MWANZA: Zaidi ya wafanyabiashara 12,000 wagoma kuhamia kwenye maeneo mapya waliyopangiwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
Zaidi ya wafanyabiashara ndogondogo 12,000 katika jiji la Mwanza, maarufu kama Machinga, wamesema hawako tayari kuondoka katika maeneo wanakofanyia biashara na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa na halmashauri ya jiji hilo ifikapo Novemba 5 mwaka huu, kufuatia baadhi ya maeneo hayo kuwa na migogoro iliyopo mahakamani na mengine kutokuwa rafiki kwa biashara zao.

Ni tamko la mwenyekiti wa umoja wa Machinga mkoani Mwanza Said Tembo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi wa mazingira ambalo hufanyika kitaifa kila jumamosi ya mwisho ya mwezi.

Baadhi ya Machinga, wameikosoa taarifa ya tathimini ya maeneo ya kuwahamishia iliyofanywa na kikosi kazi cha halmashauri ya jiji la Mwanza kwa madai kwamba ina lengo la kuwanyanyasa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba amewataka Machinga hao kuacha kuupotosha umma juu ya kauli ya rais kuhusiana na zoezi la kuwapanga upya Machinga.

Rais John Pombe Magufuli, akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza Agosti 11 mwaka huu, aligusia suala la Machinga kutohamishwa katika maeneo ya katikati ya jiji hilo na badala yake alitoa muda wa miezi mitatu kwa uongozi wa jiji la Manza kuwaandalia maeneo yenye miundombinu rafiki ya kufanyia biashara zao.

Chanzo: ITV
 
Nikisikia mwanza, shinyanga, Dodoma huwa mshipa wa huruma unakatika acha waisome namba tu
 
Mkuu yeye huwa maneno yana mtoka tu na akisikia makofi na vigelegele ndio huwa anapata mzuka kama msanii jukwaani, anamwaga free style bila kujali athari za ayasemayo. Ana mzuka kama mgombea ubunge wa moro kupitia ACT alipotoa nguo kwa kufurahisha wapiga makofi.
 
Back
Top Bottom