RUGAHIMBILA E R
Member
- Mar 5, 2009
- 95
- 34
Kwa kipindi kirefu kumekuwepo na sintofahmu jijini Mwanza hasa katika mtaa maarufu wa Makoroboi ambao hutumiwa na waenda kwa miguu wengi sana jambo ambalo lilikuwa likiwafanya machinga kung'ang'ania kufanya eneo hilo. Sasa baada ya machinga kupewa eneo laStendi ya Tanganyika Bus kwa muda, wahindi wameamua kuweka mageti na kujenga kuta ili kuziba kabisa hiyo Njia.Kwa hiyo inabidi kutafuta njia mbadala. Sasa najiuliza hivi jiji linawezaje kuruhusu kufunga hii njia ambayo iko katkikati ya jiji kwa miaka nenda rudi. Hivi kweli hata waenda kwa miguu bado wana madhara kwa misikiti ya wahindi ambayo tayari imejengewa kuta? Sitaki kuamini kwamba watu wa jiji wamewekwa mifukoni mwa hawa wenzetu.
Update:
Leo Mkuu wa wilaya akifuatana na Mkurugenzi wa Jiji walifika Makoroboi na kutangaza kusitishwa kwa ujenzi wa kuta zilikuwa zikijengwa ili kuziba mtaa huo.
Update:
Leo Mkuu wa wilaya akifuatana na Mkurugenzi wa Jiji walifika Makoroboi na kutangaza kusitishwa kwa ujenzi wa kuta zilikuwa zikijengwa ili kuziba mtaa huo.