Mwanza: Daladala za Nyasaka Mzunguko, zagoma kutoa huduma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanza: Daladala za Nyasaka Mzunguko, zagoma kutoa huduma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ntamaholo, Nov 23, 2011.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  Wana Jamvi habarini.

  Leo nimerudi na taarifa kamili baada ya kutoa angalizo, ambao wale wanaoshabikia CDM kwa uanfiki waliwaka sana kwa kuwa niliwataja madiwani na wabunge wa CDM hapa mkoani Mwanza.

  Katika thread niliyoanzisha, kuwakumbusha wabunge wangu kuingilia kati matengenezo ya barabara ya NYASAKA-MZUNGUKO, ambapo nilimlaum mbunge kukaa kimya bila kutoa taarifa kwa wananchi juu ya kipande cha kutoka KONA YA BWIRU-NYASAKA/KILORELI.

  Sasa hali imekuwa mbaya zaidi baada ya wiki iliyopita mama mmoja kujifungua BIG BITE akipelekwa hospital. Ni ubovu wa kipande hicho kilichopelekea hali hiyo.

  Leo madereva na matajiri wao, wamegoma kutoa huduma kwa madai kuwa wamechoka na services za magari yao kila siku iendayo kwa Mungu. Sasa nani wa kuwalaumu?

  HIGHNESS KIWIA-Mbunge CDM halaumiki katika hili? kwanza ni kwa kuuchuna, kukaa bila kuwapa taairfa wananchi juu ya hali hiyo, lakini ni kwa kukosa huduma za daldala, ambapo wengi wataumia.

  Kwa kumbukumbu zaidi, naambatanisha na thread ya kwanza ili tujikumbushe mjadala ulivyokuwa.

  NAIPENDA CDM, LAKINI SIWAPENDI VIONGOZI WA CDM WASIOWAJIBIKA KWA WANANCHI, KWANI HAWANA TOFAUTI NA WA CCM TUNAOWAPINGA KILA SIKU.


  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/191520-wenje-na-highness-wabunge-chadema-mwanza-msidhalilishe-chadema.html
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi mwenye dhamana ya kujenga barabara ni serikali au mbunge? Nani anakusanya kodi?
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  mie sikumbana na adha hiyo, kwani niliamka 5:30hrs kuja ofisini, nilipata gari baada ya kutembea hadi kona ya Bwiru, lakini niliona gari mbali za ruti hiyo zikiwa kazini. Taarifa hizi nimezipata toka kwa jamaa yangu aliyechelewa kufika kazini kwa kukosa usafiri hadi aliposhituka na kuchukua pikipiki. Traffic Officers wako eneo hilo, likitokea lolote la msingi nitawajulisha.

   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  '

  anayekusanya kodi ni serikali, lakini anayehakikisha kodi inatumika kwa maslahi ya wananchi ni mwakilishi wa wananchi ambapo ni mbunge/diwani. swali lingine
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Serikali iulizwe kuhusu tatizo la barabara.
   
 6. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  nani wa kuuliza serikali? wananchi au wawakilishi wao?
   
 7. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wewe huna akili kabisa, kwa obwe hili la uongozi uliopo tanzania? atasimamia vipi wakati kila akifanya mikutano, polisi wanamvamia na mahakanani wanamsubiri?
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mwanza, Mwanza nyumbani!!! Vipi diwani wa kata ya maeneo husika anasemaje? Na vipi Mbunge anazo hizo taarifa au ni kulaumy bila baadhi ya watu kuwajibika ipasavyo? Na kama analipewa hizo taarifa, vipi feedback yake ilikuwaje/alisemaje? Je wananchi wa maeneo husika wanajitoleaje kuondoa hii kero katika maeneo yao au ndo mnasubiri kila kitu mbunge awafanyie kama kawaida yetu watanzania?
   
 9. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ntamaholo - Kumbe uko Mwanza? Kama mwananchi mpenda maendeleo wa Mwanza umeshawasiliana na Mbunge mhusika moja kwa moja? au unalalama tu hapa mtandaoni ikiwa ni moja ya njia za ku-decampaign against mbunge? City Council si wako hapo pua na mdomo? Umefikisha malalamiko yako hayo? hao daladala umesikia wamegoma kwa sababu mbunge ameshindwa kuwasilisha kero hiyo au mgomo huo ni namna ya kuungana na mbunge wao kufikisha ujumbe kwa wakusanya kodi na wapanga mafungu?
   
 10. C

  Chechenya Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tingatinga na greada yameonekana site huenda barabara ikarekebishwa
   
 11. j

  jigoku JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nina vyomjua Highness tukiacha unafiki wewe ulieeleta post hii una hoja tena ya msingi sana ila inavyoonekana hoja zako unazileta tu jukwaani sidhani kama umeshakwenda ofisini kupeleka hoja hizi na ukasikia anasemaji,sina sababu ya kumtetea naungana na wewe simpendi kiongozi asietekeleza majukumu yake hasa ya kuwahudumia wananchi.Lakini Highness ukienda kumuona atajua kweli wapiga kura wake na wanaoiunga mkono Chadema wanahitaji utendaji uliotofauti na wa kipindi cha nyuma chini ya CCM.sasa hapa inaonekana unategea aharibu kisha ndo mmseme,tulisema sisi,NO nendeni mkamwambie Mh mbunge hiki mbona kiko hivi,najua atawapokea tu ni kijana ambe namfahamu,sema mimi siko mwanza lakini tungewasiliana kisha tukaenda mtafuta.Nendeni mkamwambie msiisiihie tu kwenye jukwaa.pamoja tutajenga
   
 12. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sasa wewe upo ofisini au barabalani?
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  nashukuru kunipa daraja hilo, siyo mbaya ukijichunguza vizuri. Kwa hiyo aogope? kama kufanya mikutano anaogopa, si atafute kituo kimoja cha redio/tv azungumze na wananchi kupitia media? Viongozi waoga hatuwataki Tanzania. Nadhani kama Lema angekuwa mwoga, CCM wangempa zawadi, lakini kwa kuwa anajua yuko right, na hataki ujanjaujanja, ndo maana kila siku anaandamwa na harudi nyuma mpaka haki ya wana Arusha itakapo patikana
   
 14. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  nipo kazini, umeme ulikatika kidogo nikatoka nje kwenda kuangalia pale TANESCO, zinakoanzia route, sikuona gari hata moja la route hiyo. Nimeona gari moja likitokea POLICE, lakini halikuwa na abiria hata mmoja
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  kwa kijana kama highness, naamini lazima anafika JF kuangalia wananchi tunasema nini. Ni vizuri kufika ofisi kwake na kuwaambia, lakini ninaposhindwa namkumbusha wajibu wake kupitia JF. Mbona mara nyingi yanayomhusu Zitto anajitokeza na kujibu? Highness kama haingii humu, kuna watu wake wa karibu wangemshauri aitishe mkutano na kulijadili suala la kipande kile na wananchi wakajulishwa mchawi nani
   
 16. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  wamegoma kuepuka uharibifu wa magari yao. Kama mbunge, angekuwa amesha toa tamko baada ya thread ile ya kwanza. Lkini kukaa kimya, hakumjengi kisiasa kwani ukiangalia kwenye ilan yake ya uchaguzi huduma za jamii ilikuwa ni moja ya hoja zake, linapotokea kama hivi, lazima tumshitue kwani wananchi waliomchagua ndio wa kwanza kusema, huyu ndiye tuliyemchagua.

  Kama kuna tatizo JIJI, arudi kwa waajiri wake awataarifu kuwa, ukarabati umekwama kwa sababu hizi, awaeleze
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  kama angekuja kwa wananchi, JF ingejulishwa. mpaka sasa ni kimyaa. sijasikia lolote, labda yawezekana kazi imenikeep busy, alipotoa taarifa yoyote mie sikuipata. Lakini Mwanza wananharakati wengi wangetutarifu JF
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  Site ya wapi? niliona moja tu likifanya usafi kwenye eneola soko kwa musuka, baada ya wafanya biashara kuhamishwa kwenye soko jipya lililojengwa
   
 19. j

  jigoku JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ntamaholo kwani siku hizi Mh amehama hapo Selemani Nasoro,unakata kushoto pale dukani kwa lema ,kabla hujapandisha kwa Rutalaka?mbona ni kijana ambae ana-approach nzuri kwa watu?au amebadilika?au huna update maana nasikia kuna ma-greda yapo site.kiukweli post yako imeniuma sana maana sipendi kiongozi wa chadema akiangushe chama na spendi apate lawama za kutokusaidia kutatua kero za wananchi,hebu jaribuni kufika ofisini kwake kisha akirespond vibaya au kama hana anachoona yuko concerned tuambizane wadau,ila namwamini ni mtu makini na nashawishika kufanya nae mwasiliano nijue kulikoni.lakini sipendi utendaji kazi wa chaedama ulinganishwe na CCM,kutawafanya wananchi wawe drastically confused,maana hawatkuwa na kimbilio.Ila tujenge utaratibu wa kuzitumia ofisi hizi za bunge na za madiwani na ikibidi kila hoja inapopelekwa ina kuwa officiated au tunai-document,na mwisho wa siku tupate record ya kile tulichofanikiwa na kile ambacho hatufanikiwa na tuki-identify sababu za kushindwa kwa jambo fulani,na pale juhudi za viongozi wetu hasa wa-chadema wanapokuwa wanakwamishwa na watu wa serikali tushikamane kuwaunga mkono kwa hali na mali,ila nao wabunge wetu na madiwani watupe mrejesho wa kila jambo ili tuweze kwenda swa,muhimu kuwe na mawsiliano ya karibu sana baina ya wapiga kura na waliopigiwa kura hasa kwenye masuala yanahusu umma.
   
 20. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  Pale kwa Lema alikuwepo wakati wa kampeni, kwa sasa nasikia yuko Pasiansi. in case of anything I will let you know
   
Loading...