Mwanzilishi wa WikiLeakes afungwa jela

Mwanzilishi wa WikiLeakes afungwa jela

wakatanta

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Posts
2,593
Reaction score
3,161
Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange amehukumiwa kifungo jela cha wiki 50 baada ya kupatikana na hatia ya kuruka dhamana nchini Uingereza.

Assange amehukumiwa kifungo hicho leo nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kuruka dhamana na kukimbilia ndani ya ubalozi wa Ecuador mjini London mwaka 2012 akipinga kurejeshwa nchini Sweden anakokabiliwa na kesi ya ubakaji na pia Marekani anakokabiliwa na kesi ya udukuzi.

“Ulikuwa na uamuzi na kitendo ulichochagua kufanya ilikuwa ni kuvunja sheria,” alisema jaji Deborah Taylor alipokuwa akisoma hukumu.

Taylor aliendelea kusema: “Hukujisalimisha kwa utashi wako, haukuja kwa hiyari yako hapa mahakamani.”

Mwanaharakati huyo alikamatwa na polisi wa Uingereza Aprili 11, 2019 baada ya maofisa wa ubalozi wa Ecuador kuwaita polisi wamkamate baada ya kuishi ndani ya ubalozi huo kwa miaka saba.
 
Ingekuwa hapa nchini mkulu angemuagiza hakimu anayetaka kuwa jaji amfunge maisha. Baada ya hapo kingetafutwa kituko apandishwe kuwa jaji.
 
Kesi ya kuruka dhamana afungwe maisha?! Mbona mbowe yuko uraiani!

Alikaa miezi mitatu ndani kwa suala linalodhaminika tena alikwenda mwenyewe mahakamani. Na kesi yenyewe ni ya kubambikiwa na mkulu nyuma ya pazia.
 
Una uhakika alibambikiwa na mkulu? Unaweza kuthibitisha hilo mahakamani?

Mahakama zipi, hizi hizi zinazopokea amri toka juu? Unadhani ukinitishia mahakama ndio nitaogopa? Utendaji wa mahakama zetu za kiafrika hususan hapa kwetu zinaeleweka haziko huru na huwa zinatumika kukomoa wenye mitazamo tofauti na watawala. Habari ndio hiyo.
 
Back
Top Bottom