Jiji la Mwanza likijiandaa kumpokea Mheshimiwa Rais Mama yetu SSH ndio uongozi umekurupuka tangu juzi kuzibua mitaro, kuondoa taka na mchanga, kichekesho zaidi ni Tanesco kufunga bulb za LED za matumizi ya kawaida kwenye nguzo za barabarani anakopitia Mheshimiwa Rais wetu kumhadaa jiji huwa lipo hivyo siku zote. Kiuhalisia jiji huwa ni chafu na lisilo na mikakati ya kutunza taswira na hadhi ya jiji, mama akitaka kujua anafanyiwa sanaa ashtukize ziara za kushtukiza maeneo ambayo hakupangiwa ajionee mwenyewe. Ni vibaya kumhadaa kiongozi wa nchi.