QEEN ADEMU1
Senior Member
- Dec 24, 2019
- 134
- 324
USIDANGANYIKE NA MWANZO
Usidanganyike na hatua za mwanzo za mwanzo, hakunaga mapenzi pale vile visimu na viSMS visivyo na idadi visikufanye ukajisahau ukaingia mpaka na viatu vyako.
Hatua za mwanzo za mahusiano zina maigizo mengi sana na mapenzi hayapimwi katika hatua za awali. acha kujidanganya eti week mbili tu ananipenda sana ananipigia simu kila saa ndugu yangu weee bakiza hata viatu usiingie mpaka ukaisahau akili nje.
Viwiki tu vya mwanzo ushaanza kumuita mume wangu, mke wangu; unaona mnapendana sana mpk unajisahau kabisa na kuanza kumkabidhi vitu vyako muda na wakati wowote yupo huru kwako.
Up and downs na solving techniques zenu katika matatizo yanayowakabili ndizo zitakazoonesha how much mtu anajali na ku-care!
Ukiona mtu badala ya kusolve matatizo yanayotokea kwenye mahusiano anakimbilia kusema "Utajua mwenyewe bana", anakwambia hivyo huku anaendelea kuchati na danga lake.
Sijui "Nakwambia huelewi, amaua unachotaka", mara sijui "We ulitakaje?" hata kosa likiwa lake anageuza kibao ujue tu unapoteza muda, yaani anataka hata kama amekosea yeye wewe muda wote umnyenyekee (sijui ina ukwaju ndani!)
Ashamaliza shida yake lolote linalomtoka mdomoni halali yako. Mtu akikupenda anakuwa na kahofu ka kukupoteza; hata kama atakujibu vibaya lakini baadaye atatafuta muda aje akuombe msamaha, ukiona wa hivyo jua anakupenda.
Anakuwa na woga wa kukuacha loose. Sasa kwa week munawasiliana mara mbili alafu unasema niko kwenye mahusiano; ndugu yangu wee, wewe ni single senior -- huna lolote ni heri uchague tu kama mimi kunyoa au kusuka ijulikane mapema kuliko kusema upo kwenye mahusiano yasiyo na miguu.
Bado unaimani unaamini kuwa kuna siku yatarudia tena yale ya mwanzo, mahali popote mnafatana, usipomuona unahisi kama kuishiwa pumzi.
Kuna watu ni waigizaji sana kwenye mahusiano hakutafuti kabisa lakini akiwa na shida utaanza kuona text my mambo, naomba unisaidie nimekwama ukishampa tu humuoni tena mpaka hata week mbili. Kwanini ujitese; safisha phonebook yako acha ubwege, huu ni mwaka wa kufurahia sio wa kulia.



Kuna wanawake wengine wapo wamekubali kuanzisha uhusiano kumbe lengo atunziwe tu watoto ambao alizalishwa na mabaharia. Mwanzo wanaanza na mapenzi motomoto

mpaka mwanaume anajikuta anatangaza ndoa kwa single mother. Subiri watoto wakue wafike drs la iv hivi anaanza kuwasiliana na mabaharia waliomzalisha, kiburi ndiyo kinaanza anaona huwezi tena kumuacha na watoto umeshamkuzishia. Kibaya zaidi unakuta watoto wanaitwa kwa ubini wako! Mapenzi bwana natamani kusema mwanzo unachanganya wengi.Tuwe makini sana na mwanzo, mwanzo usitudanganye. Katika ndiyo huamua hatima ya mapenzi yetu. Kwa wenza mwaka huuu usifanye kosa la kupost post mpenzi wako mtandaoni hawa watu hawaaminiki mara kusi mara shwari muda wowote sunami inaweza kuingia na ukawa umejichoresha pakubwa.
Niwatakie mchana mwema!
Nimesema kwa heri, kama unakubali gonga like na comment.
Sent using i phone x