DOKEZO Mwanza: Mtoto Mchanga adaiwa kupoteza maisha kwa uzembe wa Nesi, Kituo cha Afya Bulale

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Torra Siabba

Senior Member
Jul 24, 2016
105
102
Iko wazi kwamba Serikali ya Awamu ya Sita dhamira yake ni kuona wananchi wake hawapati shida, lakini cha ajabu ni kwamba Kituo cha Afya Bulale kilichopo Kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza badala ya kuwa msaada kwa Wananchi chenyewe kimegeauka kuwa kituo cha "mauaji".

Ni kwamba February 28, 2023 kuna familia moja ilipeleka Mama mjamzito kwa ajili ya kujifungua baada ya kufika kwenye kituo hicho cha afya walimkuta Nesi ambaye aliwapokea na haikuchukua muda yule dada akapandwa na uchungu, kwa kuwa yule nesi hakuwa na utaalamu wa kutosha ikawa patashika akashindwa kumsaidia ipasavyo ili Mama yule ajifungue.

Kilichotokea ni kwamba wakati wa kujifungua yule dada alikuwa na njia ndogo ya kujifungulia, jambo ambalo mara nyingi mzazi akiwa katika hali hiyo hufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha ya Mzazi na mtoto lakini yule Dada alishindwa kujifungua mpaka yule mtoto aliyetakiwa kuzaliwa akapoteza uhai.

Kwa mujibu wa kaka wa dada aliyepelekwa kujifungua na kupoteza mtoto ni kuwa yule nesi alikuwa hawezi chochote hali iliyosababisha Msiba katika familia hiyo, pia Mganga Mkuu wa kituo hakuwepo.

Uhakika ni kuwa kituo cha Afya BULALE kimekuwa kikilalamikiwa kutokana na kutoa huduma mbovu kwa jamii maana mbali na manesi kutojua wajibu wao hata Daktari anayetegemewa katika hospitali hiyo na yeye anatumia muda mwingi akiwa amelewa nje ya ofisi.

Nimefatilia na kugundua kuwa muda mwingi huyo Mganga Mkuu wa Kituo hata hajali Wagonjwa, sasa hali hii ikiendelea tutapoteza watanzania wangapi?

Iko haja kwa Serikali ya mkoa kupitia mganga mkuu, Mkuu wa mkoa kufanya mabadiliko ya Kiutendaji haraka katika hospotali hiyo ili kuokoa maisha ya wananchi wanaotibiwa pale, maana hata maji ya kusafishia wanaojaaliwa kujifungua au matumizi mengine ni mtihani katika hospitali hiyo ambayo awali ilikuwa zahanati kabla ya kupandishwa na kuwa kituo cha Afya.

Bulale1.jpg

Bulale 22.jpg



UFAFANUZI WA MGANGA MKUU WA MWANZA
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Thomas Rutachunzibwa anaelezea kuhusu tuhuma hizo:

"Kwa tarehe iliyotajwa (Februari 28, 2023) hatujapata ripoti ya kifo, rekodi zinaonesha kulikuwa na wanawake wawili waliojifungua na walikuwa salama, lakini tunaendelea kufuatilia sehemu nyingine.

“Tunapokea taarifa kama hizo kwa kuwa kuna wakati lisemwalo lipo, lakini majibu kama hayo huwezi kupata ndani ya siku moja, inahitaji ufuatiliaji tofauti na angepatikana mtu mmoja ambaye analalamika na kujitokeza hadharani, ikibainika tutachukua hatua.

"Kuhusu madai kama daktari anaingia hospitalini akiwa amelewa na kuna huduma mbovu, hakuna ushahidi wa moja kwa moja.

"Kuanzia taarifa ilivyotoka JamiiForums tumeshaonana na Mganga Mkuu wa Kituo, tumefanya naye vikao, wao wenyewe wanashangaa taarifa imetoka wapi.

“Mrejesho wa Jamii tunaufanyia kazi na kwa kuwa jamii imeshatupa dondoo sisi tunaifanyia kazi, hakuna taarifa ndogo, mrejesho wowote sisi tunaufanyia kazi.”
 
Mhh lkn kule bado watu wengi wanaenda Kamanga, St Clare na pale Mkolani Mbege kuna ki hospital wanahudumia vzuri.
 
Mhh lkn kule bado watu wengi wanaenda Kamanga, St Clare na pale Mkolani Mbege kuna ki hospital wanahudumia vzuri.
Hicho cha Mbege nimepiga sana Kazi baada ya kutoka chuo shida ya hivyo vituo hasa hako Ka Bulale maana ndio Home huko hakuna Staff wa kutosha na competent na GVT yamejikausha tu
 
Hicho cha Mbege nimepiga sana Kazi baada ya kutoka chuo shida ya hivyo vituo hasa hako Ka Bulale maana ndio Home huko hakuna Staff wa kutosha na competent na GVT yamejikausha tu
Ooh sawa sawa lkn hospital nyingi za Gvt ni changamoto sana.
Pale Sekotoure penyewe ni balaa yani wauguzi hawana upendo kabisa.
 
Kile ni kituo kikubwa cha Afya, huduma zikidorola uwekezaji unakua hauna Maana kabisa
 
Ndio maana tunahitaji KATIBA MPYA,hapa katiba mpya ingetupa ofisi ya PP ,huyu ndio kesi zake kama hizi na maamuzi yake yapo binding kisheria, na uamuzi wake ni wa jaji, report yake ni mahakama tu (,full bech)inayoweza kuwa aside uchunguzi wake, tuungane kwenye juhudi ya kuleta katiba mpya
 
Back
Top Bottom