Mwanza: Majambazi yavamia Amazing View Bar Bwiru

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,090
2,000
Ni hekaheka maeneo ya bwiru vitu vimelia kama nusu saa ,ahueni ya kupost imepatikana sasa hivi

Ni kwamba wazee wa ngwasuma a.k.a wazee wa hapa kazi tu walitua katika ile bar mpya inayohit mwanza maeneo ya bwiru mwanzana kufyatua risasi takribani 30 nyingine zimelia kamaa mabomu,sijui ni majambazi ya kisasa hayo jamani.

Baada ya kama dakika kumi na tano police nao walifika na wamepita karibu na ka crib changu cgha kichovu nikiwaona kwa dirishani lakini boxer ikiwa tayari imekwishalowa na mkojo,cha kushangaza policemen wale walikuwa kwenye defender ya kizamani yenye engine inayotoa mlio wa kichovu imewasha taa,wao wako mbele kama sita wakiwa na bunduki(sijaelewa hiyo tactic sababu walikuwa wamejiexpose mno kwa maono yangu)
Na hiyo ni if kama hayo majambazi yalikuwa yamekimbilia chini ya chuo cha mipango maana ndipo polisi walipokuwa wanelekea hadi nikadhani labda majamaa yalikuwa yamepanga kutoroka na boti ziwani

Sina maelezo kuhusu casualty sababu bar ipo meters 200 toka hapa ghetto na sina mpango wa kutoka nawahi bafuni kufua boxer,Plus inasemekana last week yalifika the same place yakastukiwa sababu machine gun ilionekana imechomoza kwenye bag yalivyotiliwa shaka yakasepa, haijulikani ni wivu wa kibiashara haswa ukichukulia bar hiyo ilivyohit au ni issues personal.
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,031
2,000
inawezekana sasa hata kwenda bundesliga nyasaka inabidi tuogope, hata kwa komba pale si walipaua kijinga kwa uvamizi kama huu,ila inaonekana hii ni personal vendetta au kuharibiana biashara
Kwa Komba Medical Research Mianzini mkuu?
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,031
2,000
yup walishalazaga watu pale,kuanzia siku hiyo watu wakakata mguu naona na huyu mama na mmewe wa medical research pia yamewakuta kwenye hiyo bar mpya ya amaizing view
Yalikuaga maeneo yangu ya kujidai hayo wakati wa kujenga Breweries. Mnanunua nyama ama samaki mama Komba anawapikia nguna. Miaka ya 94 95. Tukimaliza jioni tunajisogeza Delux kwa Dj Eddie na Ka milioni halafu tunapitia mbuga za wanyama Kishamapanda kuchukua Compact Disc kujiliwaza nazo usiku.
 

tofyo

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
2,690
2,000
Hapo chuo hao walinzi si wanazo vilevile.ila kama wameshuka huko itakuwa ni mkondo wa kirumba huo.hawawez kwenda ilemela.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom