Mwanza wamtaka Kikwete ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanza wamtaka Kikwete ajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 11, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Mwanza wamtaka Kikwete ajiuzulu


  na Mwandishi wetu, Mwanza


  [​IMG] CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU), mkoani Mwanza kimewataka Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha waachie ngazi mara moja kutokana na kashfa ya Dowans na vurugu zilizosababisha maafa na vifo vya raia mkoani Arusha.
  Mwingine ambaye ametakiwa kujiuzulu ni Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema. Wanadai viongozi hao watatu wameshindwa kutimiza vema wajibu wao na maamuzi yao tata yamesababisha maafa ambayo yangeweza kuepukika.
  RAAWU pia imewataka Watanzania kutoogopa wanaposimamia na kutetea haki zao za msingi Kikatiba kwani ni dhahiri kwamba serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeyumba mno na imekosa mwelekeo wa kiutawala.
  Kauli ya RAAWU ilitolewa jana na Katibu wa RAAWU Kanda ya Ziwa, Ramadhan Mwendwa, katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima juu ya mustakabali wa nchi.
  Alisema Rais Kikwete hawezi kukwepa kashfa ya Dowans ambayo sasa serikali inalazimika kuilipa mabilioni ya shilingi wakati maisha ya wananchi yakiwa duni. Dowans ndiyo ilirithi mikoba yaRichmond ambayo ilibebwa na Baraza la Mawaziri chini ya Rais Kikwete na kupewa mradi wa kufua umeme wa dharura huku wakijua kuwa haikuwa na uwezo huo.
  "Sisi RAAWU tunashawishika kuamini kwamba Rais Kikwete ameshiriki moja kwa moja katika mkataba wa Dowans, ndiyo maana ameshindwa kuueleza umma juu ya kampuni hii. Inaonekana hapa kuna mchezo mchafu unafanywa na viongozi wetu... haiwezekani serikali inatangaza kulipa mabilioni ya fedha bila Bunge na Baraza la Mawaziri kuridhia" alisema Mwendwa.
  Aidha, Mwendwa alimmwagia sifa nyingi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwa kukataa Dowans kulipwa mabilioni hayo ya fedha, na kusema: "Waziri Sitta anajua ujanja unaochezwa hapa."
  Vile vile, alihoji sababu ya serikali kuendelea kuilipa kampuni ya IPTL, huku ikilisukumia mzigo Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) lilipe fedha hizo wakati mikataba imesainiwa na serikali.
  Alisema IGP Mwema na Waziri Nahodha wameonekana kushindwa kuwatumikia Watanzania, ndiyo maana idara zao zimeanza kutumia nguvu kwa kuua raia wasiokuwa na hatia.
  "Polisi haina mamlaka ya kupiga risasi na kuua wananchi wanaoandamana kwa amani, tena hawana silaha wala hawajafanya fujo. Kwa maana hiyo, tunataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na IGP Mwema waachie madaraka yao haraka sana" alisema.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145


  Makamba na tambwe hiza watakuja hapa kumsemea bosi wao sasahivi, kwamba hao RAAWU wametumwa na Chadema.

  Mwaka huu tutashuhudia sinema nyingi kweli kweli.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Huu ni mwanzo wa vuguvugu la Bunge kupiga kura ya kukosa imani na JK na serikali yake ya kifisadi...................
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wametumwa na chadema hao.
   
 5. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kikwete akijiuzuru tutakuwa salama maana bado sreikali ipo mkiononi mwa rostam na lowassa mpaka sasa
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni kwamba anatoka JK aningia Dr.Slaa!...Rostam atahamia Canada au Iran!.period!
   
 7. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  100% correct.
  Lakini inabidi hoja hii ipewe msukumo zaidi kwani kuna watu wanasema eti JK impeachment ni mission impossible....tayari kuna thread inaongelea hili.

  Sijui kwa nini watu hatutaki kufikiria nje ya kisanduku (outside te box)?

  Mimi nadhani kuna haja ya ku-mobilize wabunge wapato 20% ya bunge lote (kwa mujibu wa katiba) wawasilishe motion ya impeachment and then we move from there.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  huu sio utamaduni wetu.
   
 9. W

  We know next JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mhh Jamani, katika historia ya Taifa hili,sijawahi kuona uongozi uliopo madarakani ukipingwa kila kona ya nchi na watu wa aina zote. Kwa kweli hapa kuna walakini.
   
 10. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huu ndo wa kwanza. Jiulize mkapa aliingia kwa asilimia ngapi awamu ya kwanza na alitoka na asilimia ngapi awamu ya pili.
  Maana yangu hapa watu hawamkumpenda mwanzo ila utendaji wake ulimpa credit ya kutosha hata watu kutamani katiba itenguke mkuu aweke mambo sawa kidogo.

  Kiukweli Mkwere kachemka, na nchi imemshjinda sema anang'ang'ania na kutaka kufa kiume.

  Hapa hakuna mchawi, atekeleze majukumu yake uone kama kutatokea tatizo. Kama atatekeleza kwa kuwapa watu stahiki zote na kutekeleza wajibu wake kiusawia then tuone kama mawazo haya yatatokea. Yakitokea kweli tutajua uko walakini
   
 11. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Na mimi naunga mkono hao watanzania wa mwanza, JK ajiuzuru kwa kutuingiza kwenye matatizo watanzania. Ni maafa kuichagua ccm tena, hayo ndo matokeo yameanzia Downs, Nauli za dala dala na mabasi, mfumko wa bei nk. sijui kwa nini hawajaachapisha noti za 50000 na 100000.
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Ni kuwa wanataka kumthibitishia JK kuwa pamoja na vijana wao i mean Jeshi la police kutomchagua JK kwenye Uchaguzi uliopita kwa asilimia kubwa bado wanampenda labda ila huu tunajua ni uhuni wa kutaka kuvunja imani kuwa wanajeshi walimchagua JK, Sie twajua ukweli 75% ya majeshi yote kwa wale waliopiga kura walimchagua Dr. Slaa na liko wazi nasikia Juzi katika maandamano huko Arusha maeneo ya Philips lilipita gari la Jeshi JWTZ na wakanyoosha vidole viwili kwa ishara ya chadema na Police wa kawaida hawa wa IGP mwema hawakufanya lolote na wakapita bila kuguswa

   
 13. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JK ajiuzulu aende wapi na nyie huko?
   
 14. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  we kweli akili zako ka za bata
   
 15. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  sio mwanza tu hata mimi.hope watanzania wote pia wanataka iwe hivyo
   
 16. AcinonyxJubatus

  AcinonyxJubatus Senior Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  they are bogus leader, wajiuzulu tuu wala hakuna hasara na kuwakosa in the government
   
 17. B

  BARKMEI Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HUYU MKWERE AJIUZULU!!!!

  ametuletea matatizo mengi sana.
  udini
  dowans
  mgao wa umeme
  mfumuko wa bei
  ufisadi na kuwalinda mafisadi
  migomo vyuo vikuu (shemeji )
  trl kufa
  atcl kufa
  huduma mbovu za afya
  kushindwa kuajiri walimu
  kuua raia kwa amri za kisiasa
   
 18. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Duh! Mkuu noti za laki moja? Kuna watu watapokea noti mbili tu mwisho wa mwezi. Hatari!!!!
   
 19. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wala jk hatasema lolote wapo wengi watajibu ni kweli mkuu. ongeza hapo na salva Rweyemamu
   
 20. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  kikwete hawezi kujiuzulu hata wangekufa watu mia mbili, ccm ni hatari sana.
   
Loading...