GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,455
- 108,567
Ni hekaheka maeneo ya bwiru vitu vimelia kama nusu saa ,ahueni ya kupost imepatikana sasa hivi
Ni kwamba wazee wa ngwasuma a.k.a wazee wa hapa kazi tu walitua katika ile bar mpya inayohit mwanza maeneo ya bwiru mwanzana kufyatua risasi takribani 30 nyingine zimelia kamaa mabomu,sijui ni majambazi ya kisasa hayo jamani
baada ya kama dakika kumi na tano police nao walifika na wamepita karibu na ka crib changu cgha kichovu nikiwaona kwa dirishani lakini boxer ikiwa tayari imekwishalowa na mkojo,cha kushangaza policemen wale walikuwa kwenye defender ya kizamani yenye engine inayotoa mlio wa kichovu imewasha taa,wao wako mbele kama sita wakiwa na bunduki(sijaelewa hiyo tactic sababu walikuwa wamejiexpose mno kwa maono yangu)
Na hiyo ni if kama hayo majambazi yalikuwa yamekimbilia chini ya chuo cha mipango maana ndipo polisi walipokuwa wanelekea hadi nikadhani labda majamaa yalikuwa yamepanga kutoroka na boti ziwani
***sina maelezo kuhusu casualty sababu bar ipo meters 200 toka hapa ghetto na sina mpango wa kutoka nawahi bafuni kufua boxer,Plus inasemekana last week yalifika the same place yakastukiwa sababu machine gun ilionekana imechomoza kwenye bag yalivyotiliwa shaka yakasepa, haijulikani ni wivu wa kibiashara haswa ukichukulia bar hiyo ilivyohit au ni issues personal.
Siku zingine usiwe unapenda sana kukimbilia Kulaumu Polisi na hili ndilo tatizo la Watanzania wengi kudhani kwamba Polisi pekee ndiyo wenye ' Jukumu ' kubwa la Kulinda Usalama na Mali zetu lakini kwa wenye akili kisawasawa wanasema kwamba ' Jukumu ' namba moja la Ulinzi wangu Mimi na Wewe ni Sisi Raia Kwanza ambao kwa 85% hadi 99% ndiyo tunaishi, tunakula, tunalala na hadi kucheka nao hao Wahalifu huko mitaani lakini huwa tunashindwa hata ' Kuwaripoti ' huko Polisi.
Ni kweli kwamba Jeshi letu la Polisi kwa kiasi fulani nalo lina mapungufu yake lakini nadhani hata Sisi Raia tuna wajibu vile vile wa kufanya ' Community Police ' halafu tukawa tumewasaidia kwa kiasi fulani hao Polisi kuja kumalizia sehemu itakayobaki ya Kuwakamata kiurahisi hao Wahalifu.
Niwapeni tu pole hao wote waliokumbwa na hiyo kadhia hapo katika hiyo Baa ila kwa uzoefu wangu mdogo sana wa masuala mazima ya Ulinzi na Usalama naweza kusema kwamba mpaka hao Wahalifu / Majambazi wameweza kufika hapo na kama ulivyosema / ulivyotanabaisha kwamba hii ni mara yao ya pili basi kuna uwezekano mkubwa sana Wahudumu wa hapo baadhi yao ' wamechomesha ' na wanashirikiana nao au kuna Wateja ' maarufu ' wa hiyo Baa ndiyo wanachora ' ramani uhalifu ' yote hiyo hadi yanatokea hayo yaliyotokea.
Wahenga hawakukosea kabisa na ule msemo wao kwamba " siku zote Kikulacho ki nguoni mwako ".