Mwanza: Vijana washawishi Madaktari kuwatafutia Wateja wa Figo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Daktari Bingwa wa Magojwa ya Figo, SAID KANENDA amesema kutokana na ongezeko la Magonjwa ya Figo kwa watu mbalimbali hali hiyo imesababisha vijana kushawishika kutafuta wateja wanaohitaji kununua kiungo hicho ili wauze.

Leo Machi 8, 2023 Hospital ya Rufaa kanda ya Ziwa Bugando imefanya upimaji wa Magonjwa mbalimbali bure kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa katika Madhimisho ya Kilele cha Siku ya Figo Duniani.

======

Mwanza. Ukistaajabu ya Musa, utaona ya Firauni! Huo ndio usemi unaofaa kuelezea taarifa za baadhi ya vijana kudaiwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza kutafuta soko la kuuza figo zao.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu ikiwa ni sehemu ya elimu kwa umma kuhusu afya ya figo, Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Figo Hospitali ya Bugando, Dk Said Kanenda amesema wengi wa vijana hao hutaja hali ngumu kimaisha kuwa miongoni mwa sababu za kufikia uamuzi huo unaokinzana na sheria.

"Tunapata watu wengi, hasa vijana wanakuja wakitaka kuuza figo; wengi wanataja hali ngumu kimaisha kufikia maamuzi hayo. Baadhi wanafikia kutushawishi kwa ahadi ya kupata sehemu ya fedha tikiwawezesha kumpata mnunuzi wa figo zao,” amesema Dk Kanenda.eongeza; "Siyo vijana pekee, bali hata baadhi ya wazee wanakuja kuulizia kama kuna uwezekano wa kuuza figo. Tunawaelimisha kuwa hakuna sehemu duniani pa kuuza figo wala kiungo chochote cha mwili, bali pale panapobidi, viungo hivyo hutolewa kama msaada kwa mgonjwa anayehitaji," amesema.

Bila kutaja takwimu za wanaojitokeza kwa mwaka, Dk Kanenda amesema pamoja na kuwakatalia maombi yao, uongozi wa hospitali hiyo huwatumia wataalam wa saikolojia na masuala ya kiuchumi kuelimisha wahusika namna ya kujipatia kipato kwa njia halali.

“Hakuna biashara ya viungo vya binadamu ikiwemo figo kote duniani; na tunawaeleza ukweli huo vijana na wote wanaojitokeza huku tukiwataka kufanya kazi kwa bidii na ubunifu kujiongeza kipato kuepuka vishawishi vya kuuza viungo vyao,” amesema mtaalam huyo.

Wagonjwa wa figo
Akizungumzia ukubwa wa tatizo la figo, Dk Kanenda amesema hospitali hiyo inapokea wagonjwa 115 kila wiki wenye matatizo ya figo wanaohitaji huduma ya kusafisha damu kutokana na figo zao kutofanya kazi kwa ufanisi.

“Kila mwezi tunawapokea na kuwahudumia wagonjwa 600 katika kliniki ya figo. Ni vema jamii ijenge utamaduni wa kupima afya kubaini matatizo na kupata tiba mapema kuepuka madhara makubwa,” amesema.

Ametaja mfumo wa maisha ikiwemo watu kutopima afya mara kwa mara kuwa miongoni mwa sababu za ongezeko la wagonjwa wenye matatizo ya figo nchini ambapo asilimia saba ya wakazi wa vijijini wanabainika kuwa na matatizo la figo huku maeneo ya mijini wakiwa ni asilimia 13.

Akizungumzia kitendo cha baadhi ya watu kujitokeza kutafuta soko la viungo vyao vya mwili, Prosper Frank, mkazi wa eneo la Bugarika jijini Mwanza amewataka vijana nchini kuacha tamaa ya mafanikio ya haraka kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na maarifa ili kujiingizia kipato halali.

"Kuuza figo siyo ni kinyume cha sheria, bali pia ni kujiweka katika hatari ya kiafya,” amesema Frank.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Ashura Songoro aliyewataka vijana kuridhika na vipato vinavyopatikana kwa njia halali badala kutamani mapato ya haraka haraka yanayoweza kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.

Chanzo: Mwananchi
 
Mimi situmii pombe kali na Pombe zote
Sivuti bangi Wala sigara
Siendekezi ngono/Uzinzi
Nina 26 yrs tu
Born in 1997

Kama Kuna Mtu ana mgonjwa naweza msaidia Figo life is about donation and not Duration natamani kufanya kitu Kama hicho kuokoa maisha ya Mtu hapa Duniani .
 
Daktari nae ajiongeze awe Dalali mtu kati Million 50 yeye anakula 25% inayobaki iende kwa Donor ! Au mshahara unamtosha?

Sasa kwa mshahara huo mtu unaendesha lini Range 😂😂😂
Hayo ndo marupu daktari !!!
 
Sio kila figo inafit kwa mtu, lazima zikubaliane ndo mtu anawekewa.
Kama ingekuwa hivyo watu wangekuwa wanauliwa sana na figo kupotea
 
Back
Top Bottom