antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 44,628
- 120,162
Wahindi na wachina wasubiri kwanza, sasa ni zamu ya waarabu kuvunaMwarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wapewa kazi ya kuendesha Mabasi ya Mwendokasi
Wahindi na wachina wasubiri kwanza, sasa ni zamu ya waarabu kuvunaMwarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wapewa kazi ya kuendesha Mabasi ya Mwendokasi
wizi, rushwaKwa lugha nyepesi kabisa ni kwamba ''Watanzania tumeshindwa kuendesha mradi wa Mwendo kasi''
Inashangaza kiasi, inawezekanaje watu binafsi wanaweza kumiliki mabasi na kuendesha huduma za usafirishaji tena ikitumia watu wa kawaida kabisa lakini serikali na taasisi zake na wake wake wasomi wanashindwa kuendesha usafirishaji wa abiria kwenye mji mmoja, tena kwenye njia chache kati ya nyingi za mji huo.
Route:
Mbezi - Kivukoni
Mbezi - Kkoo
Mbezi - Kibaha
Mbezi- Kimara
Mbezi - Morocco
Kkoo - Morocco
Morocco - Kivukoni
Hizi route ni chini ya asilimia kumi ya route za usafirishaji wa abiria hapa Dar.
Nini tunaweza kukifanya kwa ufanisi?
Ni wizi, rushwa, soga, chuki, uongo, uzushi, ngono..............
serikali ya ccm wameshindwa kusimamia mali za umma wapisheSerikali imedhamiria kusaini mkataba wa ubia na Shirika la Emirates National Group (ENG) lenye makao yake makuu Dubai ili kuendesha usafiri wa mabasi yaendayo haraka Dar (DART) awamu ya 1 mwezi ujao.
ENG chini ya Mkurugenzi Bw. Ahmed Abood Al Boasy (Pichani) inamiliki na kuendesha makampuni ambayo yanashughulika na njia zote za usafiri wa kibinafsi na wa umma, pamoja na huduma zao za ziada.
Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema kuwa ENG ilishinda zabuni hiyo.
Serikali imechukua hatua ya kukaribisha sekta binafsi kuendesha DART ili kuboresha huduma za usafiri mijini kutokana na kasi kubwa ya mabasi kuharibika, kuruka abiria kwenye stendi nyingi za mabasi mbali na vituo vikuu na mabasi mazima kubaki machache.
Mwekezaji huyo atapewa nafasi ya kupewa ruti kwenye awamu ya pili ya mradi iwapo itathibitika kuwa ameweza kuboresha huduma kwa kiasi kikubwa.
Kafulila aliongeza kuwa kuwa mwekezaji mpya anatarajiwa kuleta idadi ya kutosha ya mabasi ili kumaliza msongamano huo.
Kafulila alisema pia kuwa utiaji saini unatarajiwa kufanyika wiki mbili zijazo, huku ENG ikitarajiwa kununua mabasi na kutoa huduma za usafiri “wakati jukumu la DART litakuwa ni kusimamia mapato.”
... you have a point! ... mapato yaende hazina moja kwa moja na mkandarasi agawiwe pato kutoka hazina!Kwanini mapato washike DART, huko si kupeleka chui kwenye zizi la mbuzi?
hapo nipakuanzia tu mzee kuwahadaa watanzania, baada ya mda kila kitu anashika yeyeHuyu mwekezaji nae chizi..unawekeza halafu mapato bado wanachukua walioshindwa kujiendesha ?
Tuliwahi sana kupata uhuru sisi, mkoloni hapa angesepa kama 2010 hivi, tungekua fiti kidogoNyerere aliwaamini Wachina kwenye uwekezaji
Mwinyi aliwaamini Wananchi wake kwenye uwekezaji
Mkapa aliwaamini Makaburu kwenye uwekezaji
Kikwete aliwaamini Wazungu kwenye uwekezaji
Magufuli aliwaamini Wahindi na Mawaziri na Ma RC wake waongo uanzishwaji viwanda
Mama Samia anawaamini Waarabu kwenye uwekezaji
Ngoja tuone!
Tofauti itakua ni nini?Hii nchi tuna viongozi wenye mawazo mgando sana, kwanini tunatoa kila kitu chetu kwa wageni bila kujaribu kutoa kwa sekta binafsi wazawa tuone wao watafanye kazi atleast kwa miaka mitatu mpaka mitano?
Wametutega sio ?hapo nipakuanzia tu mzee kuwahadaa watanzania, baada ya mda kila kitu anashika yeye
Taifa lime-collapse.Kwani sisi Wa-Bongo, nini tunachokiweza? Tukisoma chuo tunaona sifa kujiita Daktari, Injinia, CPA, Wakili msomi, Chifu, Mheshimiwa, Mstahiki, Archtecture, Profesa, Komredi, PhD, nk...Lakini kumbe hta mradi wa daladala hatuwezi; kusimamia bandari /viwanja vya ndege hatuwezi, Loh! Nasubiri kuona stendi ya Magufuli nayo wakipewa hao ENG..!!
Mashirika mengi ya serikali na serikali kwa ujumla hakuna ufanisi kwa sababu ya tumbo na ubinafsi kuwa na nguvu kuliko akili na ubunifu, na upendo kwa vizazi vijavyo na hili ni chimbuko kutoka kwenye familia zetu. Ukimwibia mwajiri jamii inakusifia.Kwa lugha nyepesi kabisa ni kwamba ''Watanzania tumeshindwa kuendesha mradi wa Mwendo kasi''
Inashangaza kiasi, inawezekanaje watu binafsi wanaweza kumiliki mabasi na kuendesha huduma za usafirishaji tena ikitumia watu wa kawaida kabisa lakini serikali na taasisi zake na wake wake wasomi wanashindwa kuendesha usafirishaji wa abiria kwenye mji mmoja, tena kwenye njia chache kati ya nyingi za mji huo.
Route:
Mbezi - Kivukoni
Mbezi - Kkoo
Mbezi - Kibaha
Mbezi- Kimara
Mbezi - Morocco
Kkoo - Morocco
Morocco - Kivukoni
Hizi route ni chini ya asilimia kumi ya route za usafirishaji wa abiria hapa Dar.
Nini tunaweza kukifanya kwa ufanisi?
Ni wizi, rushwa, soga, chuki, uongo, uzushi, ngono..............
Education system yetu ni mbovu mkuu, ukitoka hapo viongozi wetu nao ni shida kabisayani bongo hakuna mamlaka ambayo huwezi itoa kasoroKwani sisi Wa-Bongo, nini tunachokiweza? Tukisoma chuo tunaona sifa kujiita Daktari, Injinia, CPA, Wakili msomi, Chifu, Mheshimiwa, Mstahiki, Archtecture, Profesa, Komredi, PhD, nk...Lakini kumbe hta mradi wa daladala hatuwezi; kusimamia bandari /viwanja vya ndege hatuwezi, Loh! Nasubiri kuona stendi ya Magufuli nayo wakipewa hao ENG..!!
Dr Doto, Dr musukuma, Dr Sir -100,Kwani sisi Wa-Bongo, nini tunachokiweza? Tukisoma chuo tunaona sifa kujiita Daktari, Injinia, CPA, Wakili msomi, Chifu, Mheshimiwa, Mstahiki, Archtecture, Profesa, Komredi, PhD, nk...Lakini kumbe hta mradi wa daladala hatuwezi; kusimamia bandari /viwanja vya ndege hatuwezi, Loh! Nasubiri kuona stendi ya Magufuli nayo wakipewa hao ENG..!!