Mwanza sehemu gani nitapata kazi

Mwanza sehemu gani nitapata kazi

Unauwezo wa kulea wazee??
Kuna deal la kulea wazee katika kituo cha kulelea wazee
 
Kwa kuanzia Nenda pale mwaloni kirumba. Kuna kazi ya kupakia dagaa kwenye malori, kuna kazi ya kushindilia dagaa kwenye mifuko, kuna kazi ya kushusha mizigo kwenye boti mbalimbali pale.
Ukishapata kamtaji, anza kulangua dagaa kisha kuziuza hapohapo mwaloni hasa wale wa kutoka bukoba-wasikuwa na mchanga
Ukishapata kamtaji pia unaweza nunua smaki na kuwauza
Amka mkuu
Ushauri murua sana huu! Bwana mdogo fanyia kazi kilichotolewa na huyu mdau
 
Naitaji sana kazi kwa muda mrefu sana, ni kijana wa miaka 24 sina kazi kwa muda mrefu sana hadi naelekea kukata tamaa sina mbele wala sina future yoyote elimu yangu ni darasa la saba ila nina sifa ya uelewa naelewa kitu mapema sana. Nipo mwanza wilaya ya ilemela kata ya mecco kusini. Mwenye uwezo wa kunisaidia tafadhari anisaidie nitafanya kazi yoyote yenye kukimu mahitaji
Anza biashara yoyote ya kimachinga
 
Njoo mjini ulizia kampuni hizi za kushusha mizigo gamba gebu friends cargo fulano zipo nyingi sina zinaupungufu mkubwa wa wafanyakazi wa kushusha mizigo kwenye magari ukienda hapo lazima upate kazi nipm nikuunge kama unaona shida kuwafata hao mabosi
 
Njoo Dodoma tufuge kuku
 
samahani kaka ofisi zao hao jamaa ziko mjini sehemu gani
 
Dikson Dumba,
James Dumba,
Stephen Dumba.

Hao Pia ni Ndugu zako au ni wewe
 
Mkuu hii elimu ya darasa la saba umeipatia shule gani? Mbona mwandiko umenyooka hivyo? Usijekuwa unatuletea mambo ya Nyete
 
Back
Top Bottom