Mwanza: Mangula azomewa kwa aibu

Mwanza: Mangula azomewa kwa aibu

Mkuu Molemo
Unahaha kutafuta udaku na majungu ndani ya uwanja ilikuwa nderemo na vifijo sera za uhakika zilimwaga; 2015 mtachagua wenyewe kipi kinawafaa.
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo maendeleo ni watu wachache wajenge maghorofa kwa hela za EPA MEREMETA na RICHMOND?
ni juavyo mimi maendeleo ni hatua kutoka sehemu fulani na kwenda sehemu nyengine.maendeleo yaweza kuwa hasi au chanya.maendeleo chanya ni kusogea kutoka katika hali duni ki maisha na kwenda kwenye hali yenye afueni kidogo.kuhusu kwamba ni nani kaendelea na nani hakuendelea huo ni mjadala mwengine.
 
tunatamani sana waje huku kusini,sisi tutawamwagia hadi ----- uwawashe mwili mzima.
Mafisadi 2015 wanaona mbali kweli kweli waikabidhi hii nchi kwa watu wenye weledi safi na uliotukuka kiuongozi,sio hawa madhaifu.
 
Mkuu Molemo
Unahaha kutafuta udaku na majungu ndani ya uwanja ilikuwa nderemo na vifijo sera za uhakika zilimwaga; 2015 mtachagua wenyewe kipi kinawafaa.
Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama gazeti la Mwananchi limekuwa la Udaku siku hizi?
 
Last edited by a moderator:
Kama Mwenyekiti wa CCM anasema foleni ya magari Dar ni ishara ya maisha bora, basi siwezi kumshangaa Mangula kwa kauli mfu kama hiyo.
 
ni juavyo mimi maendeleo ni hatua kutoka sehemu fulani na kwenda sehemu nyengine.maendeleo yaweza kuwa hasi au chanya.maendeleo chanya ni kusogea kutoka katika hali duni ki maisha na kwenda kwenye hali yenye afueni kidogo.kuhusu kwamba ni nani kaendelea na nani hakuendelea huo ni mjadala mwengine.
Mkuu kumbe Wizi kwa tafsiri nyingine huko CCM ni Maendeleo? kupakia Twiga na kumpeleka Oman halafu ukapata hela ukajenga Maghorofa hilo nalo ni maendeleo? Kuua tembo wetu ukachukua pembe ukauza ukapate hela halafu ukajenga kiwanda hayo pia ni maendeleo? CCM ni marehemu
 
Njaa mbaya sana, huyu babu bora angeendelea kulima tu kuliko kung'ang'ani hizi siasa!
 
Kiashirio cha kwanza na cha msingi ni kuboreka kwa maisha ya mwananchi wa chini kabisa.
sijauliza ni kipi kiashiria cha maendeleo maana hivi viko vingi na inategemeana na mtizamo unaotumika kuyaangalia hayo maendeleo.mimi nimeuliza yeye anaelewa ni nini maendeleo hata akatae kuwa kujenga si maendeleo.
 
Njaa mbaya sana, huyu babu bora angeendelea kulima tu kuliko kung'ang'ani hizi siasa!

Mkuu Manyi Eti huyu ndiyo wa kupambana na Mpambanaji Dr Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Ina maana maenedeleo ni Magorofa? Na hayo Magorofa yamejengwa na Serikali? Vilaza wa CCM ni wengi sana, sehemu kuna weza kukawa na Nyumba zilizo ezekwa kwa majani lakini kukwa na maendeleo,

Sio utamaduni mzuri kwa wananchi kuwa na tabia ya kuzomea viongozi wao, tabia hii ikiendelea inaweza kujenga kizazi kisichoheshimu Mamlaka. Kwa mantiki hiyo, kutakuwa na uadui baina ya wananchi na viongozi(serikali). Ni vizuri walio madarakani wakafanya tathmini kubaini tatizo limetokea wapi ili lilirekebishwe mapema, kabla hakijaja kizazi ambacho tofauti na kuzomea hakitajitokeza katika shughuli za maendeleo. Aidha, vingozi nao wawe wanashahauriwa kabla ya hotuba zao. Kitendo kuwepo na maghofa Mwanza ni maendeleo kinaweza kisiwe na maana kwa mwananchi wa kawaida ambaye hajawahi hata kuingia kwenye hilo ghorofa, vile vile maghofa hayo unaweza kuta yanamilikiwa na watu wachache sana ikilinganishwa na idadi ya wakazi wa Mwanza. Labda mfano mzuri wa maendeleo ungekuwa barabara ya lami Dar - Mwanza.
 
Mkuu kumbe Wizi kwa tafsiri nyingine huko CCM ni Maendeleo? kupakia Twiga na kumpeleka Oman halafu ukapata hela ukajenga Maghorofa hilo nalo ni maendeleo? Kuua tembo wetu ukachukua pembe ukauza ukapate hela halafu ukajenga kiwanda hayo pia ni maendeleo? CCM ni marehemu
wewe nina uhakika umeelewa unachotaka sasa ni malumbano.
 
Ina maana maenedeleo ni
Magorofa? Na hayo Magorofa yamejengwa na Serikali? Vilaza wa CCM ni
wengi sana, sehemu kuna weza kukawa na Nyumba zilizo ezekwa kwa majani
lakini kukwa na maendeleo,

ajarbu kuchora pyramid ya maendeleo ya wananchi aone figure atakayoipata kama si aibu tupu
 
Ni aibu kubwa kwa Mangula ambaye ni mzoefu wa siasa za Tanzania,ilitakiwa ajipange kabla ya kuanza kusimama majukwaani maana Tanzania ya sasa si ile ya watu kukubali kila kitu wanachoambiwa.
Hili ni funzo kwa wanasiasa wote ambao hawana kitu mbadala cha kuwaambia wananchi ambao fikra zao zimebadilika na wanataka mabadiliko.
 
Nilichoelewa nikuwa hakuna maendeleo yeyote tuliyoyapata tokea tupate UHURU zaidi ya kuua hata vile tulivyoachiwa na Wakoloni kama Reli na Baadhi ya viwanda
ok! sawa. mungu katuumba akili hatufanani.hata tukipewaq mtihani wengine wanapata 90% wengine wana reseat.
 
Ni dhambi na kufuru kusema ccm haikuleta maendeleo katika miaka 50 iliyopita:target:

Mkuu Jomos unajua maana ya maendeleo au umekurupuka kutoka usingizini?

1.Asilimia kubwa ya wananchi hawana uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku hayo ndo maendeleo?
2.Kuishi kwenye nyumba za tende ndo maendeleo?
3.Hospital na vituo vya afya hakuna madawa ilkhali MSD wanatumia mabilion ya fedha za walipa kodi kuteketeza madawa yaliyo expire hayo ndo maendeleo?
4.Utitiri wa secondary za kata zisizokuwa na walimu na vifaa vya kufundishia ndo maendeleo?
5.Jangili mzoefu ambaye ndiye Katibu mkuu wa CCM (Kinana ) kumaliza tembo wetu ndo maendeleo?
6.Rushwa iliyokithiri ndani ya chama na serikali ndo maendeleo?
7.Mikataba tata ya madini ndo maendeleo?
8.Kansa ya ufisadi inayoliangamiza taifa ndo maendeleo?
9.Polisi kuua raia wasiokuwa na hatia ndo maendeleo?
10.Ndege ya jeshi kutua KIA na kupakia twiga wetu na kuwapeleka Uarabuni ndo maendeleo?
11.Watoto wa vigogo kuuza madawa ya kulevya ndo maendeleo?

Mkuu Jomos yakupasa ukasome nini maana ya maendeleo kisha ndo urudi hapa janvini.
 
Ni aibu kubwa kwa Mangula ambaye ni mzoefu wa siasa za Tanzania,ilitakiwa ajipange kabla ya kuanza kusimama majukwaani maana Tanzania ya sasa si ile ya watu kukubali kila kitu wanachoambiwa.
Hili ni funzo kwa wanasiasa wote ambao hawana kitu mbadala cha kuwaambia wananchi ambao fikra zao zimebadilika na wanataka mabadiliko.

Dr Slaa akihutubia wasomi wa vyuo vikuu Mkoa wa DSM alitumia zaidi ya saa 1 na nusu kuhutubia bila kusoma popote.Hotuba yake ilifananishwa na hotuba ya Rais Barack Obama.
 
- sihitaji mtu wa kunishawishi niwaamini.

Hizi zomea zomea hatuoni picha wala sauti za kuzomea
 
Mkuu chama,

Makamanda wa Chadema wanazidi kujichanganya Mkuu Molemo na Mohamedi Mtoi, walianzisha uzi na kusema Gazeti la Mwananchi ni maalumu kwa propaganda za CCM leo wanalitumia kama ushahidi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom