Mwapachu Apewa Tuzo na Kibaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwapachu Apewa Tuzo na Kibaki

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Omutwale, Dec 14, 2011.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aliyekuwa Katibu wa Jumuhiya ya Africa Mashariki Mtanzania Balozi Mwapachu amepewa Tuzo ya Ushupavu na Rais Kibaki ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuanzisha ushuru na soko la pamoja na kuweka misingi ya kuelekea kuwa na sarafu moja. Wakati Kenya ikimtambua na kumtunuku Mtanzania huyu nchi yake ambayo pia ni Mwanajumuhiya haikumuona kuwemo miongoni mwa watu walioliletea Taifa heshima katika utumishi wa Kimataifa uliotukuka juzi ilipokuwa inahadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

  Ni aibu iliyoje jirani zetu wanadhamini mchango ya watu wetu kwenye sherehe zao za Uhuru na kuwatunuku nishani huku sie tukionyesha kutowatambua?
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamaa wala hawatojali kitu!
   
 3. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huu ni uchokozi sasa lol
   
 4. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nimewaza, hivi katika waliopewa Nishani na JK, kuna Mwana-Usalama hata mmoja? Majeshi yetu yamefanya kazi kubwa toka ukombozi, ulinzi wa mipaka ya nchi (Vita ya Kagera) na yametuletea heshima kubwa (Sheli sheli, comoro, etc). Na pia viongozi wake ukiachilia kina Shimbo wamekuwa wavumilivu sana kwa kwa ufedhuli wa viongozi wakuu ambao kama wangesikiliza kelele za walionje, basi nchi hii ingekwisha pinduliwa. Nafikiri ilikuwa vema viongozi wao wangepewa Nishani za heshima ukiachilia mbali zile wanapewa Jeshini.


  Complete story: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/170164-zaidi-ya-suti-wikileaks-yafunua-mgongano-kati-ya-jk-kapuya-na-gen-waitara.html
   
 5. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwapachu alikuwa ana serve interest za waganda na wakenya, ndiyo maana anakubalika huko. Msaliti mkubwa yule wa Tanzania. Alipewa rushwa kuptisha mambo yao mengi. WaTZ walioko humo wanajua!
   
 6. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni vema nasi ukatujuza. Maana Watanzania tumekuwa na ugonjwa wa kuhukumu kila jambo, mafanikio na kila mtu upande hasi bila kutoa ushahidi au maelezo tosherezi. Yawezekana ukawa uko sahihi lakini ni vema ukakamilisha usahihi wako kwa kutoa maelezo toshelezi e.g mifano halisi inayoshindilia tuhuma zako.


   
 7. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Kwa sisi tunaomjua nakwambia Mkuu Omutwale huyo Bwana Mwapachu ni jembe la uhakika, yeye personal ndiye alileta changes nyingi tuu kwenye hii jumuiya ya Afrika Mshariki!!!!!!!!!Kuanzia maslahi ya staff in all categories, sera na mwelekeo wa Jumuiya, Customs Union, Common Markets etc, all these things some one have to be focused!!!!!!!! The man is a mover, motivator and can negotiate to achieve a purpose!!!!!!!!
   
 8. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nami namtambua katika muelekeo huo. Namshangaa The Quonquerer kuleta hoja isiyoshiba juu ya hili Jembe. Labda wacha tumpe muda arejee kutetea na kushibisha hoja yake.
   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Wewe Bwn wacha uongo wako Watanzania gani walioko humo unaowasema????? Kama hujui jambo uliza kwa umakini, kwenye hiyo position yake kama Secretary General wa EAC ALIFANYA MAMBO MENGI SI KWA TANZANIA PEKEE bali kwa wote wenye malengo ya Jumuiya yenye nguvu!!!!!!! Hiyo rushwa alipewa na nani, kwenye mitandao na weak leaks zote isijulikane kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kapewa rushwa???????? Wacha unafiki labda unachukia msimamo wake maana anachukia ufisadi!!!!!!!!!!!!

   
 10. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tuzo zetu waTz zimejaa majungu tu... lazima uwekaribu na mtu fulani au kuwe na pressure ndio upate tuzo.. Big up mwapachu
   
 11. E

  Edo JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ndugu zangu, Kibaki kwa sasa ndiye kachukua usukani wa EAC, na hii tuzo ni kutoka EAC sio Kenya! Kibaki amempa kama kiongozi wa EAC na si kwa mamlaka yake kama Rais wa Kenya. Tanzania haimtambui/kumthamini? si kweli ndo maana alichukuliwa toka sekta binafsi na kuwa Balozi, na baadaye kama nchi ikaona ndiye anafaa kuwa Kinara wa EAC, kazi aliyoifanya vema na kupelekea kupewa hiyo tuzo.
   
 12. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  nimekuelewa sasa,nilidhani tuzo imetoka kwa wakenya,nikajiuliza wakenya hawaoni wakenya wenzao mpaka kutoa tuzo kwa foreigner?
   
 13. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukarimu siku zote huanzia nyumbani, pamoja na kuwa seconded kwenye EAC, Serikali ya Tanzania (Tanganyika) imefanya nini kutambua mchango wa Balozi Mwapachu?
   
 14. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naomba tuweke kumbukumbu zetu sawa.
  [h=1]PRESIDENT MWAI KIBAKI AWARDS AMBASSADOR JUMA V. MWAPACHU MORAN OF THE ORDER OF GOLDEN HEART (MGH). - MO BLOG[/h]http://dewjiblog.com/2011/12/16/president-mwai-kibaki-awards-ambassador-juma-v-mwapachu-moran-of-the-order-of-golden-heart-mgh/December 16, 2011
  [​IMG]
  Ambassador Juma Mwapachu

  During the 48[SUP]th[/SUP] Independence celebrations of Kenya commemorated on 12[SUP]th[/SUP] December 2011, the President of the Republic of Kenya H.E Mwai Kibaki (MP; CGH) awarded Ambassador Juma V. Mwapachu with the MORAN OF THE ORDER OF GOLDEN HEART (MGH). This is the third highest honour accorded by the Government of Kenya to any person.
  The award is in recognition of Ambassador Mwapachu's outstanding performance during his tenure of office as the Secretary General of East African Community, during his tenure he oversaw the implementation of the Customs Union, launched the negotiations of the Common Market Protocol and realized its implementation; launched the on- going negotiations for the establishment of the Monetary Union and put in place a Peace and Security architecture for the East African Community.

  The Management and the Community of UDOM, congratulates Ambassador Mwapachu (MGH) who is the Chairman of the University of Dodoma Council for this deserved high achievement and wish him more success in the future.
   
 15. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,806
  Likes Received: 2,579
  Trophy Points: 280
  It is instructive to see that our neighbours award performance while we award party loyalty.
   
 16. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Big NO with No Thanks!

  Asante sana Kombo.
  Record imewekwa sawa!
   
 17. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Soma tena sasa ili uone kama ulikuwa kweli umemuelewa au alikupotosha!

  Na Je, ulikuwa umemuelewa ama ndo sasa umeelewa!
   
 18. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Pamoja sana Mkuu.
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wote mnaozungumza juu ya kutambuliwa Juma Mwapachu nadhani pengine mngefurahi kama nae angetunukiwa nishani; lakini msishangae kwani Kingunge Ngomale Mwiru aliyemtetea Kikwete kwenye CC mpaka akapata nomination ya kuwa mgombea Urais naye pia hakupata nishani!! There is a lot of mediocrity at our state house.
   
Loading...