Mwanza: Tetemeko la ardhi limetokea, Askari mmoja apoteza maisha

wamisako

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
917
871
Leo mchana huu kumetokea tetemeko dogo mkoani Mwanza, Tetemeko liameanza sa 6:56-6:57 limedumu kwa sekunde zisizozidi 40. Watu wengi wameonekana kukimbilia mahala ambapo wanaweza kujistiri.


---------------Update-------------
Tetemeko la ardhi lililopita muda si mrefu limeacha madhara hapa Misungwi kwa kusababisha kifo cha askari mmoja kwa jina la Joyce. Mwili umepelekwa hospitali ya Misungwi
 
Kwa tuliopo Mwanza hivi ni kweli au naota? Mwenzenu Nimehisi katetemeko kakipita
 
Mlioko mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi mwa nchi yetu tunaomba udhibitisho wa hili. Uko mliko pako shwari ama kushaharibika tena

Tujuzeni
 
Kuna hali ya mtikisiko mkubwa imetokea sasa hivi hapa jijini Mza . Je kuna athari yoyote ? Kama ipo tuhabarishane!
 
Back
Top Bottom