Mwanzo wa epa katika picha

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,821
2,772
Shukrani sana wana JF kumbe huyu Jeetu Patel alianza siku nyingi sana kuwa karibu na viongozi wetu? Nilipoangalia posts za wenzangu nimeweke hii kama historia fupi ya Mwanzo wa EPA.

Hapa Jeetu Patel anatafuta ushindi kwa Mwalimu ili kwake iwe ni rahisi kufanya anachotaka hasa katika kujipatia fedha haramu. Jinsi mambo yenyewe yalivyo picha hizi zinaashiria kwa watanzania kwamba ni kama vile viongozi wetu wamerogwa.

HAPO MWANZO KULIKUWAPO NYERERE ALIKUTANA NA JEETU PATEL MAMBO YAKAWA HIVI: IKAWA ASUBUHI IKAWA JIONI, SIKU YA KWANZA.

Nyerere patel.jpg


Baada ya Mzee Ruksa kuingia madarakani alkaona sasa kipindi hicho ni cha mavuno maana mambo mengi ni ruksa tu hapo kama sikosei ni Ikulu.

NAYE PATEL AKANENA SEMA RUKSA KWA KILA KITU, YAKAWA KAMA ALIVYONENA. IKWA ASUBUHI IKAWA JIONI, SIKU YA PILI.

View attachment 2122

Hapa tunamuona huyu huyu Jeetu Patel akiwa na mkewe bila kumsahau Mzee wa Uwazi na Ukweli akiwa naye na mkewe wakisherehekea baada ya mafanikio ya UKUSANYAJI MAPATO WA YAO MAKAMPUNI BINAFSI (JMRA) yaani Jeetu and Mkapa Revenue Authority.

PATEL AKASEMA NA TUKUSANYE FEDHA KIWANGO TUTAKACHO, IKAWA HIVYO. AKASEMA NATUCHEZE BAADA YA KUPATA MAFANIKIO HAYO. IKAWA ASUBUHI IKAWA JIONI SIKU YA TATU.

View attachment 2123

Hapa chini JK anakuna kichwa nini atajibu kwa wananchi kwani wananchi wamekuwa werevu sana kwa masuala haya kwa miaka mingi. Miaka mingi wamedanganywa hadi wakaelewa mbinu kijanja za wanasiasa.

KULIVYOPAMBAZUKA WATANZANIA WOTE WAKAPATA AKILI, JEETU AKAPOTEA MACHONI PA WATESWA WAKE. NAO WATESWA WAKASEMA KESHENI MKIOMBA HADI JEETU PATEL AKAMATWE, IKO HIVYO HADI LEO SIKU YA NNE.

View attachment 2124

JEETU PATEL RUDISHA HELA ZETU.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom