Majambazi yavamia kwa bomu, yaua Mkurugenzi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,851
18,951
Majambazi yavamia kwa bomu, yaua Mkurugenzi


Na Suleiman Abeid,Shinyanga

WATU wanaohisiwa kuwa majambazi wamevamia Kiwanda cha kuchambua Pamba na Kusindika Mafuta ya Kula kiitwacho Nsagali Company Ltd. na kumshambulia kwa risasi hadi kufa mmoja wa wakurengenzi wa kiwanda hicho

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Shaibu Ibrahim alimtaja Mkurugenzi aliyeuawa kuwa ni Bw. Kushaha Silanga (24) na kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa 7 usiku huko katika kijiji cha Nyakabindi wilayani Bariadi Mkoani Shinyanga.

Kamanda Ibrahimu alisema kundi la watu 10 wakiwa na bunduki inayohisiwa kuwa ni SMG au SAR lilivamia katika kiwanda hicho kinachomilikiwa na Bw. Emmanuel Gungu baada ya kuvunja sehemu ya ukuta kwa kutumia bomu lililotengenezwa kienyeji.

Alisema baada ya kuingia ndani ya kiwanda hicho, Bw. Kushaha alichukua bunduki yake aina ya shotgun yenye namba a.10462na kuanza kurushiana nayo risasi kwa lengo la kujihami.

Hata hivyo majambazi hayo yalimzidi nguvu kutokana na kuwa na silaha yenye uwezo zaidi kuliko ya kwake na kufanikiwa kumpiga risasi kifuani upande wa kushoto na kufa papo hapo.

Majambazi hayo baada ya kuona, Bw. Kushaha amekufa, yalichukua bunduki na simu yake, pia simu ya mfanyakazi mwingine aliyetambuliwa kwa jina la Bw. Edward Ngwesa ambaye alikuwa amelala chumba kimoja na marehemu.

Kamanda Ibrahimu, alisema Jeshi lake linawasaka majambazi hayo na ametoa mwito kwa raia wema kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi wamuonapo mtu yeyote wanayemtilia shaka.

Habari ambazo hazijathibitishwa zimeeleza kuwa majambazi hayo yalikuwa yamepanga kupora kiasi cha sh. milioni 200 zilizokuwa zimepelekwa kiwandani hapo kwa ajili ya kununulia pamba kutoka kwa wakulima ambazo zilikuwa zimechukuliwa benki.

Hata hivyo hawakuweza kufanikiwa kuzipata fedha hizo ambazo tayari zilikuwa zimesambazwa katika vituo vya kununulia pamba siku moja kabla ya tukio hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom