea uwezo watu wetu na kuwainua kiuchumi
2. Tungetengeneza ma/tajiri mwingine mzawa
3. Tungekuwa na uhakika huyu mzawa angezungusha hiyo hela yake hapa nchini

Wenzetu Wachina na Wahindi wanafanya hivi kwao. Hawaruhusu wageni kufanya uwekezaji wa 100% bila wenyeji kuhusishwa

Serikali ifikirie kuwahusisha wenyeji kwenye uwekezaji unaofanywa na wageni nchini
 
Mwinyi aliwapa kila kitu waarabu

Kikwete aliwaamini wahindi na waarabu

Nyerere aliwaamini Wachina kwenye uwekezaji
Mwinyi aliwaamini Wananchi wake kwenye uwekezaji
Mkapa aliwaamini Makaburu kwenye uwekezaji
Kikwete aliwaamini Wazungu kwenye uwekezaji
Magufuli aliwaamini Wahindi na Mawaziri na Ma RC wake waongo uanzishwaji viwanda
Mama Samia anawaamini Waarabu kwenye uwekezaji

Ngoja tuone!
 
Nyerere aliwaamini Wachina kwenye uwekezaji
Mwinyi aliwaamini Wananchi wake kwenye uwekezaji
Mkapa aliwaamini Makaburu kwenye uwekezaji
Kikwete aliwaamini Wazungu kwenye uwekezaji
Magufuli aliwaamini Wahindi na Mawaziri na Ma RC wake waongo uanzishwaji viwanda
Mama Samia anawaamini Waarabu kwenye uwekezaji

Ngoja tuone!
Sijui Watanzania tunaweza nini!?

Kichekesho ni kwamba eti tunaweza kuongoza shirika la ndege halafu la town busses tunaishindwa.... 🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom