Mwanza: Mangula azomewa kwa aibu

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Makamu Mkiti wa CCM Philip Mangula alionja joto ya jiwe mkoani Mwanza pale msafara wake ulipozomewa vibaya njia nzima tokea alipotoka uwanja wa nyamagana kwenye mkutano wa hadhara.

Aibu hiyo ya zomeazomea iliwakumba pia Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye.

Wananchi walijipanga njia nzima msafara huo ulipopita huku wakionyesha ishara ya vidole viwili na zomeazomea ikishika kasi.

Awali Mangula alihutubia kwa dakika 5 tu kitu kilichowashangaza wengi na swala la msingi alilosema ni kwamba CCM imeleta maendeleo katika kipindi cha miaka 50 kwani zamani Mwanza ilikuwa na ghorofa moja tu la Bugando lakini sasa kuna 'Mabugando' mengi.

Source:Mwananchi Jumatatu.

 
Ina maana maenedeleo ni Magorofa? Na hayo Magorofa yamejengwa na Serikali? Vilaza wa CCM ni wengi sana, sehemu kuna weza kukawa na Nyumba zilizo ezekwa kwa majani lakini kukwa na maendeleo,
 

hahahahaha...mwananchi mara mnaamini stori zao mara mnaponda
 
hii ya mabungando mengi imenichekesha kweli yaani ndiyo uwezo wao wa kufili umekomea hapo, watu wanataka maendeleo ya moja kwamoja unawaonyesha mabugando wakati milo mitatu tabu, elimu duni, afya duni, mahakamani hakuna haki, polisi wanatuwinda watuue badala ya kutulinda...
 
Na hapo bado ,amekaa siku tano na kuambulia zomea zomea. Hajui hata hela za ziara hizi zinatoka wapi.
 
Asante sana mkuu Molemo! Hapa hadi siku nimeianza vyema.. Asante sana kwa taarifa.
 
hahahahaha...mwananchi mara mnaamini stori zao mara mnaponda

pole sana kwa kashi kashi ya wana mwanza jana nasikia mliwapiaga sijui kwanini zoezi la kuwapiga siku ile Arusha mliliacha maana tungewafata mpaka mahoteli kwenu..eti Green Guards nani kawapa kibali cha kupiga na kuua watu,
 
Si jambo la kufurahia sana. Tunajenga kizazi cha watu wasioridhika na uendeshaji wa serikali. Watoto wetu wanajifunza kutoiheshimu na kuithamni serikali bila kupata ufumbuzi wa haraka. Watoto wanaona kwamba serikali ni chombo cha maadui wao. Kwa hakika itakuwa kazi kubwa kuwawajibiosha huko tuendako.
CCM jifunzeni kwa reaction za watu. Huu si upepo tu kama msemavyo, bali ni hali halisi "mnachukiwa sana" kibaya zaidi mnatuharibia sana kizazi tutakachokitawala sisi watu makini.
 
Niliona Nnauye anawaonyesha wazomeaji kidole kama ishara ya kufirwa. Nimemwona kama kiongozi asiye na Busara,akiri na hekima,naomba apewe ushauri nasaha namna ya kuvumilia wananchi pale wapomkataa.
 
Mwanza CCM ilikufa kifo cha mende na tukaizika!
 
Mangula ni sawa na Kumchukua Nelson Mandela kwakua alishawahi kuwa bondia Arudi ulingoni kupigana na Maywether (Dr.Slaa) Leo hii pale MGM Grand..Mangula na Siasa za leo wapi na wapi yaani baada ya kuona sasa kuiba tena Epa hawawezi wamemtuma kinana kumaliza tembo wetu ili wapate pesa za kuhonga wenye njaa...JK aje ajibu yule mtoto wa kigogo wa CCM na Kiongozi wa serikali alikuwa aliyekamatwa China akiuza dawa za kulevya alikuwa nani?na Ccm ilimtuma ili pesa ziende wapi?
 
Ni dhambi na kufuru kusema ccm haikuleta maendeleo katika miaka 50 iliyopita:target:
 
Na hawatajifunza kamwe kutokana na ombwe la kushika utamu. Wakakamate mafisadi na majangili waliopo kwenye chama na serikali, pia warejeshe pesa zetu zilizofichwa nje na kutaifisha Mali za mafisadi hapo tutawaunga mkono 100%.
 



.
.....MWANZA...TUKIAMUA TUNAWEZA......!!!


The Big SHOW (Kusini corridor )


CC LUMUMBA
nyumba ya majangili
 
Ina maana maenedeleo ni Magorofa? Na hayo Magorofa yamejengwa na Serikali? Vilaza wa CCM ni wengi sana, sehemu kuna weza kukawa na Nyumba zilizo ezekwa kwa majani lakini kukwa na maendeleo,

Mkuu Chasha sikujua Mangula hana hoja kwa viwango hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Mayor wa Ilemela hakuwepo atumie vifungu kuwazuia wananchi wasimzomee Mangula?
 

watakuja kukwambia wananchi walikuwa wanawashangilia maccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…