Akipata nafasi tumekubaliana tukutane jioni ya leo nitazungumza nae kwa kina sana hizi hoja (Angalizo:mimi si msemaji wake wala katibu wake ila ni mdau wa maendeleo na kwa bahati Namfahamu Mh Highness nilipata kuishi nae Mwanza).
Moja juu ya barabara na mambo mengine ya jimbo hilo la ilemela,maana hofu yangu ni kurudi jimbo kwa wachumia tumbo wakati tuko kwenye kipindi hiki kigumu cha kuikomboa nchi, sasa kama tumeshapiga hatua 23 nisingependa kurudi nyuma japo hatua moja, kwa namna yoyote,ila nachosisitiza tuwe na mkakati wa pamoja wa kutatua matitizo yetu kwa kuzingatia Participatory process to identify problems/needs and to strategize solutions, to involve team work and multiple stakeholders.
Involvement of communities in the project design and implementation na mambo mengine kama hayo yatakayotusaidi kuwa na njia mbadala kutufikisha kwenye maendeleo ya kweli,na ndio maana nasisitiza mawasiliano baina ya wanachi na waheshimiwa madiwani na wabunge.
Na pale kunapokuwa na sababu za makusudi za kukwamisha juhudi za pamoja za Mbunge na wananchi basi tukatae kwa ku-impose nguvu ya umma kwenye kuyafikia maendeleo.Nasisitiza pia kufikisha kero kwa utaratibu ambao utatusaidia kuwa na refernce ya kumhoji mtu kwa nini hiki au kile hakikutekelezeka.
Hata Mh Highness kwenu nunyi wana Ilemela jengeni umoja wote bila kujali itikadi na kumpa support na ndio maana nikasema mki-document hoja zenu kesho mtamuuliza vizuri na kumsuta vizuri.
Nae anahitajika kutoa mrejesho kwa kila anachokifuatilia au kukisimamia kwa manufaa ya wana Ilemela.natoa wito kwa wananchi wote kuliko na wabunge wa Chadema,sina hakika kwa wabunge wa CCM maana wako kichama zaidi,mshirikiane na wabunge kutatua matatizo yetu,tuwe utaratibu wa ku-officiate hoja zetu ili tuweze kuwapima wabunge wenu kwa utekelezaji wao na kuwe na mawasiliano endelevu.
Ntamaholo nikipata kukutana na Mh Higness nitamshauri awe anapita humu Jukwaani kuokota hoja za watu ama malalamiko ya wapiga kura wake,lakini pia wito wangu nayi mpite ofisi kwa wabunge wetu kufanya,physical contact.